Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-04 17:49:53    
Mkutano wa kwanza wa ushirikiano wa hifadhi ya mazingira

cri

    Mkutano wa kwanza wa ushirikiano wa hifadhi ya mazingira ulifanyika tarehe 21 mwezi Februari huko Nairobi mji mkuu wa Kenya, ambapo naibu waziri mkuu wa China Bw. Zeng Peiyan, mkurugenzi wa ofisi kuu ya hifadhi ya mazingira ya taifa la China Bw. Jie Zhenhua pamoja na maofisa wanaohusika wa nchi za Afrika walihudhuria mkutano huo. Mkutano huo unamaanisha ushirikiano katika hifadhi ya mazingira kati ya China na Afrika umefungua ukurasa mpya, vilevile umeanzisha sehemu mpya katika Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika. Leo tunawaletea maelezo kuhusu mkutano huo.

    China na Afrika zimekuwa na uhusiano wa kirafiki kwa muda mrefu. Katika miongo kadhaa iliyopita, China na nchi za Afrika zimejenga uhusiano wa kirafiki wa kushirikiana na kusaidiana wakati zinapokabiliana na masuala ya maendeleo ya uchumi na jamii. Baadaye, ili kuhimiza ustawi na maendeleo ya pamoja, pande hizi mbili zimeanzisha Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, na kwa nyakati tofauti, ziliitisha mikutano miwili ya ngazi ya mawaziri. Hali ambayo imeweka msingi wa kukuza ushiriano kati ya China na Afrika.

    Mkurugenzi wa ofisi kuu ya hifadhi ya mazingira ya China Bw. Xie Zhenhua aliyehudhuria mkutano huo anasema,

    "Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika limetoa mahali pazuri kwa ushirikiano katika hifadhi ya mazingira kati ya pande hizi mbili. Ninatarajia ushirikiano huo unaweza kunufaisha pande zote mbili, na kutoa mchango katika kuendeleza uhusiano wa kila upande kati ya China na Afrika."

    Baada ya kutekeleza sera za mageuzi na kufungua mlango, uchumi wa China umepata maendeleo ya haraka na mfululizo. Nguvu ya taifa imeongezeka, ambapo maisha ya wananchi yameboreshwa kwa kiasi kikubwa. Lakini kutokana na idadi kubwa ya watu, na tofauti ya kiwango cha maendeleo katika sehemu mbalimbali, China inakabiliwa na matatizo ya ajira, maliasili na mazingira. Naibu waziri mkuu wa China Bw. Zeng Peiyan aliyeiwakilisha serikali ya China kushiriki kwenye mkutano huo alisema kuwa, ili kutimiza malengo ya maendeleo ya kila upande, China itatilia maanani zaidi katika hifadhi ya mazingira, na kushughulikia vizuri masuala ya maendeleo ya uchumi, idadi ya watu, maliasili na mazingira.

    Bw. Zeng anasema, "Ili kufanikisha maendeleo endelevu duniani, zinahitajika jitihada za pamoja za nchi mbalimbali duniani. Serikali ya China inashiriki kikamilifu kwenye ushirikiano wa pande mbalimbali wa hifadhi ya mazingira duniani. China pia imesaini na kuridhia mikataba kadhaa ya kimataifa ya hifadhi ya mazingira, na kubeba wajibu na kutekeleza yanayohusika majukumu zinazohusika."

    Bw. Zeng alieleza kuwa, katika miaka miaka mingi iliyopita, China imepata misaada kutoka mashirika yanayohusika ya kimataifa katika kazi ya hifadhi ya mazingira. Baadaye mbali na kufanya vizuri kazi ya hifadhi ya mazingira nchini, China vilevile itaendelea kuhimiza ushirkiano wa kimataifa katika kazi hiyo.

    Bw. Zeng anasema, "Ushirikiano katika hifadhi ya mazingira kati ya China na Afrika una fursa kubwa, na utaendelea vizuri. China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, ambapo Afrika ina nchi nyingi zaidi zinazoendelea duniani. Idadi ya watu wa China na Afrika inachukua theluthi ya watu wote duniani. Kuimarisha ushirikiano huo kutatoa fursa nzuri kwa China na Afrika kufundishana, na kusaidia katika ushirikiano wa hifadhi ya mazingira kati ya nchi zinazoendelea.

    Katika mkutano huo, serikali ya China pia imetoa mapendekezo kadhaa juu ya ushirikiano katika hifadhi ya maizingira kati yake na Afrika. Mapendekezo hayo, kwanza ni kupanua mawasiliano na mabadilishano ya kazi ya hifadhi ya mazingira, pili ni kuhimiza kwa nguvu ushirikiano wa teknolojia katika kazi hiyo, na tatu ni kuongeza mafunzo kwa wataalam.

    Bw. Zeng mwishoni alieleza kuwa, kukuza ushirikiano katika hifadhi wa mazingira na sekta nyingine za maendeleo kati ya China na Afrika, ni mchango mkubwa kwa maendeleo endelevu duniani. Pia alieleza kuwa China ingependa kubadilishana maoni na maarifa na nchi za Afrika, na kuhimiza ushirikano, ili kuendelea kwa pamoja. Alieleza kuamini kwamba, chini ya jitihada za pamoja, ushirikiano katika hifadhi ya mazingira bila shaka utapata maendeleo, na kupata mafanikio mazuri.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-04