Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-10 20:29:56    
Picha zilizochorwa ukutani za Dunhuang

cri

    Mapango ya Mogao yako katika sehemu yenye miti na chemchemi katika jangwa lililoko kilomita 25 kusini mashariki ya mji wa Dunhuang mkoani Gansu. Mwezi Desemba mwaka 1987, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) iliyawekza mapango ya Mogao kwenye orodha ya urithi wa utamaduni duniani pamoja na Mlima Tai, ukuta mkuu, kasri la wafalme na sanamu za askari na farasi za kaburi ya mfalme Qinshihuang kama ni urithi adimu wa kiutamaduni wa binadamu.

    Mapango ya Mogao yalianza kuchongwa kuanzia mwaka 366. Na ujenzi wa mapango hayo ulipamba moto katika enzi ya Tang(618-907). Wakati mama malkia Wu Zetian aliposhika madaraka, idadi ya mapango ya huko ilikuwa zaidi ya elfu moja. Katika enzi za baadaye mapango mapya yaliendelea kuchongwa hadi kufikia Enzi ya Yuan(1206-1368). Hivi sasa milimani bado kuna mapango zaidi ya elfu 7 na mapango makubwa 492. Mapango ya Mogao ni mapango yaliyochongwa zamani zaidi na yenye vitu vingi zaidi nchini China, pia ni mapango yaliyochongwa kwa muda mrefu zaidi katika historia. Sehemu ya mapango hayo ina urefu zaidi ya mita 1600. Katika mapango hayo nyaraka zaidi ya elfu 50 zinahifadhiwa, na kuna picha zaidi ya mita za mraba elfu 45 zilizochorwa katika enzi 10. Pia kuna sanamu 245 zenye rangi, majengo matano yaliyojengwa kwa ubao ya enzi za Tang na Song, nguzo zenye nakshi ya mayungiyungi na maelfu ya marumaru yenye mapambo sakafuni. Tukiunganisha picha zote pamoja, zitaweza kuwa na urefu kilomita 25, ambao utakuwa wa kipekee duniani.

    Mwanzilishi wa mapango ya Mogao huko Dunhuang ni sufii Lezun. Ili kuweza kuchora picha kwenye miamba, wasanii wa enzi mbalimbali walipaka matope yaliyochanganywa na majani kutani na madari ya mapango kwanza, halafu wakapaka udongo mweupe na mwishowe walianza kuchora picha. Baada ya kumaliza kuchora picha walifnyanga sanamu zenye rangi. Katika mapango hayo picha kubwa kabisa ina urefu wa zaidi ya mita 40 na upana zaidi mita 30, na picha ndogo kabisa inaurefu usiozidi futi moja.

    Picha nyingi za Dunhuang zinasimulia hadithi za dini ya buddha. Kwa mfano, katika pango la 257 kuna picha za enzi ya Wei ya Kaskazini zinazosimulia hadithi ya msahafu wa dini ya buddha kuhusu swala wenye rangi tisa.

    Picha zilizochorwa ukutani za Dunhuang ni pamoja na picha za buddha, miungu, mizimu, wanyama, milima, mito, majengo na nakshi za mapambo. Picha hizo ni hazina kubwa ya sanaa ya dini ya Buddha, zimeonesha sifa tofauti za michoro ya enzi mbalimbali. Picha hizo zilizochorwa mwanzoni ni za aina fulani ya magharibi ya China, baadaye ni za aina ya kabila la Wahan. Si kama tu zimeona maendeleo ya sanaa ya picha za ukutani katika enzi kumi, pia zimeonesha mambo mengi kuhusu historia, mila, desturi, hadithi, milima na majengo ya China.


1  2  3