Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-09 17:50:56    
Kwa nini China haikubaliani na marufuku ya ku-"clone" binadamu

cri

Baraza kuu la 59 la Umoja wa Mataifa liliidhinishasha "Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu ku-clone binadmau" kwa kura 84 za ndiyo, 34 za hapana na kura 37 hazikupigwa. Azimio hilo ambalo lilipitishwa na kamati ya sheria ya umoja huo mwezi uliopita, linataka nchi zote duniani kufikiria kupiga marufuku ku-clone binadamu kwa mtindo wa kila aina, kitendo ambaco kinakwenda kinyume cha heshima ya binadmu.

Habari zinasema kuwa azimio hilo halina nguvu ya kisheria isipokuwa ni azimio la kisiasa tu.

China, Uingereza, Ubelgiji, Ufaransa na India ni nchi ambazo zinazounga mkono kum-clone binadmau kwa lengo la matibabu, zilipiga kura za hapana. Kiongozi wa ujumbe wa China alisema kuwa sababu ya China kupiga kura hapana, siyo kupinga marufuku ya ku-clone binadamu bali ni kusisitiza kuwa katika hali ya hivi sasa ambayo teknolojia ya viumbe imepata maendeleo ya kasi duniani, waraka wa azimio hilo ungeeleza kwa kirefu na kikamilifu. Neno la "kupiga marufuku" katika waraka huo ni rahisi kwa watu kuelewa vibaya kuwa azimio linapiga marufuku ku-clone binadamu kwa aina namna zote ikiwemo na kwa malengo ya matibabu, jambo ambalo China haikubaliani nalo. Aidha, kwa kuwa azimio hilo halikueleza wazi maoni tofauti ya nchi mbalimbali kuhusu suala hilo, hivyo azimio hili siyo kamili. Walakini China itaendelea kushikilia msimamo wake wa kupinga ku-clone binadamu kwa lengo la uzazi, na itaendelea kuimarisha usimamizi na udhibiti kuhusu utafiti wa ku-clone binadamu kwa lengo la tiba ili kuhakikisha kuwa heshima ya binadamu na wazo kuhusu uhusiano wa binadamu visiharibiwe.

Katika miaka ya karibuni, utafiti na teknolojia ya ku-clone iliendelezwa kwa mfululizo. Tokea mwaka 2001 kamati ya sheria ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikijaribu kutunga makubaliano ya kimataifa kupiga marufuku ku-clone binadamu kwa lengo la uzazi, ili kulinda heshima ya binadamu, lakini kulikuwa na maoni tofauti kuhusu ku-clone binadamu kwa lengo la matibabu. Kutokana na kuweko tofauti kubwa ya maoni, siku si nyingi zilizopita Umoja wa Mataifa uliamua kuacha jitihada ya kutunga sheria ya kimataifa kuhusu ku-clone binadamu, ukajaribu kupitisha azimio la kisiasa lisilo na nguvu ya kisheria. Kutokana na hayo azimio hilo la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la ku-clone binadamu ni la kufanya usuluhishi.

Ukweli ni kuwa kuna tofauti kihalisi kati ya ku-clone binadamu kwa lengo la matibabu na uzazi. Ku-clone binadamu kwa lengo la tiba ni ku-clone mimba ya binadamu kwa kutumia teknolojia ya kuhamisha kiini cha chembe ya mwilini ya binadamu ili kupata chembe kavu ambazo zinatumika katika tiba kwa baadhi ya magonjwa ya binadamu. Ndiyo maana, baadhi ya wanasayansi wamependekeza kutumia maneno ya "teknolojia ya kuhamisha kiini cha chembe ya mwilini ya binadamu" badala ya maneno ya ku-clone binadamu yenye lengo la tiba, ili kuepusha kueleweka vibaya kwa watu. Wanasayansi wanaona kuwa kutokana na kuwa teknolojia ya aina hiyo inaweza kuleta matumaini kwa wagonjwa wa aina nyingi, hivyo maendeleo yake yatakuwa na athari kubwa kwa binadamu katika siku za baadaye. Hivi sasa wanasayansi wa baadhi ya nchi zikiwemo Uingereza na Korea ya Kusini wameanza kufanya baadhi ya utafiti katika maabara kuhusu ku-clone binadamu kwa lengo la matibabu, wakitarajia hatimaye wataweza kutibu baadhi ya magonjwa sugu yakiwemo kisukari na kuwa punguani kwa baadhi ya wazee.

Mambo yanayotakiwa kuelezwa zaidi ni kuwa tofauti ya maoni ya nchi mbalimbali kuhusu suala la ku-clone binadamu zilitokana na dini na mazingira tofauti ya utamaduni. Baadhi ya nchi zinaona kuwa uhai wa binadamu unaanza kipindi cha mimba, wakati baadhi ya nchi nyingine zinaona kuwa uhai unaanza wakati mtoto anaumbika ndani ya tumbo la mzazi au baada ya mzazi kujifungua. Hivi sasa baadhi ya nchi zikiwemo China na Uingereza zinaona kuwa mimba inakuwa na uwezo wa hisia na kukua kwa mshipa wa neva yaani katika siku ya 14 tangu mama mzazi kupata uja uzito. Hivyo mimba inayotumika katika utafiti wa ku-clone binadamu kwa lengo la matibabu ndani ya maabara lazima kutekelezwa ndani ya siku 14 ya mimba hiyo.

Katika mwanzo wa mwaka 2004, China ilitekeleza Kanuni kuhusu wazo la ubinadamu katika utafiti wa chembe kavu za mimba ya binadamu, ambayo inapiga marufuku utafiti wa ku-clone binadamu kwa lengo la uzazi. Hivyo kanuni za China hazigongani na msingi wa azimio hilo lililopitishwa na Umoja wa Mataifa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-09