Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-10 20:32:54    
Kamati ya hadhi ya wanawake ya Umoja wa Mataifa yafanya mkutano kutathmini mafanikio ya mkutano wa wanawake duniani uliofanyika mjini Beijing

cri

Mkutano wa 49 wa kamati ya hadhi ya wanawake ya Umoja wa Mataifa ulifunguliwa tarehe 28 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York. Maofisa kutoka serikali za nchi zaidi ya 180 duniani na wawakilishi wa mashirika zaidi ya 100 yasiyo ya kiserikali wanahudhuria mkutano huo ambapo watatathmini mafanikio yaliyopatikana katika miaka kumi iliyopita ya mkutano wa wanawake duniani uliofanyika mjini Beijing na hali ya wanawake duniani.

Mkutano huo wa siku 12 utajadili utekelezaji wa Taarifa ya Beijing na mpango wa utekelezaji uliopitishwa kwenye mkutano wa nne wa wanawake duniani uliofanyika mjini Beijing mwaka 1995, kutafiti mabadiliko ya hadhi ya wanawake dunaini na kujadiliana masuala kadhaa kuhusu kuzidi kulinda maslahi ya wanawake na watoto.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan alihudhuria ufunguzi wa mkutano huo na kutoa hotua akitaka nchi mbalimbali duniani zichukue hatua halisi kuwaheshimu wanawake na kuwalinda watoto. Alisema kuwa, mkutano wa wanawake duniani uliofanyika miaka 10 iliyopita, ulikubali wazi kuwa usawa wa jinsia ni muhimu sana kwa amani na maendeleo ya dunia. Katika miaka kumi baadaye, wanawake wanatambua wazi zaidi haki zao na kuwa na haki nyingi zaidi, na wanawake na watoto wa kike wamepata faida nyingi zaidi.

Bw. Annan alieleza kuwa, suala la haki za wanawake bado linakabiliwa na changamoto kubwa, kwa mfano usafirishaji wa wanawake na watoto bado unaendelea, ni vigumu kwa watoto wa kike kupata fursa ya kusoma katika nchi zinazoendelea, na tishio la ugonjwa wa Ukimwi ni kubwa zaidi kwa wanawake. Lakini matatizo hayo yataweza kutatuliwa, binadamu wanaweza kushinda changamoto hizo kwa akili yao. Ripoti ya mradi wa milenia imetoa mapendekeo 7. Bw. Annan anatumai kuwa nchi mbalimbali duniani zitafanya juhudi kutatua matatizo hayo.

Bw. Annan alisisitiza kuwa, kusukuma mbele haki za wanawake ni wajibu wa binadamu wote. Njia inayofaa ya kutimiza maendeleo ni kuwapa wanawake haki zao. Wanawake wakipewa na haki zao, uchumi utapata maendeleo, vifo vya watoto wachanga vitapungua, ugonjwa wa ukimwi utadhibitiwa, watoto watapata elimu ya kutosha, migogoro itasimamishwa mapema, na mchakato wa amani utaharakishwa. Kwa ujumla, kuwapatia wanawake haki zao kutaipatia jamii ya binadamu faida nyingi.

Mkutano wa nne wa wanawake duniani uliofanyika mwaka 1995 mjini Beijing ulipitisha mpango wa utekelezaji ambao ni muhimu katika historia. Mkutano maalum wa 23 wa baraza la Umoja wa Mataifa uliofanyika mwezi Juni mwaka 2000 ulipitisha taarifa ya kisiasa, ikikubali kutathimini utekelezaji wa mpango huo kila baada ya muda, na kuzikusanya pande husika kutathimini maendeleo ya mpango huo na kujadili mapendekezo mapya mwaka huu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-08