Hivi karibuni, Iran ilieleza kithabiti msimamo wake kuhusu suala la nyuklia la Iran, jambo ambalo limefuatiliwa sana na jumuiya ya kimataifa. Kutokana na kuwa katika wiki hii Iran, na nchi tatu zinazouwakilisha Umoja wa Ulaya (Ufaransa, Ujerumani na Uingereza) zitakuwa na mazungumzo kwa mara nyingine huko Geneva, hivyo watu wanajiuliza kama Iran kushikilia kithabiti msimamo wake ni mbinu ya Iran inayotumia kabla ya kufanyika kwa mazungumzo ili iweze "kupigania bei" na nchi hizo tatu, au ni kubadilika kimsingi kwa msimamo wake katika mazungumzo?
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Hamid Riza Asefi tarehe 6 alisema kuwa hata hatimaye suala la Iran litawasilishwa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Iran pia haitaacha haki yake kuhusu matumizi ya amani ya nyuklia. Katika suala hilo, sera za aina yoyote za kutishia na kushawishi hazitafanikiwa. Katibu wa kamati ya usalama wa taifa ya Iran, ambaye pia ni mwakilishi wa kwanza kwenye mazungumzo Bw. Hassan Rowhani tarehe 5 alitishia kuwa, endapo mazungumzo kati ya Iran na Umoja wa Ulaya yatashindwa kutokana na shinikizo la Marekani, na kusababisha suala la nyuklia kuwasilishwa kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, siyo tu kwamba Iran haitekeleza ahadi yoyote iliyotoa kuhusu suala la nyuklia, bali pia usalama na utulivu wa sehemu ya mashariki ya kati na mauzo ya mafuta ya petroli duniani yatakumbwa na matatizo, ambapo Umoja wa Ulaya na Marekani zitakuwa za kwanza kuathirika. Kabla ya hapo, ofisa mwandamizi wa Iran alipozungumzia kuhusu Marekani kuanzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran, alisema kuwa kushambulia Iran ni sawa na kuhatarisha mafuta ya petroli ya Saudi Arabia hata sehemu nzima ya mashariki ya kati, bei ya mafuta duniani itapanda hadi dola za kimarekani 70 kwa pipa moja. Baadhi ya magazeti ya Ulaya yanaona kuwa Iran sasa inatumia "silaha ya mafuta".
Katika miaka ya karibuni, suala la nyuklia la Iran lilikuwa na migogoro mingi. Kuhusu suala hilo, wahusika wakuu watatu wa Iran, Umoja wa Ulaya na Marekani wote wameonesha kikomo cha mwisho.
Umoja wa Ulaya unakiri kuwa Iran ina haki ya kutumia nyuklia kwa njia ya amani, isipokuwa inapaswa kuacha moja kwa moja kusafisha uranium nzito ili kuhakikisha kuwa mpango wake wa matumizi ya nyuklia siyo wa kijeshi. Marekani inataka Iran iache kabisa majaribio ya nyuklia. Ingawa hivi karibuni msimamo wa Marekani ulionekana kulegea kidogo, lakini undani wake bado unaona kuwa nia halisi ya Iran ya kutoacha kabisa majaribio ya nyuklia ni kutaka kuwa na silaha za nyuklia.
Kikomo cha mwisho cha Iran kwenye mazungumzo ya suala la nyuklia ni kuhifadhi haki yake ya kufanya utafiti na kutumia nyuklia kwa njia ya amani. Mgongano hasa kati yake na Umoja wa Ulaya ni kuwa Iran inaruhusiwa kuwa na uhuru kamili katika kufanya utafiti wa nyuklia. Iran ikitaka kuwa na uhuru kamili katika utafiti wa nyuklia, basi haina budi kurejesha usafishaji wa uranium na kukuza na teknolojia zote kuhusu nyuklia ikiwa ni pamoja na kujenga kinu rahisi cha maji mazito cha nyuklia. Tofauti kati ya kinu cha maji mazito na kinu cha maji mepesi ni kuwa kinu cha maji mepesi yanaweza tu kutumika katika kuzalisha umeme, lakini kinu cha maji mazito licha ya kuweza kutumika katika kuzalisha umeme kinaweza pia kutumika kuzalisha malighafi kwa ajili ya kutengeneza silaha za nyuklia. Ni kutokana na sababu hiyo, Umoja wa Ulaya unakubali kuipatia Iran kinu cha maji mepesi na kupinga Iran kufanya utafiti kuhusu teknolojia ya nyuklia.
Tofauti kati ya misimamo ya pande hizo tatu inamaanisha kuwa mazungumzo hayo yatakuwa magumu hata kushindwa kabisa. Iran inafahamu sana hali hiyo, hivyo wakati inapojiandaa kukabiliana na matokeo mabaya kabisa, inajitahidi kupeleka utatuzi wa suala la nyuklia kwenye mwelekeo inaotaka.
Iran inaona kuwa nchi yake ni ya pili kwa wingi wa usafirishaji wa mafuta ya petroli katika jumuiya ya nchi zinaozosafirisha mafuta ya petroli duniani OPEC ikiifuatia Saudi Arabia, tena hivi sasa bei ya mafuta duniani inaendelea kupanda, hivyo nchi za magharibi huenda hazithubutu kulishawishi baraza la usalama la umoja wa mataifa kuiwekea vikwazo Iran, sembuse Marekani kuanzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi yake.
Lakini baadhi ya magazeti ya nchi za Ulaya yamesema kuwa kuonesha msimamo mgumu kwa Iran hivi karibuni ni mbinu yake ili iweze "kupigania bei" na nchi hizo tatu kwenye mazungumzo, msimamo wa Umoja wa Ulaya utakuwa imara endapo mazungumzo kushindwa kupata maendeleo kadiri siku zinavyopita.
Idhaa ya Kiswahili 2005-03-07
|