Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-28 14:49:32    
Mwimbaji wa Tibet Ronzonrja

cri

Mliosikia ni wimbo alioimba Monzonrka "Mandhari ya Ajabu Jiuzhaigou". Huu ndio wimbo uliompatia umaarufu mwimbaji huyo. Kwa wimbo huo alijipatia tuzo ya fedha na sifa ya Mwimbaji Mwanamume Anayependwa na wasikilizaji wengi katika mashindano ya kitaifa ya waimbaji mwaka 2000. Kutokana na jinsi wimbo huo ulivyoenea ndivyo jina la mwimbaji huyo lilivyovuma zaidi miongoni mwa vijana.

Neno "Jiuzhaigou" ni jina la mahali mkoani Sichuan nchini China. Huko kuna vijiji tisa vya Watibet, ni mahali penye mandhari ya kupendeza kimaumbile. Wimbo huo kwa sauti na maneno uliisifu mandhari ya maskani ya mwimbaji huyo.

Mliosikia ni wimbo aliouliotungwa na mwimbaji Ronzonrja "Mandhari ya Ajabu Jiuzhaigou".

Ronzonrja alizaliwa katika ukoo wa wafugaji Watibet, toka alipokuwa mtoto alikuwa anapenda kuimba, alipokuwa na umri wa miaka 16 kwa mara ya kwanza alipanda jukwaani na kuimba, na tokea hapo alikuwa na hamu na tamaa ya kuwa msanii. Baada ya kumaliza chuo cha ualimu, alirudi nyumbani na kuwa mwalimu, na wakati huo alianza kujifunza elimu ya muziki na kujaribu utunzi wake. Mwaka 1994 Ronzonrja alikuwa mwimbaji mkuu wa Kundi la Sanaa la Jiuzhaigou. Baadaye alikwenda kupata mafunzo zaidi katika Chuo Kikuu cha Muziki mkoani Sichuan na kujifunza utungaji wa muziki kwa mtunzi mkubwa Wang Fulin. Tokea mwaka 1991 alianza utunzi wake wa nyimbo, hadi sasa ametunga nyimbo karibu mia moja. Nyimbo zake zimechanganywa kwa mtindo wa kikabila na mtindo wa kisasa na kuwa mtindo wake pekee.

Mliosikia ni wimbo uliotungwa na kuimbwa na Ronzonrka "Mandhari ya Ajabu Jiuzhaigou". Alisema wimbo huo aliutunga kwa makusudi ya kusifu mahali alipozaliwa.

Kuzifanya nyimbo za Kitibet ziwe za kimataifa ni tumaini kubwa la Ronzonrja. Mwaka 1994 alianza kutembea huko na huku mkoani Tibet akikusanya nyimbo miongoni mwa Watibet, na amepata nyenzo nyingi za utunzi wake. Bw. Ronzonrja alisema, atatumia lugha ya Kitibet na mtindo wa kisasa kuimba nyimbo za kikabila ili nyimbo zipokelewe katika nchi za nje. Hadi sasa amerekodi nyimbo nyingi na baadhi zinaimbwa sana na watu.

Mwishoni mwa mwaka 2003 Ronzonrja alitoa sahani sita za nyimbo zake kwa jina la "Mwanangu Mzuri". Sahani hizo zimekusanya nyimbo zake tano alizotunga mwenyewe, uimbaji wa nyimbo hizo ni wa mchanganyiko wa mtindo wa kikabila na wa kisasa.

Hivi sasa, Ronzonrja amekuwa mwimbaji mkuu na mkuu wa bendi ya Ronzonrja. Alisema atajaribu kuifanya bendi yake iwe yenye mchangnyiko wa mtindo wa kikabila na wa kisasa na kuandaa waimbaji wengi mahiri.

Kabla ya kumaliza kipindi hiki, tuburudike na wimbo wake mwingine "Baraka". Wimbo huo unasema, "Nakutakia furaha iambatane nawe. Nakutakia baraka ikuangukie. Pokea furaha na baraka hizo ninazokutakia kwa moyo wangu wa dhati."

Idhaa ya kiswahili 2005-02-28