Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-10 15:34:39    
Poslisi wanawake wa China nchini Haiti

cri

Mwezi Septemba mwaka 2004, kutokana na mwaliko wa Umoja wa Mataifa, serikali ya China ilituma kikosi cha polisi wa kulinda amani nchini Haiti. Miongoni mwa polisi 125 kuna polisi wanawake 13. ingawa polisi hao 13 ni wanawake, lakini katika kazi ya kulinda amani kwao haina tofauti yoyote na ya polisi wanaume, walijitahidi kufanya kazi ili kulinda amani ya Haiti.

Mkuu wa kikosi cha polisi wa kulinda amani wa China kilichoko Haiti Bw. Zhao Xiaoxun alisema kuwa, anajivunia sana polisi hao wanawake 13, kwa kuwa walipokumbwa na matatizo au kubabiliana na hatari walionesha utulivu na ushujaa, na mwishowe walishinda matatizo.

Habari zinasema kuwa, kikosi hiki kitamaliza kazi na kurudi China mwezi Aprili. Bw. Zhao Xiaoxun alimwambia mwandishi wa habari kuwa, polisi 125 wa China watarudi China kwa vikundi viwili, na wakati huo huo askari wengine 125 kutoka mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China watakwenda kuendelea na kazi ya kulinda amani nchini Haiti. Kikundi cha kwanza cha askari 30 kinatazamiwa kurudi China tarehe 2 mwezi Aprili na kikundi cha pili cha askari 95 kitarudi China tarehe 17 mwezi Aprili.

Bw. Zhao alidokeza kuwa, hadi tarehe 19 mwezi Februali, kikosi cha polisi wa kulinda amani kilifanya oparesheni 197 nchini Haiti, zikiwemo kulinda usalama wa sehemu mbalimbali, kunyang'anya silaha, kuwakamata wanamgambo, kuanzisha vituo vya ukaguzi na kuzuia maandamano, kwenye opresheni hizo hakuna askari hata mmoja aliyejeruhiwa.

Askari hao wanawake 13 wanatoka Beijing, Tianjing, Chongqing, Jilin, Guangdong na sehemu nyingine nchini China. Walipokuwa nchini China walikuwa wanafanya kazi za kutuliza ghasia, ukalimani, madaktari na waunguzi.

Kazi ya kikosi cha polisi wa kulinda amani wa China ni kutoa uungaji mkono kwa polisi wa Haiti na polisi wa mambo ya kiraia wa Umoja wa Mataifa. Bw. Zhao alisema kuwa, wakati wa kutekeleza oparesheni, hakuna tofauti kati ya wanaume na wanawake. Kama polisi wanaume wanavyofanya, polisi wanawake pia walipaswa kuingia kwenye sehemu za hatari, kushika bunduki na kuvaa nguo za kuzuia risasi. Mbali na hayo walipaswa kuvumilia jua kali na mvua mkubwa.

Nchini Haiti, si kama tu wanamgambo wanashambulia raia, bali pia wanashambulia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, hasa askari wa kulinda amani. Bibi Han Yiqiu ni mkalimani wa kikosi cha kufanya doria. Tarehe 18 mwezi Novemba mwaka jana kikosi chake kilipofanya doria mitaani, walisikia mlio wa sisasi, wakati huo huo, polisi mwengine alimsaidia kumpeleka ndani ya gari lenye silaha. Hali hiyo ya hatari ni ya kawaida kwa maisha ya polisi wa China nchini Haiti.

Bibi Ji Lan na Liu Zhengzheng wanaotoka Chong Qing, walifanya kazi ya kulinda ghala la ya risasi na bunduki. Kutokana na umuhimu wa kazi zao, hawawezi kulala kwa siku 10 kila mwezi. Ingawa wanachoka sana lakini hawafanyi makosa yoyote.

Hivi sasa kikosi hicho cha polisi wa kulinda amani wa China bado kinafanya kazi kwa bidii nchini Haiti. Polisi hao wakiwemo polisi wanawake 13 wanatoa mchango ili kudumisha amani na usalama wa nchi hiyo.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-10