Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-15 14:33:52    
Mkutano wa 61 wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wafunguliwa

cri

    Mkutano wa 61 wa kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ulifunguliwa tarehe 14 huko Geneva. Mkutano huo utajadili mada kuhusu haki za binadamu.

    Kwa mujibu wa takwimu kutoka ofisi ya sekretariati ya mkutano huo, wajumbe rasmi wa nchi mbalimbali na wajumbe wa jumuiya zisizo za kiserikali zaidi ya 5,000 wanahudhuria mkutano huo. Mkutano wa wiki ya kwanza ni mkutano wa ngazi ya juu, ambapo maofisa zaidi ya 90 wa ngazi ya juu kutoka nchi mbalimbali watatoa hotuba kwenye mkutano huo.

    Kama ilivyokuwa zamani, mkutano huo utaendelea kwa wiki 6, unakadiriwa kumalizika tarehe 22, mwezi Aprili. Mkutano huo utasikiliza ripoti za baadhi ya wachunguzi 41 wa haki za binadamu. Hatimaye utafanya upigaji kura kwa maazimio na maamuzi 120, yakiwemo miswada ya maazimio kuhusu namna ya kulinda haki za binadama na uhuru wa kimsingi katika mapambano dhidi ya ugaidi, na kupiga marufuku kutesa wafungwa.

    Mwenyekiti wa mkutano huo Bw. Makarim Wibisono, ambaye pia ni mwakilishi wa Indonesia katika ofisi ya Geneva ya Umoja wa Mataifa aliendesha ufunguaji wa mkutano huo. Aliomboleza vifo vya watu waliokufa katika maafa ya tsunami kwenye bahari ya Hindi yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana, na kusema kuwa nchi zote lazima zishirikiane ndipo zinapoweza kushinda maafa ya kimaumbile. Pia alisema kuwa, jumuiya ya kimataifa lazima ifanye mapambano dhidi ya ugaidi kwa msingi wa kuheshimu haki za binadamu. Kwenye mkutano ofisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu Bw. Louise Arbour alipopongeza alisema kuwa, haki za maendeleo, uchumi, jamii na utamaduni haziwezi kutengana na wananchi na haki za siasa, kwa kuwa baada ya mtu kuwa na heshima ndipo anapoweza kutimiza haki mbalimbali za binadamu.

    "Kundi lenye misimamo inayolingana" linaloundwa na nchi karibu 20 zinazoendelea limekuwa ni kundi muhimu katika sekta ya haki za binadamu ya kimataifa katika miaka ya karibuni. China mwaka huu inaendelea na kipindi chake kuwa msuluhishi wa kundi hilo. Kwenye ufunguzi wa mkutano huo, mkuu wa ujumbe wa China katika Umoja wa Mataifa huko Geneva Bw. Sha Zukang alieleza msimamo wa pamoja wa China na nchi nyingine zinazoendelea kuhusu mageuzi ya mkutano wa haki za binadamu na kazi yake. Alisema, kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa baada ya kuanzishwa, iliwahi kufanya kazi muhimu katika kuhimiza na kulinda haki za binadamu duniani. Lakini katika miaka ya karibuni, kamati hiyo imekuwa ni jukwaa la mashindano ya kisiasa. Baadhi ya nchi za magharibi hazijali masuala yao ya haki za binadamu, lakini zinatumia mkutano huo kuziaibisha nchi zinazoendelea kutokana na mahitaji yao ya siasa. Hatua hiyo inaharibu heshima ya kamati ya haki za binadamu. Hivi sasa, kamati ya haki za binadamu imekwenda kinyume cha madhumuni na lengo lake. Bw. Sha alizitaka nchi wanachama za kamati hiyo zifanye zaidi ushirikiano na mazungumzo, pia alisisitiza kuwa ni lazima kufanya mageuzi kwa mfumo maalum wa kamati hiyo ili kuimarisha kazi yake.

    Kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ilianzishwa mwaka 1946, ambayo ni idara maalum ya Umoja wa Mataifa ya kukagua na kujadili suala la haki za binadamu. Mwaka 1992, nchi wanachama wake walifikia 53, na kipindi chake kuwa ni miaka mitatu. Katika kipindi cha mkutano wa haki za binadamu, licha ya nchi wanachama 53, nchi wanachama wengine wa Umoja wa Mataifa, idara mbalimbali, jumuiya za kikanda, jumuiya zisizo za kiserikali pia zinaweza kuwa wachunguzi kuhudhuria mkutano huo.

    Baada ya kurudishwa uanachama kwenye Umoja wa Mataifa mwaka 1971, China imeanza kushiriki kwenye majadiliano ya baraza la Umoja wa Mataifa na baraza la uchumi na jamii kuhusu suala la haki za binadamu. Mwaka 1981, China ilichaguliwa kuwa mwanachama wa kamati ya haki za binadamu kwenye mkutano wa kwanza wa baraza la uchumi na jamii la Umoja wa Mataifa, na kuendelea na uanachama wake hadi sasa.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-15