Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-02-28 15:56:48    
Akili tulivu yavunja mzunguko mbaya wa kulipiza kisasi kwa milipuko

cri

Mlipuko uliotokea tarehe 25 huko tel Aviv ulivunja hali tulivu kati ya Israel na Palestina, na watu walikuwa na wasiwasi kuwa huenda mlipuko huo utaanzisha tena mzunguko mbaya wa kulipiza kisasi kwa milipuko na kuharibu fursa nzuri isiyopatikana kwa urahisi ya kuweza kupata amani. Lakini uvumilivu wa kiakili uliochukuliwa na serikali na wananchi wa nchi mbili umewatia moyo na matumaini kuhusu mchakato wa amani kati ya nchi mbili.

Baada ya mlipuko kutokea huko Tel Aviv, Palestina ilitumia maneno makali yasiyowahi kutumika kulaani tukio hilo. Mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Mahamoud Abbas alisema kuwa aliyeongoza mlipuko huo nyuma ya pazia ni "mhaini", na Palestina hakika itamwadhibu kisheria bila huruma.

Hali ilivyokuwa zamani ni kuwa, kila mlipuko ukitokea nchini Israel, vikundi vyenye siasa kali vya Palestina vilijitokeza na kutangaza kuhusika, na kwa juhudi hutukuza mambo ili kujiletea umaarufu. Lakini mara hii baada ya mlipuko kutokea, kinyume cha kawaida ya zamani, vilikana kuhusika na mlipuko huo. Vyombo vya habari vinaona sababu ni kuwa, mabadiliko makubwa yametokea nchini Palestina. Baada ya Abbas kushika madaraka, hali kati ya Palestina na Israel imetulia. Baada ya Abbas kufanya juhudi kubwa Israel imekubali kuacha masharti mengi na jumuyia ya kimataifa imeanza kuisaidia Palestina kisiasa na kiuchumi. Wananchi wa Palestina wanaona kuwa sera ya Abbas ya kutetea kufanya mazungumzo ya amani inafaa na wamejawa na imani na sera yake. Wakati watu wa Palestina karibu watafaidika na "matunda ya amani" kuzushwa kwa mlipuko huo kunakwenda kinyme na tumaini la Wapalestina.

Kadhalika, Israel pia ilichukua msimamo ulio tofauti na wa zamani na kuwa kimya. Kama mlipuko huo ungetokea zamani Israel ingechukua hatua ya kulipiza kisasi mara moja, kubomoa makazi ya watu wa Palestina na "kuwafyeka viongozi wa vikundi vyenye siasa kali" na kuwakamata watu wengi wenye silaha, lakini mara hii Israel haikuchukua hatua hiyo, bali kusimamisha tu shughuli za kukabidhi miji ya kando ya magharibi ya Mto Jordan na kuishinikiza Palestina kidiplomasia ichukue hatua ya kupambana na vikundi vyenye siasa kali. Vyombo vya habari vinaona kuwa Israel imechukua "msimamo adimu" wa kiakili na kuiomba serikali "imwachie muda mrefu zaidi na imvumilie zaidi Bw. Abbas".

Uvumilivu wa Israel unatokana na sababu tatu: Kwanza, viongozi wa Palestina na wananchi wote kweli wana nia ya kutaka amani, na juhudi kubwa za Palestina za kupambana na vikundi vyenye siasa kali zinajulikana kwa wote, kama Israel ingechukua hatua za kulipiza kisasi hakika itabeba lawama kwa kuharibu mchakato wa amani; Pili, hali ilivyo imethibitisha kuwa ni kwa kushirikiana tu na Palestina iliyokuwa na nia ya kweli ya kutaka amani, ndio usalama wa Israel unapoweza kuhakikishwa. Mapambano ya kijeshi yasiyo na mwisho hayasaidii kitu bali yanaharibu sifa ya Israel. Tatu, kutokana na mkakati wa Mashariki ya Kati, Marekani inataka Israel ivumilie uchokozi wa vikundi vyenye siasa kali ili kukwepa hali kuzidi kuwa mbaya.

Hata hivyo, ingawa Israel haikutumia "fimbo nene ya kijeshi" lakini pia haikuahidi kuacha hatua yake ya kulipiza kisasi kwa nguvu za kijeshi. Israel mara nyingi imetangaza kuwa, kama Palestina haitakuchukua hatua dhidi ya vikundi hivyo, Israel itasimamisha mazungumzo na Palestina na kuchukua hatua kali za kijeshi.

Wachambuzi wanaona kuwa katika muda wa miaka minne ya migogoro, hali ya "mlipuko mmoja kuweza kusababisha mzunguko mbaya wa kulipiza kisasi" iliwahi kutokea mara nyingi. Uvumilivu uliochukuliwa sasa na pande mbili ni muhimu katika kuvunja mzunguko huo mbaya na kuweza kuanzisha mchakato wa amani.

Idhaa ya kiswahili 2005-02-28