Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-02 16:39:08    
Mtu wa Beijing aliyechaguliwa kuwa mbunge wa New Zealand

cri

Tarehe 27 mwezi Novemba mwaka 2004, wa-new Zealand wenye asili ya China wanaoishi nchini New Zealand walifurahi sana, na magazeti yote ya kichina ya nchi hiyo yalitoa habari moja kwamba, Bw. Wang Xiaoxuan alichaguliwa kuwa mbunge wa New Zealand. Siku hiyo katika mkutano na waandishi wa habari, balozi wa China aliyeko Auckland alipongeza kuwa, Bw. Wang Xiaoxuan alizaliwa huko Beijing, mji mkuu wa China, yeye ni mnewzealand mwenye asili ya China wa pili kuchuguliwa kuwa mbunge wa New Zealand, na pia ni mbunge wa kwanza wa New Zealand kutoka China bara.

Bw. Wang Xiaoxuan alifika New Zealand alipokuwa ana umri wa miaka 31, katika miaka 18 iliyopita, kutokana na jitihada kubwa, alianzisha kampuni ya matangazo na ukuaji wa masoko, ambayo ilikua kwa haraka. Katika uchaguzi alipata imani ya wapiga kura, hasa wapiga kura wenye asili ya China wanaoishi nchini humo. Hivyo alifanikiwa kuingia kwenye siasa za New Zealand.

Bw. Wang Xiaoxuan alisema kuwa, alipaswa kudumisha akili timamu, kwa kuwa akiwa mbunge wa New Zealand alikuwa anapaswa kuzingatia maslahi ya wanewzealand wenye asili ya China wanaoishi nchini humo, atafanya kazi kwa bidii ili kuwasaidia wachina na kutoa mchango kwa ushirikiano na maingiliano kati ya China na New Zealand.

Kwenye mahojiano, Bw. Wang alimwambia mwandishi wa habari kuwa, katika maisha yake kulikuwa na nafasi mbili ambazo zimeleta mabadiliko makubwa. Kwanza ni kujifunza uchoraji, hii iliweka msingi mzuri wa kazi yake katika siku za baadaye, na nyingine ni kuingia kwenye sekta ya siasa, alipochaguliwa kuwa mbunge alikuwa na umri wa miaka 50.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge nchini New Zealand, Bw. Wang alikuwa anashiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii za New Zealand, na pia alijitahidi kuwahudumia wanewzealand wenye asili ya China wanaoishi nchini humo. Mwaka 1993 alianzisha jumuia ya Zhonghua pamoja na watu wengine, hii ni jumuia yenye athari kubwa huko Auckland, mafanikio makubwa yalipatikana katika maslahi ya wanewzealand wenye asili ya China na jumuia yao. Mwaka 2000 na 2001 alikuwa mwenyekiti wa jumuia hiyo kwa vipindi viwili.

Hadi sasa Bw. Wang Xiaoxuan amekuwa anafanya kazi katika Bunge la New Zealand kwa miezi kadhaa. Kila Jumatatu hadi Alhamisi alikwenda Wellington na kurudi nyumbani siku za mwisho wa wiki. Alisema kuwa, zamani alikuwa anaangalia Bunge la Taifa kutoka nje, lakini sasa akiwa mbunge alijisihi wajibu wake mkubwa na matarajio makubwa ya wapiga kura hivyo anapaswa kufanya kazi kwa bidii zaidi. Baada ya miezi sita Bw. Wang Xiaoxuan atashiriki kwenye na uchaguzi wa bunge kwa mara nyingine. Kuhusu jambo hilo, ana imani kubwa, kwani wanewzealand wenye akili ya China walioishi nchini humo wanamunga mkono sana.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-02