Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-15 15:13:44    
Mchakato wa amani nchini Cote D'ivoire umekwama

cri

Kikundi hicho cha wanasheria kilichoongozwa na waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini Bw. Mosiuoa Lekota kiliwahi kukutana na wajumbe wa vikundi mbalimbali vya Cote d'Ivoire na kilitoa mapendekezo ya mageuzi ya sheria ili kuridhia matakwa ya "mkataba wa amani wa Marcoussis" uliotiwa saini mwezi Januari mwaka 2003 na kuanza tena mchakato wa amani nchini humo. Bw. Mosiuoa Lekota pia atajadiliana na vikundi mbalimbali kuhusu tatizo la usalama wa nchini na hasa tatizo la kuvunja nguvu za kijeshi za vikundi mbalimbali.

Mwishoni mwa mwaka jana, kikundi cha upinzani cha "Nguvu Mpya" kilitangaza kujitoa kwenye mchakato wa kuvunja nguvu za kijeshi na kujiondoa kutoka serikali ya usuluhishi wa makabila, pia kiliafikiana na vikundi vingine kuhusu vifungu vya kuvunja nguvu za kijeshi ndani ya mkataba wa amani na mageuzi ya kisheria. Kisha bunge la Cote d'Ivoire lilipitisha katiba iliyorekebishwa ambayo imefutwa baadhi ya masharti ya uchaguzi, na marekebisho yamemwezesha waziri mkuu wa zamani na viongozi wa vikundi vya upinzani kushiriki kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba. Lakini kwa mujibu wa katiba, ratiba iliyorekebishwa lazima ipitishwe kwa kura za maoni ya wananchi kabla ya kutekelezwa, kikundi cha wanasheria kitatoa mapendekezo kuhusu mageuzi ya sheria na hasa upigaji kura za maoni za wananchi ili kutimiza vifungu vya sheria ndani ya mkataba wa amani vinavyoweza kutekelezwa, kikitumai kulazimisha "nguvu mpya" kuweka chini silaha.

Msimamo wa "Nguvu Mpya" kukataa kuvunja nguvu za kijeshi ni kidonda cha mchakato wa amani nchini Cote d'Ivoire. Kikundi hicho kinadai kuwa serikali haikutekeleza vilivyo hatua za mageuzi zilizoandikwa kwenye mkataba wa amani. Kikundi cha wanasheria cha Umoja wa Afrika hivi sasa kinajitahidi kusaidia serikali kukamilisha mageuzi hayo ili kuondoa kisingizio cha "nguvu mpya" cha kukataa kuvunja kwa nguvu za kijeshi.

Lakini kutokana na hali ilivyo sasa nchini humo, hata serikali ikikamilisha mageuzi mchakato wa amani pia utakumbwa na matatizo mengi. Kwanza tokea mwezi Septemba mwaka 2002 vita vya wenyewe kwa wenyewe vianze, "nguvu mpya" imeimarika siku hadi siku hata imedhibiti sehemu ya kaskazini ya nchi hiyo, na nia yake ya kuimega sehemu ya kaskazini iwe yake imekuwa wazi zaidi. "Nguvu mpya" haitaweka chini silaha mpaka ipate ushindi kwenye uchaguzi mkuu.

Pili, "nguvu mpya" hivi karibuni itatangaza "tahadhari kwa vita", ikisema kuwa jeshi la serikali litachukua hatua za kijeshi na kusema kuwa kama ikishambuliwa haitachukua hatua za kujilinda tu, taarifa yake hiyo inamaanisha kuwa kikundi hicho cha "nguvu mpya" kinaweza kukataa kuweka chini silaha kwa kisingizio cha "usalama".

Tatu, uchaguzi mkuu umeamuliwa kufanyika mwezi Oktoba. Lakini wataalamu wanaona kuwa matayarisho ya uchaguzi huo yanahitajika miezi 18 au hata zaidi, kwa hiyo uchaguzi huo ni vigumu kufanyika kwa wakati. Na hata ukifanyika kwa wakati pia ni vigumu kuwa mwanzo wa mchakato wa amani.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-15