Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-02 16:52:21    
Namna ya kupika figili na mizizi ya yungiyungi

cri

Mahitaji

Figili gramu 250, mizizi ya yungiyungi yenye rangi nyeupe, chumvi vijiko 2, unga wa nyama ya kuku kijiko moja, mvinyo wa kupikia nusu kijiko, na mafuta gramu 10

Njia

1. Osha figili, na uikate kishazari iwe vipande, vipakue ndani ya bakuli na tia chumvi kijiko kimoja.

2. chambua mizizi ya yungiyungi na uioshe.

3. mimina maji ndani ya sufuria, chemsha, tia vipande vya figili na mizizi ya yungiyungi, chemsha tena, ipakue, na uipooza kwa maji baridi.

4. pasha moto na tia mafuta ndani ya sufuria, mpaka yachemke, tia vipande vya figili na mizizi ya yungiyungi, koroga, tia chumvi, unga wa nyama ya kuku, mvinyo wa kupika, korogakoroga na kisha upakue. Sasa chakula hiki kiko tayari kuliwa.