Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-08 16:40:47    
Maendeleo ya uchumi binafsi yakabiliwa nafsi mpya

cri

Hivi karibuni serikali ya China ilitangaza sera zinazokusudia kuhimiza maendeleo ya uchumi binafsi. Kutokana na sera hizo, uchumi binafsi utaruhusiwa kuingia katika sekta yoyote ambayo haikatazwi na sheria yoyote ya China, zikiwa ni pamoja na sekta za umeme, mawasiliano ya habari, reli, usafirishaji wa ndege, mafuta ya petroli na mambo ya fedha, ambazo zilihodhiwa na uchumi wa taifa. Licha ya hayo, sera hizo zinahamasisha uchumi binafsi kushiriki uwekezaji, ujenzi na uendeshaji wa sekta za utoaji huduma na miundombinu. Maofisa husika wanasema kuwa kutekelezwa kwa sera hizo kutatoa nafasi mpya ya maendeleo kwa uchumi binafsi.

Mwanauchumi mashuhuri wa China Bw. Cheng Siwei amesema kuwa sera madhumuni hasa ya hizo zilizotolewa na serikali za kuhamasisha maendeleo ya uchumi binafsi ni kupunguza masharti ya kuingia katika masoko kwa uchumu binafsi. Licha ya hayo sera hizo zimetoa hatua nyingi za kuhimiza maendeleo ya uchumu binafsi. Alisema,

"Hapo zamani tulikuwa na makosa ya kuzuia na kubagua uchumi binafsi, kwa mfano, baadhi ya shughuli hata sisi tuliruhusu kampuni za nchi za nje kuzifanya, lakini tulivinyima viwanda binafsi nafasi hiyo. Mimi ninaona kuwa kitu kilicho muhimu zaidi cha sera hizo ni utoaji kibali cha kuingia sokoni yaani usawa wa kuingia katika masoko bila ubaguzi, ikiwa ni pamoja na kuingia katika sekta zilizohodhiwa na kampuni za kiserikali kwa viwanda binafsi, pamoja na kuingia katika maeneo, ambayo yaliruhusiwa tu kwa kampuni za nchi za nje."

Maendeleo ya uchumi binafsi nchini China yalianzia mwishoni mwa miaka ya 70. baada ya kuendelezwa kwa zaidi ya miaka 20, hivi sasa uxhumi binafsi umekuwa moja ya sehemu muhimu za uchumi wa kimasoko nchini. Takwimu zinaonesha kuwa hivi sasa nchini China kuna viwanda kiasi cha milioni 4, ambavyo vilisajiriwa kuwa na mali Yuan zaidi ya trioni 4 ikiwa ni ongezeko la mara zaidi ya 50 kuliko ile ya kabla ya miaka 10 iliyopita. Aidha, nafasi ya uchumi binafsi katika jumla ya thamani ya uzalishaji nchini hivi sasa imefikia theluthi moja ikilinganishwa na upungufu ya asilimia moja ya kabla ya miaka 27 iliyopita.

Katika muda wa karibu miaka 10 iliyopita, China ilitekeleza sera za kuhamasisha maendeleo ya uchumi binafsi na kueleza kuboresha utaratibu wa kisheria wa kulinda mali binafsi katika mswada wa marekebisho ya katiba ya nchi., mambo ambayo yameboresha zaidi mazingira ya nje ya maendeleo ya uchumi binafsi nchini China.

Mwanauchumi Bw. Cheng Siwei anaona kuwa licha ya kustawisha uchumi wa miji na vijiji, kuongeza pato la serikali na kuongeza ajira kwa jamii, maendeleo ya uchumi binafsi yanaongeza uhasama wa uchumi wa kimasoko. Alisema,

"Ninaona kwamba umuhimu mkubwa wa uchumi binafsi ni kuongeza nguvu ya maendeleo ya uchumi wa China na kuongeza uhasama wa uchumi wa kimasoko. Kuweko kwa viwanda binafsi kunaboresha masoko, kuhimiza ushindani, kuvunjilia mbali uhodhi, kuhamasisha masoko na kuleta manufaa kwa maendeleo ya uchumi wa tiafa na wanunuzi."

Hata hivyo, maendeleo ya uchumi binafsi nchini China hivi sasa yanakabiliwa baadhi ya shida na matatizo, ambayo ni pamoja na kubaki nyuma kwa mawazo ya baadhi ya idara za mikoani, kutokamilika kwa sheria husika; Kuweko baadhi ya vikwazo katika utoaji kibali cha kuingia masokoni, njia finyu ya kukusanya fedha kwa viwanda; Kutokamilika kwa mfumo wa utoaji huduma za jamii, kutoridhisha kwa usimamizi na huduma za serikali. Maofisa husika wanaona kuwa kutolewa kwa sera hizo kwa serikali ya China kutaanzisha mazingira bora ya sera ya kutatua masuala hayo. Kwa mfano sera hizo zinaruhusu viwanda binafsi kuingia katika eneo la mambo ya fedha, hatua hiyo itachangia utatuzi wa shida ya kukusanya fedha kwa viwanda binafsi. Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanaviwanda na Wafanya-biashara nchini China Bw. Huang Mengfu alisema,

"Ninaona vifungu vya sera hizo kuhusu kuyaunga mkono katika mambo ya fedha viwanda binafsi na viwanda vya wastani na vidogo ni kamili, kwanza vinaruhusu mitaji binafsi kuingia katika eneo la mambo ya fehda, pili vinaimarisha uungaji mkono katika mambo ya fedha kwa viwanda vidogo , wastani na viwanda binafsi. Licha ya hayo, sera hizo zinataka baadhi ya benki za mikoa na benki ndogo na wastani zianzishe sehemu za kutoa mikopo kwa viwanda vya wastani na vidogo, kuongeza mikopo kwa viwanda vya wastani, vidogo na viwanda binafsi."

Sera hizo za serikali za kuhamasisha maendeleo ya uchumi binafsi zinapendwa na viwanda na kampuni binafsi. Kampuni ya Xin Ao yenye wafanyakazi zaidi ya elfu 8 ni kampuni kubwa binafsi inayoshughulikia biashara ya ges katika miji ya China, katika muda wa miaka zaidi ya kumi iliyopita mali ya kampuni hiyo imezidi Yuan za Renminbi bilioni 5. Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Bw. Wang Yusuo alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari alisema kuwa sera hizo za serikali zimeongeza nafasi za kuchagua na kuwekeza kwa viwanda na kampuni binafsi.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-08