Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-14 15:01:47    
Kwa nini Marekani na Ulaya zimebadili sera zao katika suala la nyuklia la Iran

cri

    Mazungumzo ya duru la nne kati ya Nchi tatu za Ulaya Ufaransa, Ujerumani na Uingereza na Iran yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita hayakupata mafanikio. Wakati huo, kinyume cha kawaida Marekani ilitangaza ghafla kuwa itachukua "hatua ya kuuhimiza uchumi" kwa Iran, wakati huo Ufaransa, Ujerumani na Uingereza, ambazo zilisisitiza kutatua suala la nyuklia la Iran kwa amani, zilidai kuwa iwapo Iran itaanzisha tena shughuli za uranium nzito, basi Umoja wa Ulaya utakubali kuwakilisha suala hilo kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa nini misimamo ya Marekani na Ulaya imebadilika?

    Maoni ya raia wa Ulaya ni kuwa, hali hiyo kwa kweli ni matokeo ya Marekani na Ulaya kufikia makubaliano ya kikanuni katika suala la nyuklia la Iran. Maoni ya raia wa Ulaya yanakadiria kuwa, kubadili sera kwa Marekani kutaathiri mwelekeo wa suala la nyuklia la Iran katika siku za usoni; mashindano ya pande tatu za suala la nyuklia la Iran yataingia katika kipindi kipya.

    Habari zinasema kuwa, Marekani na Ulaya tarehe 11 zilikubaliana kuwa "zitasema kwa kauli moja" katika suala la nyuklia la Iran katika siku za usoni: Marekani haitapinga ombi la Iran kujiunga na Shirika la Biashara Duniani(WTO), na kuzingatia masuala moja baada ya lingine kuhusu Umoja wa Ulaya kuiuzia Iran vipuri vya ndege za abiria; na Umoja wa Ulaya pia utabadili msimamo wake, na kukubali kuwa kama mazungumzo kati yake na Iran yakishindwa, basi utalikabidhi suala hilo kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

    Wachambuzi wanaona kuwa, sababu za Marekani kubadili msimamo wake ni kwamba:

    Kwanza, Marekani inafahamu kuwa kama itaendelea na msimamo wake mkali kwa Iran, na haitazijali nchi tatu za Ulaya, basi Ulaya hautaamini kama madai ya Marekani "kusawazisha uhusiano wa nchi za kando mbili za Bahari ya Atlantic" ni ya dhati. Hivi sasa, masuala mengi ya kimataifa yanayoikabili Marekani yanahitaji uungaji mkono wa Ulaya, hivyo Marekani inapaswa kufanya mambo kadhaa ili kuboresha ushusiano kati yake na Ulaya.

    Pili, watu wameona kuwa, ingawa kwa siku nyingi Marekani inachukua msimamo mkali kwa Iran, lakini haikupata mafanikio. Hali hii haitaathiri tu heshima yake ya kidiplomasia katika kushughulikia suala la kutosambaza silaha kali, bali pia itaathiri "mpango wake wa mageuzi ya kidemokrasia ya Mashariki ya Kati".

    Tatu, vita ya Iraq imeifanya Marekani kutoweza kuanzisha vita nyingine; na Marekani mpaka sasa haina "ushahidi wa kutosha" kuhusu Iran kuendeleza silaha za nyuklia.

    Wachambuzi pia wanaona kuwa, kwa kweli Marekani haiamini kama kuna uwezekano wa kuilazimisha Iran kuacha mpango wake wa nyuklia kwa njia ya mazungumzo. Jambo inalozingatia ni kuwa kama mazungumzo yakishindwa, basi Umoja wa Ulaya na wanachama wa Shirika la Nishati ya Atomiki Duniani(IAEA) hazina budi kukubali Marekani kuwasilisha suala la nyuklia la Iran kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

    Kwa upande wa nchi tatu za Ulaya, zimefanya mazungumzo kwa duru nne na Iran, lakini hazikupata maendeleo. Zimeona kuwa mazungumzo hayatapata mafanikio bila ya msaada wa Marekani, kwa kuwa kwa upande mmoja wa Umoja wa Ulaya hauwezi kutimiza ahadi ya kuisaidia Iran kujiunga na WTO. Sasa umepata uungaji mkono kutoka Marekani, hivyo nguvu za nchi hizo tatu zimeimarishwa. Inakadiriwa kuwa, nchi hizo tatu zitazidi kutoa shinikizo kubwa kwa Iran ili kupata mafanikio.

    Iran inasisitiza kuwa itaendelea na utafiti wa kutumia kiamani nishati ya nyuklia na haitaacha haki yake ya halali. Lakini wachambuzi wanaona kuwa, kadiri mazungumzo yanavyoendelea, Iran inapaswa kufanya uamuzi wake kwa mujibu wa jinsi Iran inavyoelewa hali.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-14