Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-07 14:53:34    
Kiongozi wa ujumbe wa China atoa mwito wa kusukuma mbele maendeleo endelevu ya juhudi za kina mama duniani

cri

Bibi Zhao Shaohua alisema kuwa, mikutano minne ya kina mama duniani iliyoitishwa na Umoja wa Mataifa tokea mwaka 1975, imefanya kazi kubwa ya kusukuma mbele kazi ya kutimiza usawa kati ya wanaume na wanawake na maendeleo ya wanawake kote duniani, "Katiba ya Umoja wa Mataifa", "Katiba ya kutokomeza ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya kina mama" na mikataba miwili kuhusu haki za kisiasa za kina mama, yote hayo yamechukua malengo ya kutimiza usawa kati ya wanaume na wanawake, kuhimiza na kulinda haki za kisiasa na haki za uchumi, jamii na utamaduni za kina mama kuwa malengo makubwa ya kutimiza haki za kawaida za binadamu. Lakini Bibi Zhao aliainisha kuwa, hali ya kuwabagua kina mama na hali ya umaskini ya kina mama, bado ni mbaya sana, jumuiya ya kimataifa inakabiliwa na kazi ngumu na ya muda mrefu katika kuhimiza na kulinda haki za kina mama.

Bibi Zhao Shaohua alisema kuwa, mkutano wa 4 wa kina mama duniani uliofanyika mjini Beijing mwaka 1995 ulipitisha "Taarifa ya Beijing" na "Mpango wa utekelezaji". Hatua hiyo imeleta athari muhimu kwa juhudi za kina mama duniani na maendeleo endelevu ya binadamu katika siku za usoni. Alisema kuwa, katika miaka 10 iliyopita, jumuiya ya kimataifa ilifanya juhudi za pamoja, kutekeleza kwa bidii "Mpango wa utekelezaji" na nyaraka za Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kina mama, ambapo mawazo kuhusu jinsia katika jamii, yamewekwa kwenye kazi kuu ya utoaji sera, na utaratibu mbalimbali umeanzishwa kutokana na hayo.

Bibi Zhao alisema, katika miaka 10 iliyopita, serikali ya China ilichukua hatua halisi kutimiza ahadi zake, kuichukulia kazi ya kutimiza usawa kati ya wanaume na wanawake kuwa sera moja ya kimsingi ya taifa katika kusukuma mbele maendeleo ya jamii ya China, ambapo imetunga "Mwongozo wa maendeleo ya wanawake wa China", kufanya juhudi katika kuhimiza maendeleo mazuri na endelevu ya utulivu ya jamii na uchumi, kufanya juhudi kutokomeza ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya kina mama, na kutekeleza kwa makini "Mpango wa utekelezaji wa Beijing", serikali ya China imefanya juhudi thabiti kwa ajili ya maendeleo ya kina mama wa China, na kupata mafanikio makubwa ya kuvutia walimwengu.

Bibi Zhao Shao amezitaka nchi mbalimbali duniani zitimize kihalisi ahadi zao, kuchukua hatua halisi kuondoa ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya kina mama, na kufanya juhudi za pamoja kusukuma mbele maendeleo endelevu ya juhudi za kina mama kote duniani na maendeleo ya ustaarabu wa binadamu wote, na kutimiza lengo tukufu la usawa, amani na maendeleo.

Mkutano wa 49 wa kamati ya hadhi ya kina mama ya Umoja wa Mataifa ulifanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York kuanzia tarehe 28 Februari hadi tarehe 11 Machi.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-07