Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-11 15:33:57    
Wafanyabiashara wa China wanaoanzisha kituo cha biashara cha China nchini Afrika kusini.

cri

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na maendeleo ya kasi ya uchumi wa China, serikali ya China inahamasisha makampuni na matajiri wa China kwenda nchi za nje kuwekeza vitega uchumi. Hivyo wachina wanaoanzisha shughuli zao nchi za nje wanaongezeka siku hadi siku.

Watu wa Wenzhou wa mkoa wa Zhejiang, mashariki ya China wanajulikana kuwa ni watu wenye akili nyingi za kufanya biashara nchini China, ambao wameanzisha kituo cha maduka ya Wenzhou nchini Cameroon, hivi karibuni wanafanya maandalizi ya kuanzisha kituo cha maduka ya Wenzhou,China nchini Afrika ya kusini ambacho kitauza bidhaa zinazotengenezwa nchini China.

Mkurugenzi wa Shirikisho la wafanyabiashara wa Zhejiang la kusini mwa Afrika ambaye pia ni meneja mkuu wa kundi la biashara la kimataifa la Hushi la Afrika ya kusini Bwana Hu Liming mwenye umri wa miaka 47 mwaka huu alimwambia kwa furaha mwandishi wa habari kuwa, hivi karibuni yeye na mfanyabiashara wa Hongkong wakishirikiana wamenunua ardhi yenye eneo la kilomita za mraba elfu 50 huko Johannensburg, na wanafanya maandalizi ya kuanzisha kituo cha maduka ya Wenzhou,China. Wafanyabiashara wa Wenzhou,China wameanzisha kituo kama hicho nchini Marekani, Russia, Ujerumani, Uholanzi na nchi za falme za kiarabu, na pia wanafanya maandalizi ya kujenga kituo kama hicho nchini Uingereza.

Ardhi iliyonunuliwa na Bwana Hu Liming na mshiriki wake iko katika mtaa uliostawi mjini Johannesburg, ambayo inafaa sana kwa kujenga kituo cha maduka. Bwana Hu alisema kuwa, kwenye ardhi hiyo, kuna majengo ya mita za mraba 1600 yaliyokamilika, baada ya kufanyiwa ukarabati kwa miezi 6 hadi 10, maduka 180 yataanzishwa ndani; na baada ya ujenzi wa kipindi cha pili na cha tatu maduka mengine 600 yataanzishwa tena ndani; wakati kukamilika ujenzi wa mradi mzima, kituo hicho kitakuwa na maduka 800.

Bwana Hu Liming ana imani kuwa juu ya mustabali wa kituo chake cha maduka. Alisema kuwa, licha ya wafanyabiashara kutoka mkoa wa Zhejiang,China, kituo hicho kinawakaribisha watu wote wa China, wazungu, waafrika, wahindi na waarabu kuanzisha maduka yao kwenye kituo hicho. Alieleza kuwa maduka yatakayoanzishwa kwenye kituo hicho yatakuwa ya aina mbaimbali, duka kuba itakuwa na mita zaidi ya 100 za mraba, na duka dogo litakuwa na mita 30 za mraba tu.

Kituo cha maduka cha Weuzhou,China kiko karibu n "Kituo cha biashara cha Hongkong,China" mjini Johannesburg, siku za baadaye vituo hivyo viwili vitaungana kwa daraja la barabarani. Meneja wa Kituo cha biashara cha Hongkong,China Bwana Lin Sheng ni mwenye hisa pia wa Kituo cha maduka ya Wenzhou,China, siku za baadaye atatumia njia yake ya kihongkong kuendesha Kituo cha maduka ya Wenzhou,China, kwani ameendesha vizuri Kituo cha biashara cha Hongkong, China. Bwana Lin aliema kuwa, tangu kuanzishwa kwa Kituo cha biashara cha Hongkong,China huko Johannesburg mwaka jana, kituo hiki kimepata ufanisi mzuri. Kwenye kituo hicho, kuna maduka ya aina mbalimbali yanayouza nguo, vitu vya kuchezea kwa watoto na vitu vingine vingi. Wafanyabiashara kwenye kituo hicho walitoka sehemu mbalimbali duniani. Kituo hicho licha ya kuuza maduka na kutoza kodi, pia kinatoa huduma ili kuwahakikisha wafanyabishara wa kituo hicho wanaweza kuchuma pesa. Bwana Lin alisema kuwa kituo hicho kina ufanisi mzuri, kwa wastani kila duka linaweza kuuza bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 1.6.

Bwana Lin Shen alisema kuwa, mwaka huu kituo hicho pia kimekabiliwa na changamoto kubwa, hasa hali ya usalama nchini Afrika ya kusini. Ili kupambana na majambazi, kituo hicho kimelazimika kutumia pesa nyingi kuwaajiri askari ulinzi 24 na kuwanunulia silaha ili kulinda usalama kutwa kucha.

Ingawa hali ya usalama siyo nzuri nchini Afrika ya kusini, lakini wafanyabiashara wa China hawataki kuondoka kutokana na hofu. Bwana Lin Liming aliema kuwa, ingawa hawawezi kuhakikishiwa usalama, lakini biashara zao nchini humo zinaendelea vizuri, ambapo wanaweza kupata fursa nyingi, hivyo wafanyabiashara wa China wanaedelea na shughuli zao nchini humo.

Wasikilizaji wapendwa, mlikuwa mkisikiliza maelezo kuhusu wafanyabiashara wa China wanaoanzisha kituo cha biashara nchini Afrika ya kusini. Hadi hapo ndio kwa leo tumekamilisha kipindi hiki cha Daraja la urafiki kati ya China na Afrika, ni mtangazaji wenu

Idhaa ya kiswahili 2005-03-11