Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-01 14:43:47    
Msukosuko wa kisiasa nchini Lebanon wazidi kuwa mbaya

cri
    Kutokana na shinikizo kubwa la chama cha upinzani na waandamanaji, serikali inayoongozwa na Omr Karami ilijiuzulu tarehe 28 Februari. Msukosuko wa kisiasa uliosababishwa na kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani hayati Hariri umezidi kuwa mbaya. Wachambuzi wanaona kuwa kama vikundi mbalimbali vya kisiasa havitapata njia ya kutuliza wasiwasi huo kwa haraka, huenda vita vya wenyewe kwa wenyewe vikazuka tena nchini Lebanon.

    Kwenye mkutano wa bunge uliofanyika siku hiyo wabunge wa upinzani walishutumu vikali wakisema serikali lazima ichukue jukumu la kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani Hariri na kuitaka serikali hiyo ijiuzulu. Waandamaji elfu kadhaa walifanya maandamano mjini Beirut bila kujali marufuku iliyopigwa na serikali. Kutokana na shinikizo kubwa siku hiyo jioni serikali ya Karami ilitangaza kujiuzulu ili kukwepa serikali yake isiwe kikwazo cha maendeleo ya taifa.

    Jioni ya siku hiyo rais wa Lebanon alikubali ombi la kujiuzulu kwa serikali, na kusema kuwa ataitisha mkutano wa kitaifa wa masikilizano na vikundi mbalimbali vya kisiasa na ili kuanzisha serikali mpya.

   Baada ya serikali ya Karami kujiuzulu, viongozi vya vikundi vya upinzani na waandamaji walisherehekea ushindi wao katika mapambano yao dhidi ya serikali, na walitoa wito kwa wananchi waendelee na harakati zao mpaka ukweli kuhusu kifo cha Hariri ufichuliwe na jeshi la Syria liondoke kutoka Lebanon.

    Serikali ya Syria imesema, kujiuzulu kwa serikali ya Lebanon ni jambo la ndani la nchi hiyo na imekataa kuzungumzia lolote kuhusu tukio hilo. Lakini ikulu ya Marekani inafurahia tukio la kujiuzulu kwa serikali hiyo na inahimiza kuundwa kwa "serikali inayoweza kuwakilisha wananchi wa Lebanon" haraka iwezekanavyo.

    Wachambuzi wanaona kuwa kujiuzulu kwa serikali ya Karami kutaathiri hali ya nchi ya Lebanon na Mashariki ya Kati.

    Kwanza, Lebanon ni nchi yenye utata wa matatizo ya kidini na ya kikabila. Katika miaka mingi iliyopita vikundi mbalimbali vilikuwa vikipigana vikali, na nguvu za nje pia hazikuwahi kuacha kutia mkono katika mambo ya ndani ya nchi hiyo. Katika miaka ya 70 ya karne iliyopita kutokana na mivutano mbalimbali vita vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka na kudumu kwa zaidi ya miaka 10, na nchi hiyo imekuwa uwanja wa mashindano ya kisehemu na mataifa makubwa. Mwaka 2000 baada ya jeshi la Israel kuondoka kutoka nchi hiyo, nguvu za kikabila ziliongezeka, na kuwa nguvu kubwa katika msukosuko huo. Lakini wachambuzi wanaona kuwa nguvu za vikundi vya upinzani sasa bado hazijawa imara, mambo yanawezekana kwenda kinyume na matarajio yao, na msukosuko huo wa kisiasa pengine utashindwa kudhibitiwa.

    Pili, baada ya serikali ya Karami kujiuzulu, uhusiano kati ya Syria na Lebanon utakuwa muhimu katika kuamua hali ya kisasa nchini Lebanon. Vikundi vya upinzani siku zote vinang'ang'nia jeshi la Syria liondoke kutoka Lebanon na kuondoa wapelelezi wake nchini humo ili Lebanon itimize uhuru wa kweli wa taifa. Ingawa vikundi hivyo mara nyingi vinadai kuwa harakati zao za kupinga serikali kwa njia ya amani na hazitakiuka "mkataba wa Taif", na "zitarekebisha tu uhusiano na Syria, wala sio kutaka kuwa maadui wa Syria". Lakini kwa makadirio Syria haitaridhisha matakwa ya vikundi hivyo. Rais wa Syria alisema kuwa aidha kutoka "teknolojia" au kutoka "mkakati" Syria haitaondoa jeshi lake kutoka Lebanon.

    Na mwisho, kutokana na mabadiliko ya hali ya Mashariki ya Kati, kubadilisha hali ya siasa ya Lebanon na kutenganisha Syria na Lebanon ili kushinikiza Syria na Iran na kuzilazimisha nchi hizo mbili zishirikiane na Marekani limekuwa suala muhimu la Marekani katika sera yake ya mambo ya nje. Kwa hiyo ushindi wa mwanzo wa vikundi vya upinzani vya Lebanon pia ni mafanikio ya Marekani katika utenganishaji wake. Kama Lebanon itapita muda huo wa msukusuko salama na kuitisha mkutano wa kitaifa wa masikilizano na kuanzisha serikali mpya, itadhoofisha taathira ya Syria kwa Lebanon na hata italegeza msimamo wa Syria kwa Lebanon. Lakini kama msukosuko huo usipoweza kudhibitiwa au hata kuzusha vita vya wenyewe kwa wenyewe, vikundi vinavyoipendelea nchi za Magharibi vitategemea nchi za Marekani na Ufaransa kumaliza matokeo mabaya ya msukosuko huo, na hali ya Lebanon itakuwa ya utatanishi zaidi.