Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-14 15:38:22    
Mapato ya wakulima na wafugaji wa Tibet yaongezeka kwa zaidi ya asilimia kumi kwa miaka miwili mfululizo

cri

Baada ya mapato ya wakulima na wafugaji wa mkoa unaojiendesha wa Tibet kufikia wastani wa yuan RMB 1690 mwaka 2003, ambayo yaliongozeka kwa asilimia 11.1 kuliko mwaka 2002, mapato yao ya mwaka 2004 yalifikia wastani wa yuan za RMB 1863, na kuongezeka kwa asilimia 10.2 kuliko mwaka 2003, ambayo iliongezeka zaidi ya asilimia kumi kwa miaka miwili mfululizo.

Mkuu wa idara ya kilimo na mifugo ya Tibet Bw. Jian Can alifahamisha kuwa, kuongezeka kwa kasi na kwa hatua madhubuti kwa mapato ya wakulima na wafugaji kunatokana na kilimo na ufugaji maalumu, uendeshaji wa shughuli za aina mbalimbali na usafirishaji wa nguvu kazi kwa sehemu za nje.

Katika miaka ya karibuni, kwa lengo la kuzidisha njia ya kuongeza mapato ya wakulima na wafugaji, mkoa wa Tibet umefanya juhudi kuongeza ubora wa mifugo katika muda mfupi, kutoa maziwa mazuri, kukuza sekta za ufugaji wa nguruwe wa kitibet na kuku wa kitibet kwenye msingi ambao utoaji wa nafaka kutokuwa chini ya tani laki 9.5. Aidha, mkoa huo unafuatana na masoko, umepunguza eneo la upandaji wa mazao ya chakula cha kijadi, kuzidisha eneo la upandaji wa shayiri, chakula kizuri cha mifugo, na mazao mengine ya uchumi, na kubadilisha uwiano wa mazao ya chakula, ya uchumi na chakula cha mifugo uwe 71: 19: 10 wa hivi sasa. Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka 2004 mapato ya wakulima na wafugaji wa Tibet kutokana na mazao ya kilimo na ufugaji na sekta maalumu yalichukua zaidi ya asilimia 30 katika mapato ya mwaka mzima kwa kila mtu.

Hoteli za familia katika sehemu za kilimo na ufugaji, maduka ya bidhaa za utalii, na viwanda vya kutengeneza mazao ya kilimo zimekuwa moja ya njia za kuongeza mapato ya wakulima na wafugaji. Mwaka 2004 mapato ya jumla ya watu hao mkoani Tibet kutokana na uendeshaji mbalimbali yalifikia yuan za RMB bilioni 2.1, na kuongezeka kwa asilimia 18 kuliko mwaka 2003.

Katika upande wa usafirishaji wa nguvu kazi kwa sehemu za nje, mkoa wa Tibet umeanzisha utaratibu kikamilifu wa shirikisho la usafirishaji wa nguvu kazi kwa sehemu za nje la sehemu, wilaya na vijiji, na kuyaunga mkono mashirika kuandikisha nguvu kazi wa ziada kwenye sehemu za kilimo na ufugaji kwa kutoa sera nzuri za kutangaza zabuni kujenga miradi, ushuru wa mashirika, na mipango ya miradi. Hivi sasa mkoa wa Tibet umesaidia kuanzisha makundi maalumu zaidi ya 50 ya kujenga miradi ya wakulima na wafugaji, yenye wafanyakazi elfu 12. Mwaka 2004 idadi ya wakulima na wafugaji waliosafirishwa kwa sehemu za nje mkoa mzima ilifikia laki 5.4, mapato kutokana na usafirishaji huo yalifikia yuan milioni 630.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-14