Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-08 15:24:32    
Jeshi la Syria nchini Lebanon laanza kurudishwa kwenye Bonde la Bekaa

cri

Tarehe 7 kamati mbili za viongozi wakuu wa Syria na Lebanon walikubaliana kwamba jeshi la Syria nchini Lebanon litarudishwa kabisa kwenye Bonde la Bekaa kabla ya mwishoni mwa mwezi huu. Jioni ya siku hiyo jeshi la Syria lilianza kurudishwa kwenye Bonge la Bakaa, mashariki mwa Lebanon. Wachambuzi wanaona kuwa kurudishwa kwa jeshi la Syria hakutasaidia kupunguza shinikizo kubwa kwa Lebanon kutoka ndani na nje ya nchi.

Kamati mbili za viongozi wakuu za Syria na Lebanon zilifanya mkutano mjini Damascus na kujadili hatua za kurudishwa kwa jeshi la Syria. Rais Rashar al Assad wa Syria na rais Emile Lahud wa Lebanon pamoja na mawaziri, maspika mawaziri wa mambo ya nje na mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo mbili, walihudhuria mkutano huo. Huu ni mkutano wa kwanza kufanywa na kamati hizo mbili katika muda wa miaka mitatu. Taarifa ya mkutano inasema, jeshi ya Syria litarudishwa kwenye Bonde la Bekaa, mashariki mwa Lebanon kabla ya mwishoni mwa mwezi huu. Mkutano huo pia umeagiza kamati ya kijeshi ya muungano wa Syria na Lebanon ijadili muda na idadi ya askari wa Syria kwenye bonde hilo na pia ulijadili uhusiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili na kutoa mwafaka kamili, ili kuweka ratiba ya kuondoa kabisa jeshi la Syria kutoka Lebanon.

Kabla ya mkutano huo marais wa nchi mbili waliwahi kukutana, wakisisitiza pande mbili lazima zitekeleze "Mkataba wa Kirafiki wa Ushirikiano" uliotiwa saini mwaka 1991 baada ya vita wenyewe kwa wenyewe kumalizika.

Kuhusu uamuzi uliofanywa na kamati mbili za viongozi wakuu, watu wana maoni tofauti: Baadhi wanaufurahia uamuzi huo, lakini baadhi wanasema huu ni ujanja wa Syria kuchelewesha muda kwa makusudi, kwani lengo lake ni kutaka kudumisha athari yake kwa Lebanon. Katika siku hiyo watu wa Lebanon waliitikia wito wa vikundi vya upinzani na kufanya maandamano wakitaka kufichua ukweli wa tukio la kuuawa kwa waziri mkuu wa zamani Bw. Hariri na kumtimua na kumwadhibu wakuu wa idara za usalama wa Lebanon na kuhimiza askari wa Syria waondoke kabisa haraka iwezekanavyo kutoka Lebanon. Katibu mkuu wa chama cha Hizbullah Nasrullah alitoa wito kwa waislamu wa madhehebu wa Shia wafanye maandamano mjini Beirut tarehe 8 kupinga nchi za nje kuingilia kati na kuondoa jeshi la Syria nchini Lebanon kwa kufuata azimio la Baraza la Usalama Nam. 1559.

Msemaji wa ikulu ya Ufaransa tarehe 7 alisema marais wa Marekani na Ufaransa walijadiliana kwa njia ya simu kuhusu suala la Lebanon. Pande mbili zinaona kuwa azimio la Baraza la Usalama Nam. 1559 lazima litekelezwe, na Syria lazima iondoe kabisa askari wake na wapelelezi wake wa habari kutoka Lebanon, na kufanya uchaguzi mkuu ulio huru na wazi nchini Lebanon. Siku hiyo rais wa Ufaransa na chansela wa Ujerumani walitoa taarifa ya pamoja baada ya kukutana, ikitaka Syria iondoe kabisa askari na wapelelezi wake kutoka Lebanon kwa haraka iwezekanavyo.

Wachambuzi wanaona kuwa kutokana na shinikizo linalotoka pande nyingi, mstari wa mwisho wa Syria ni kurudisha askari wake kwa hatua na utaratibu, lakini kabisa haitakubali nchi kubwa za magharibi, Marekani na Ufaransa, hila ya kufarakanisha uhusiano kati ya Syria na Lebanon. Kufuatana na uamuzi wa kurudisha askari kwa "ratiba isiyo wazi", sasa Syria imerudi karibu kufikia mstari wake wa mwisho. Katika hali kama hiyo kama vikundi vya upinzani vikichukulia maslahi ya kitaifa kama ni jambo muhimu zaidi na kushirikiana na msimano wa Lahud katika juhudi za kuunda serikali ya mpito na maandalizi ya uchaguzi wa bunge, basi hali ya Lebanon inatazamiwa kuwa tulivu. La sivyo, iwapo vikundi hivyo vikiendelea kushinikiza serikali ya sasa kwa kuungwa mkono na nchi za magharibi, basi hali nchini Lebanon itakuwa mbaya zaidi.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-08