Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-09 15:11:47    
Maisha ya mwanafunzi mwenye matatizo ya kiuchumi Pan Liling katika chuo kikuu

cri

    Majira ya joto ya mwaka 2004, msichana Pan Liling anayetoka kijiji kimoja cha mkoa wa Shanxi, kaskazini magharibi mwa China, alifaulu mtihani na kujiunga na Chuo Kikuu cha Viwanda cha Kaskazini Magharibi. Lakini kutokana na umaskini wa familia yake, alikaribia kuacha fursa ya kujiunga na chuo kikuu. Baada ya kujua wanafunzi kama yeye wanaweza kuomba mkopo wa taifa wa kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi kulipa ada za vyuo vikuu, akakwenda chuoni na jiandikisha akiwa na pesa kidogo zilizoazimiwa na wazazi wake kutoka kwa watu wengine.

    Aliishi vijijini kutoka utoto wake, hivyo alipoona barabara kubwa zenye magari mengi yanayokimbia na majengo mengi marefu mjini alishtuka huku akiwa na wasiwasi; na alifurahishwa na maktaba kubwa, ukumbi mpya wa michezo na madarasa makubwa ya chuo kikuu, huku akiwa hakujua la kufnaya. Lakini kitu kilichomsumbua kabisa ni ukosefu wa fedha.

    Pan Lingli anaishi na wenzake watatu bwenini, hao wote wanatoka miji mikubwa, na hali ya kiuchumi ya familia zao ni nzuri, hivyo maisha yake ni tofauti na ya Pan Lingli. Pesa zilizotumiwa nao kwa mlo mmoja huzidi zile za Pan kwa siku moja nzima, na wasichana hao kuenda nje ya chuo kikuu kula na kununua vitu. Pan alipowaona, alijihisi kuwa ni mtu wa chini, kwa kuwa ili kuendesha maisha ya kila siku, alipaswa kuwa na uangalifu katika matumizi ya kila cent. Hata bwaloni Pan hununua vyakula vya bei za chini, sembuze kununua nguo na vitu vyingine madukani.

    Kutokana na hali hiyo, Pan hakupenda kwenda nje ya chuo kikuu wala kula pamoja na wanafunzi wengine, na yeye hufanya mambo peke yake, na wenzake walidhani kuwa ni vigumu kuwa pamoja naye. Hivyo, kulikuwa na umbali kati ya Pan na wanfunzi wengine.

    Mbali na matatizo katika maisha, pia Pan aliona shule ni ngumu. Kwa kuwa yeye anatoka kijijini, alikuwa hajui jinsi ya kutumia kompyuta, na hakuweza kutamka maneno ya Kiingereza sahihi, hivyo alisumbuliwa sana na masomo hayo mawili. Zaidi ya mwezi mmoja baada ya darasa la kompyuta kuanzishwa, Pan bado aliona vigumu kujifunza. Ili kufikia wanafunzi wengine, kila ifikapo siku za mapumziko alikwenda darasa la kompyuta na kufanya mazoezi. Ingawa alifaulu mtihani uliofanyika miezi miwili baadaye, lakini alishindwa mtihani wa Kiingereza. Hakujua la kufanya wakati alipopata matokea ya mtihani wa Kiingereza, alisema:

    "Nilipoona ripoti ya mtihani nilishtuka sana, kwa kuwa nilishindwa mtihani wa Kiingereza, niliona kizunguzungu wakati huo huo. Hapo awali nilikuwa sijashindwa mtihani. Wakati huo huo, nilisikitika sana, nilikuwa najichukia."

    Kuanguka mtihani kulitokana na Pan kutojua lugha ya Kiingereza vizuri, hasa sarufi ya Kiingereza. Hivyo alimwuliza mwalimu maswali kuhusu Kiingereza mara kwa mara. Mwalimu wa Kiingereza Bi. Hu Huarong alipendezwa na msichana huyo akisema:

    "Pan aliniuliza maswali mara kwa mara, na nilijibu maswali yake yote na kumfundisha sarufi ya Kingereza, na nilimwonesha makosa yake katika makala ya kiingereza. Kutokana na juhudi zake, alifaulu mtihani wa Kiingereza katika jaribio la pili."

    Siku hadi siku Pan alipendwa na wanafunzi wengine kwa makini na bidii yake. Wenzake walipojua hali ya kiuchumi ya familia yake, walijitokeza kumsaidia kadiri walivyoweza. Mmoja wa wenzake bwenini, msichana Liulu anatoka Beijing, na wazazi wake walipopata habari kuhusu Pan, walimnunulia nguo nyingi; na msichana mwingine Hu Qianqian alitaka kumpa Pan simu moja ya mkononi, alimwambia mwandishi wa habari akisema:

    "Hali ya kiuchumi ya familia ya Pan sio nzuri, nikiwa mwezake bwenini ninastahili kumsaidi. Nlimletea simu ya mkononi, alikataa kuipokea kutokana na kujiheshimu."

    Kwa kawaida Pan alikataa kwa maneneo mazuri misaada kutoka kwa wenzake, mara chache tu alipokea vitu chache kwa sababu ya ukarimu wao. Pan aliamua kujitegemea, hivyo mara alipojiunga na chuo kiuu alianza kutafuta fursa ya kuchuma pesa. Mara yake ya kwanza ya kuchuma pesa ni kuwa mwalimu binafsi wa mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi.

    Aidha, alipendekezwa kuwasaidia walimu ofisini. Kati ya wanafunzi wengi wanaofanya kazi ya ziada, Pan ni wa bidii na hodari kabisa. Ingawa pesa zilizotokana na kazi ya ziada sio nyingi, lakini pesa hizo zilipunguza kwa kiasi kikubwa mizigo yake ya maisha, na Pan anaamini kuwa hali ya siku za usoni katika chuo kikuu itakuwa nzuri zaidi, akisema:

    "Ingawa nilizaliwa katika familia maskini, lakini nitabadilisha hali hiyo. Iwapo ninajitahidi zaidi, naweza kuwafikia wanafunzi wengine katika masomo na maisha."

    Pan aliwashukuru wanafunzi wengine kwa misaada yao. Baada ya siku za mapunziko za majira ya baridi, aliwaletea wenzake matende na matufaha yaliyozalishwa nyumbani kwake. Pan alifurahi sana alipoona wenzake wanayapenda matunda hayo.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-09