Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-11 14:19:30    
Umoja wa Mataifa watoa mwito kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mapambano dhidi ya ugaidi.

cri

Mkutano wa kimataifa wa siku tatu kuhusu demokrasia, mapambano dhidi ya ugaidi na usalama ulifungwa tarehe 10 huko Madrid, Hispania, ambapo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alitoa ripoti ya "Mikakati ya mapambano dhidi ya ugaidi ya dunia nzima", akisisitiza kuwa nchi mbalimbali duniani zinapaswa kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Bwana Annan alisema kuwa, ugaidi ni tishio moja kubwa linaloikabili dunia nzima katika karne ya 21, Umoja wa Mataifa unapaswa kufuatilia zaidi suala la ugaidi. Katika ripoti yake Bwana Annan ametoa mikakati mitano mikubwa kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi, yaani nchi mbalimbali zinapaswa kukinga na kuzuia shughuli za ugaidi, ugaidi unapaswa kulaaniwa katika hali yoyote na utamaduni wa aina yoyote; nchi mbalimbali zinapaswa kuzuia mbinu za magaidi za kuanzisha mashambulizi, kuimarisha usimamizi wa usafirishaji bidhaa nje, kuwazuia magaidi wasipate vifaa vya nyuklia na silaha kali, pia zinapaswa kupambana na vitendo vya kuingiza fedha haramu kwenye mzunguko wa fedha; kutounga mkono ugaidi; kuongeza uwezo wa kuzuia shughuli za magaidi, kuanzisha na kudumisha mfumo wa utekelezaji sheria wenye ufanisi mkubwa ili kulingana na mahitaji ya mapambano dhidi ya ugaidi; na lazima kuheshimu na kulinda haki za binadamu wakati wa kupambana na ugaidi. Bwana Annan ameyataka mashirika yote ya Umoja wa Mataifa lazima yasaidie kutekeleza mikakati hiyo ya dunia nzima.

Kulinda amani na usalama wa dunia ni jukumu la kwanza la Umoja wa Mataifa, na mapambano dhidi ya ugaidi ni changamoto mpya inayoukabili Umoja wa Mataifa katika hali mpya ya historia, ambayo haikwepeki, na mapambano dhidi ya ugaidi pia yamekuwa suala linalofuatiliwa pamoja na jumuiya ya kimataifa siku hadi siku. Hivi sasa mikataba ya kimataifa au nyaraka za sheria zilizotungwa na Umoja wa Mataifa na shirika lake husika zimefikia 12. Baada ya tukio la tarehe 11 Septemba nchini Marekani, Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilianzisha pia kamati maalum ya kupambana na ugaidi. Mkutano kuhusu ugaidi ulifanyika mmoja baada ya mwingine, ambapo Mkutano maalum wa 4 wa kamati ya mapambano dhidi ya ugaidi ulifanyika mwezi Januari mwaka huu huko Almaty, Kazakhstan; mkutano wa kimataifa wa mapambano dhidi ya ugaidi ulifanyika tena mwezi Februari huko Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia; na mkutano wa mapambano dhidi ya ugaidi ulioandaliwa na Klabu ya Madrid iliyoundwa na wakuu zaidi ya 50 wa zamani wa nchi au serikali umefanyika wakati wa kukumbuka mwaka mmoja tangu tukio la ugaidi la tarehe 11 Machi Madrid litokee, mikutano hiyo yote imeonesha ufuatiliaji mkubwa wa jumuiya ya kimataifa kuhusu suala la ugaidi.

Ingawa nchi mbalimbali duniani zimefanya ushirikiano na kupata mafanikio kadhaa katika kupambana na ugaidi, lakini bado zina migongano mikubwa kuhusu namna ya kuthibitisha suala la kimsingi kuhusu shughuli za ugaidi. Baadhi ya watu walidhihirisha kuwa, shughuli za ugaidi kabisa siyo matukio kama tukio la tarehe 11 Septemba peke yake, suala hilo lina maana kubwa zaidi, lazima kuhusisha juhudi za kupambana na ugaidi na shughuli za uuzaji haramu wa silaha, silaha za nyuklia, silaha za viumbe na kemikali na silaha nyingine kali, ili kupambana na ugaidi wa aina yoyote. Lakini masuala hayo ni nyeti ambayo yanahusiana pia na sera za sasa za nchi kadhaa, hivyo nchi mbalimbali bado hazijafikia kauli moja kuhusu masuala hayo. Lakini zimeona kuwa kwanza lazima kuthibitisha maana ya ugaidi itakayoweza kukubaliwa na nchi zote.

Kuhusu suala hilo Bwana Annan alisema kuwa jumuiya ya kimataifa inapaswa kuthibitisha maana ya ugaidi kutokana na msingi uliothibitishwa na kikundi cha watu mashuhuri cha suala la mageuzi cha Umoja wa mataifa, yaani mtu au watu kutumia kwa makusudi mbinu za kuwaogopesha au kuwalazimisha watu kukidhi matakwa yao na kusababisha vifo na majeruhi ya raia, kitendo chochote kama hicho ni cha ugaidi. Bwana Annan amedhihirisha pia kuwa, lazima kuhamasisha nguvu zote za jumuiya ya kimataifa kufanya juhudi ili kupata ushindi katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-11