Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-28 15:07:24    
Mji wa Linxia

cri

Mji Linxia uko kusini magharibi ya mkoa wa Gansu, magharibi ya China. Mji huo ambao uko karibu sana na Lanzhou, mji mkuu wa mkoa wa Gansu si mkubwa. Watalii wakitembea mjini Linxia, popote wanapoenda wanaweza kusikia muziki wa kienyeji "Hua er", pia wanaweza kujihisi kila wakati hali ya uislamu wa kichina, na kuona misikiti mikubwa na midogo zaidi ya 30 iliyotapakaa kwenye mji huo. Kando za njia ni nyumba moja moja zenye kuta za rangi nyeupe zilizoezekwa vigae vya rangi nyeusi, ambavyo milango ya nyumba ilichongwa nakshi, hata matofali ya kauri yaliyochorwa maua ya rangi hutiwa kwenye kuta za matofali. Mjini Linxia makazi mengi ni yasiyo na ghorofa, kila mlango wa nyumba kunapepea msahafu wa kurani ulioandikwa kwa lugha ya kiarabu. Popote unapokwenda unaweza kuona waislamu wanaume waliovaa balaghashia nyeupe na waislamu wanawake wanaovaa baibui za rangi nyeusi, nyeupe au kijani. Na waislamu wazee wanaopiga chesi au kupiga soga mbele ya nyumba zao wanawavutia sana watu macho.

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Beijing Dada Xia Wenxi aliyewahi kutembelea mjini Linxia alimwambia mwandishi wa habari akisema:

Nimepata picha kubwa kuhusu watu wa Linxia ambao wanatilia maanani sana desturi na adabu. Hata katika siku za joto, niliona waislamu wazee wanaopiga soga au kupiga chesi mbele ya nyumba zao kila mmoja huvaa mavazi rasmi, hata ndevu zao hukatwa kwa makini. Na wanawake wa huko wanazingatia zaidi mavazi yao na kuonesha adabu walizo nazo.

Mbali na kabila la wahui, mjini Linxia pia wanaishi watu wa makabila mengine mawili ya wadongxiang na wabaoan ambao wana urithi maalum sana na mila na desturi pekee za utamaduni, lakini ni vigumu kwa wageni kutoka nje kuwatofautisha na wahui na huko.

Chakula cha nyama za kondoo cha wadongxiang ni kizuri na maarufu sana, mzee Ma Fukang mwenye umri wa miaka 63 mwaka huu anaendesha mkahawa mmoja wa chakula cha nyama za kondoo, alisema:

Chakula cha nyama cha wadongxiang kinatofautiana na chakula hicho na makabila mengine kwa upishi wake, sisi huwalisha kondoo kwa chakula kizuri na huwachija wakati wa kuuza nyama zao, hivyo sifa za nyama za kondoo za sehemu yetu ni nzuri zaidi.

Watu wa kabila la wabaoan ni wa vizazi vya waTujue na wamongolia, ambao walihamia Linxia wa mkoa wa Gansu kutoka mkoa wa Qinghai wakati wa karne ya 17. Wanaume wa kabila la wabaoan wanapenda kuvaa ukanda mwekundu na kisu cha wabaoan, wanaonekana ni mashujaa wenye nguvu kubwa. Kisu cha wabaoan hutengenezwa kwa nguvu za mikono kwa taratibu zaidi ya 40 za kikazi.

Mji wa Linxia uko kwenye njia muhimu ya mawasiliano kati ya mikoa mitatu ya Guansu, Qinghai na Sichuan, ambayo ni sehemu yenye maliasili nyingi. Katika sehemu hiyo pia kuna sanaa yenye mtindo pekee ya michongo ya matofali ya kabila la wahui ya Hezhou iliyoanzia karne ya 10. Michongo hiyo ina sura mbalimbali za kupendeza ambayo inaonesha taswira na maonesho mbalimbali, lakini hakuna maonesho ya shughuli za watu, kwani watu wa kabila la wahui wanaamini dini ya kiislamu, na hawaabudu mtu yeyote.

Katika mji wa Linxia wanakoishi waislamu milioni 2, saa za mikono na kengele ni kama mapambano tu, kwani misikiti iliyotapakaa kila pembe la mji huo huadhini mara 5 kwa siku, kuwakumbusha waislam kwenda miskitini kuswali.

Idhaa ya kiswahili 2005-02-28