Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-02 17:46:55    
Jokofu lisiloleta uchafuzi kwa mazingira na linalotumia umeme kidogo linapokewa na wateja wa China

cri
    Jokofu lisiloleta uchafuzi kwa mazingira na linalotumia umeme kidogo linapokewa na wateja wa China siku hadi siku. Jokofu likiwa ni moja ya mahitaji, limeanza kutumiwa na watu wa kawaida wa China, lakini majokofu mengi yanayotumika hivi sasa yanatumia umeme mwingi na kutoa hewa inayoongeza ujoto duniani. Ili kutatua matatizo hayo, katika miaka ya karibuni, serikali ya China imekuw ikiwahamasisha watu watumie majokofu yasiyoleta uchafuzi kwa mazingira na yanayotumia umeme kidogo. Hivi sasa, wateja wengi wa China wanachagua majokofu ya aina hiyo.

    Bibi Qian Changxia, mwenyeji wa Beijing, siku za karibuni alinunua jokofu, Bibi Qian alimwambia mwandishi wa habari akisema:

    "Jokofu jipya nyumbani kwangu sio tu linaonekana kuwa ni zuri, bali pia halileti uchafuzi kwa mazingira na linatumia umeme kidogo. Sisi sote nyumbani tumeridhika nalo."

    Bibi Qian alisema kuwa jokofu hilo jipya linatumia umeme kidogo zaidi kwa asilimia 50 kuliko jokofu lake la zamani ambalo lilikuwa limefanya kazi kwa muda wa zaidi ya miaka 10, hivyo ameokoa pesa nyingi za matumizi ya umeme, kutokana na hali hiyo, jokofu la aina hiyo ni zuri zaidi kiuchumi ingawa bei yake ni kubwa kuliko majokofu mengine ya kawaida.

    Hivi sasa, majokofu yanayouzwa kwenye soko la China karibu yote ni ya aina hiyo mpya, ambayo hayaleti uchafuzi kwa mazingira na yanatumia umeme kidogo zaidi, hali ambayo inatokana na juhudi kubwa za serikali ya China. Ofisa wa idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya China Bi. Song Xiaozhi alisema:

    "Serikali ya China inazingatia sana hifadhi ya mazingira, kutokana na msimamo huo, imechukua hatua mbalimbali zikiwemo za kuinua kiwango cha teknolojia ili kuongeza ufanisi wa majokofu na kuwahamasisha watu wanunue majokofu ya aina mpya. Hatua hizo zitaleta ufanisi mkubwa kwa uchumi, mazingira na jamii. Kuongezeka kwa mwamko wa wateja wa kawaida kuhusu kuokoa nishati na huhifadhi mazingira pia kunahimiza jamii nzima kuokoa nishati na kuhifadhi mazingira."

    Imefahamika kuwa katika miaka ya karibuni, majokofu zaidi ya milioni 14 yamenunuliwa na wateja wa China kwa mwaka. Kwa takwimu za karne iliyopita, majokofu yote yaliyomilikiwa na wachina yalitumia umeme zaidi ya kilowati bilioni 600 kwa saa katika miaka 10 iliyopita, na kila mwaka yalitoa hewa chafu tani milioni 60.

    Ili kubana matumizi ya nishati na kuhifadhi mazingira, serikali ya China imeendeleza kwa juhudi jokofu lisiloleta uchafuzi kwa mazingira na linalotumia umeme kidogo, kuweka vigezo vya kubana matumizi ya umeme kwa viwanda vya kutengeneza majokofu, kuwahamasisha watu watumie majokofu yasiyo na freon na kushirikiana na mashirika ya kimataifa kuanzisha mradi wa miaka kadhaa wa kueneza majokofu ya aina hiyo. Ofisa wa idara kuu ya hifadhi ya mazingira ya China anayeshughulikia mradi huo Bw. Sun Xuefeng alisema:

    "Kwa upande mmoja tunainua kiwango cha viwanda vya majokofu, ambapo tulivisaidia kiufundi na kuviandalia wafanyakazi; kwa upande mwingine, tunatumia vyombo vya habari kuongeza ujuzi wa wateja kuhusu ulazima wa hifadhi ya mazingira na kubana matumizi ya nishati, na kuwashawishi wateja wanunue majokofu ya aina hiyo."

    Kupitia mradi huo viwanda vikubwa vya majokofu vya China vimeanza kutengeneza majokofu yasiyoleta uchafuzi kwa mazingira na yanayotumia umeme kidogo. Kiwanda kikubwa kabisa cha majokofu cha China, kundi la Haier, hivi sasa kimeanza kutumia kompresa isiyo na freon ambayo haitoi hewa chafu na inatumia umeme kidogo kwa karibu asilimia 50. Mfanyakazi wa idara ya masoko ya kiwanda hicho Bw. Gongzhen alifahamisha:

    "Kundi ya Haier linazingatia sana hifadhi ya mazingira na kubana matumizi ya umeme katika vipindi vya utafiti, utengenezaji, uuzaji na huduma. Hivi sasa bidhaa za kundi hilo unatumia kompresa yenye ufanisi mkubwa zaidi na kuleta uchafuzi kidogo. Pia kampuni hiyo inatumia vifaa vya kudhibiti ujoto vilivyotumika kwenye chombo cha safari za anga ya juu katika majokofu mapya, ambavyo vinaweza kutumika tena."

    Mpaka sasa majokofu yote yaliyozalishwa na kampuni hiyo yanatumia umeme chini ya kilowati 0.7 kwa saa kwa siku, hata majakofu mapya kabisa yanatumia umeme kilowati 0.4 kwa saa kwa siku. Kiwango cha ubanaji wa matumizi ya umeme cha baadhi ya uzalishaji wa kampuni hiyo kimezidi kile cha majokofu ya nchi zilizoendelea.

    Hivi sasa, licha ya kundi la Haier, zaidi ya viwanda kumi vya majokofu vya China vimefikiakigezo cha serikali kuhusu hifadhi ya mazingira na kubana maumizi ya nishati.

    Ili kueneza majokofu yasiyoleta uchafuzi kwa mazingira na yanayotumia umeme kidogo, makampuni ya majokofu ya China yamewaandaa kwa makini watu wanaoshughulikia mauzo ili wajue majokofu yanavyobana vipi matumizi ya umeme na vifaa gani vilivyotumika kwenye jokofu la aina hiyo.

    Bw. Ma Kaiming ni mwuzaji wa duka la vifaa vya umeme mjini Beijing, na alikuwa mshindi wa kwanza katika kuuza majokofu mengi ya aina hiyo. Alimwambia mwandishi wa habari kuwa aliuza majokofu ya aina hiyo kutokana na moyo wa wajibu wa kuhifadhi mazingira akisema kuwa, nishati duniani inapungua siku hadi siku, na nishati ya jadi kama makaa ya mawe na mafuta yanaleta uchafuzi mwingi, na kila anapofikiri hivyo, atafurahisha anavyofanya na kuwaelezea wateja kwa makini na kwa undani umuhimu wa majokofu ya aina hiyo, ambapo anawaelezea zaidi kuhusu kubana matumizi ya gharama ya umeme na umuhimu wa kuchagua majokufu ya aina hiyo kwa sisi binadamu.

    Takwimu zinaonesha kuwa kutokana na juhudi za serikali, viwanda vya ma jokofu na watu wanaoshughulikia mauzo, majokofu yasiyoleta uchafuzi kwa mazingira na kutumia umeme kidogo yanapokewa na wateja wa China siku hadi siku, na yamechukua karibu asilimia 50 ya soko la China.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-02