Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-02 16:47:52    
Umoja wa Mataifa wachambua hali na mapambano dhidi ya dawa za kulevya duniani

cri

Shirika la Udhibiti wa Dawa za Kulevya Duniani mnamo tarehe mbili Machi ilitoa "ripoti ya mwaka 2004". Baada ya kuchmbua hali ilivyo ya dawa za kulevya duniani, ripoti hiyo imependekeza nchi zote zidhibiti dawa za kulevya kwa kuunganisha pamoja utoaji na mahitaji, hatua hii ndio inayoweza kuleta mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Ripoti hiyo inasema kuwa utoaji na mahitaji yanaonekana kama mambo mawili yasiyohusiana, lakini kwa kweli ni mambo mawili yasiyoweza kutenganishwa. Mahitaji ya dawa za kulevya yanachochea utoaji wa dawa hizo, na utoaji wa dawa hizo unasaidia mahitaji kuongezeka. Hivi sasa nchi nyingi zinatilia mkazo katika kukomesha usafirishaji wa dawa hizo, njia hii inaleta mafanikio ya muda tu lakini si ya muda mrefu. Uzoefu umethibitisha kuwa mkakati wa kuunganisha mambo yote mawili kwa pamoja, utoaji na mahitaji, ndio njia pekee inayofaa zaidi katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya. Kwa hiyo ripoti hiyo inatoa ushauri kwa kila nchi iweke muundo wa kuunganisha mambo hayo mawili katika mapambano.

Kuhusu hali ya dawa za kulevya duniani, ripoti inasema kuwa Afghanistan ni nchi kubwa duniani inayozalisha kasumba, kilimo cha kasumba katika nchi hiyo kinaimarika zaidi badala ya kupungua, na maeneo ya kilimo hicho yaliyokuwa hekta elfu 80 mwaka 2003 yaliongezeka hadi hekta elfu 130 mwaka jana. Tani 4200 za kasumba zilizalishwa nchini humo mwaka jana ambazo ni zaidi ya robo tatu ya kasumba iliyozalishwa dunia nzima. Tatizo la kulima mazao badala ya kasumba ili kutatua tatizo la maisha ya wakulima halikutatuliwa kwa muda mrefu. Uchukuzi, uzalishaji na uendelezaji wa dawa za kulevya unatawala nchi hiyo kichumi, kiutamaduni na kisiasa na zao hilo limekuwa tishio kubwa kwa nchi hiyo katika ujenzi wa mfumo wa kidemokrasia, utulivu wa kisiasa na ufufuaji wa uchumi. Mbele ya hali hiyo, Afghanistan imeweka mkakati wa kitaifa wa kupambana na dawa za kulevya kwa lengo la kukomesha kabisa uzalishaji na uchukuzi katika muda wa miaka 10. Idara husika za Umoja wa Mataifa zimekuwa zikishirikiana kuiunga mkono Afghanistan kutimiza lengo hilo.

Ripoti inasema, kampeni ya kupambana na dawa za kulevya katika bara la Amerika ya Kusini ni muhimu sio tu kwa bara hilo, bali kwa sehemu nyingine duniani. Uzalishaji wa cocaine barani humo unafikia tani 655 kwa mwaka na asilimia 90 zinasafirishwa kwenda sehemu nyingine kupitia bahari. Mwaka jana baadhi ya nchi za Amerika ya Kusini zilishirikiana na kufanikiwa kuvivunja vikundi 8 vya kueneza dawa za kulevya na kudhoofisha vikundi 7, mafanikio hayo ni ya kufurahisha.

Aidha, ripoti inasema, Marekani ni soko kubwa la dawa za kulevya duniani. Ingawa idadi ya wanafunzi wa sekondari wa Marekani wanaotumia dawa za kulevya imepungua katika miaka ya karibuni, lakini matumizi ovyo kwa ajili ya matibabu yamekuwa suala kubwa lililojitokeza karibuni nchini humo. Katika bara la Ulaya, watu wanaotumia bangi ni wengi. Katika muda wa miaka 10 iliyopita hali ya kutumia bangi ilishamiri. Mwaka jana kwa makadirio, walikuwako watu milioni 28.8 yaani asilimia 5.3 ya watu wote wa Ulaya waliwahi kutumia bangi, chanzo cha suala hilo ni kuwa baadhi ya watu wa Ulaya wanatangaza kwamba kasumba haina madhara kwa afya.

Kadhalika, mauzo haramu ya dawa zinazodhibitiwa katika maduka ya dawa kupitia mtandao wa internet yanaongezeka. Sababu ni kuwa kama duka fulani linalouza dawa hizo kinyume cha sheria likishukulikiwa kisheria katika nchi yake, duka hilo "linahamia" nchi nyingine kwa urahisi. Ripoti inatoa wito kwa kila nchi ipeleleze na kuadhibu maduka kama hayo.

Shirika la Udhibiti wa Dawa za Kulevya Duniani lilianzishwa mwaka 1991 kwa idhini ya Umoja wa Mataifa, kazi yake muhimu ni kusimamia madawa na dawa za kulevya duniani.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-02