Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-02 14:36:22    
Mtu aliyeathirika katika uwezo wake wa kuongea hana matatizo katika uwezo wake wa kufanya hesabu

cri

Mtaalam wa lugha Bw. Jomsky anaona kuwa uwezo wa binadamu kuhusu lugha ni uwezo wa kimsingi, ambao ubongo wa binadamu unautumia kutekeleza majukumu mbalimbali yanayohusika na sarufi yakiwemo ya hisabati. Wataalam pia wanachukulia kuwa ubongo wa binadamu unatumia rasilimali za ufahamu za namna moja kuhusu kuongea na hisabati. Lakini utafiti mpya wa wanasayansi wa Uingereza umetoa changamoto kwa maoni hayo ya jadi.

Mtaalam wa neva wa Chuo Kikuu cha Seferde Rosmary Wally baada ya kufanya utafiti kuhusu wagonjwa watatu waliopoteza uwezo wa kuongea aliona kuwa wagonjwa hao walishindwa kuongea, lakini walielewa "kanuni za sarufi" za hisabati. Kushindwa kuongea ni upungufu wa uwezo wa kuongea kwa kusababishwa na kiharusi na kujeruhiwa sehemu ya ubongo, ambapo wagonjwa wanashindwa kuelewa na kutumia misamiati. Wagonjwa hao watatu walikuwa kati ya umri wa miaka 50 na 60, walielimika vizuri, na mmoja kati yao alikuwa Profesa wa chuo kikuu.

Utafiti unaonesha kuwa wagonjwa hao watatu walishindwa kuelewa uhusiano wa kisarufi kwenye sentensi rahisi. Kwa mfano, katika maneno ya "wavulana wanawaandama wasichana", walishindwa kufahamu nani walitenda na nani walitendewa, na walishindwa kuitofautisha sentensi hiyo na sentensi nyingine ya "wasichana wanawaandama wavulana". Watafiti walionesha uhusiano unaofanana na nani aliyetenda na nani aliyetendewa kwa kutumia njia ya hisabati kama vile "9030" na "3090", hata walitumia kama "90-[(3+17)x3]" ambayo ni uhusiano mgumu wa kihisabati ulio kama kueleza kwa muundo wa kisarufi wa "mtu huyu alimwua simba mwenye hasira". Utafiti ulionesha kuwa ingawa wagonjwa hawakuweza kueleza kwa maneno, lakini waliweza kufanya hesabu kwa usahihi kwa kutumia kalamu kwenye karatasi. Ingawa walishindwa kuelewa maana ya maneno ya "tatu" na "tisini", lakini hawakuona matatizo baada ya "tatu" na "tisini" kubadilishwa kuwa tarakimu.

Rosmary Wally anaona kuwa utafiti huo unaonesha kuwa kutumia uwezo wa wagonjwa wa kuelewa "sarufi ya hisabati", huenda ataweza kuwasaidia kupata njia ya kuelewa maneno waliyoambiwa au yaliyoandikwa kwenye karatasi.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-02