Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-16 14:54:47    
Pro.Shao Yiming afanya juhudi kubwa katika shughuli za kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi nchini China

cri

Pro. Shao Yiming

Mkutano wa tatu wa baraza la kumi la mashauriano ya kisiasa la China umemalizika siku za karibuni hapa Beijing, ambapo wajumbe zaidi ya 2000 wa baraza hilo wanaotoka sehemu mbalimbali nchini China walihudhuria mkutano huo na kutoa mapendekezo kwa ajili ya maendeleo ya China na ujenzi wa jamii yeneye masikilizano. Wengi wa wajumbe walioshiriki hao ni wasomi na wataalamu wa sekta mbalimbali. Katika kipindi cha leo, tunawaletea maelezo kuhusu mtaalamu wa China wa suala la ugonjwa wa ukimwi Pro. Shao Yiming.

Pro. Shao mwenye umri wa miaka 48, alikuwa mshauri wa suala la ugonjwa wa ukimwi duniani katika Shirika la Afya Duniani (WHO), na hivi sasa ni mtaalamu wa kwanza katika kituo cha kinga na udhibiti wa magonjwa ya zinaa na ukimwi cha China, na mkurugenzi wa maabara ya takwimu za ugonjwa wa ukimwi. Akiwa mwanasayansi kijana, Pro. Shao ametunukiwa tuzo tatu za taifa, na makala zake nyingi za taaluma zimechapishwa kwenye machapisho mengi ya nchini na ya nchi za nje. Mwaka 1992, alipata tuzo ya Mfuko wa Kimataifa wa Ugonjwa wa Ukimwi kwa utafiti wake kuhusu ugonjwa huo. Mwaka 2003, Pro. Shao alichaguliwa kuwa mjumbe wa baraza la kumi la mashauriano ya kisiasa la China, na katika miaka miwili iliyopita ametekeleza kwa makini wajibu wake na kutoa mapendekezo karibu 30 kuhusu masuala ya afya nchini China, hasa suala la ugonjwa wa ukimwi. Pendekezo moja Pro. Shao alilowasilisha kwenye baraza la mashauriano ya kisiasa la China mwaka 2003 wakati mkutano wa kwanza wa baraza hilo ulipofanyika, lilizingatiwa na viongozi wa China. Alimwambia mwadishi wa habari akisema:

"Nilifurahi sana wakati nilipoona kuwa katika mwaka mmoja baada ya pendekezo langu kutolewa, fedha zilizotengwa na serikali katika utafiti wa ugonjwa wa ukimwi zimeongezeka kuwa zaidi ya yuan milioni 20 kutoka milioni 1, na idadi ya watafiti imeongezeka kwa kiasi kikubwa."

Akiwa mtu ambaye yuko mstari wa mbele katika utafiti wa ugonjwa wa ukimwi, Pro. Shao alifuatilia sana hali ya maambukizi ya ugonjwa huo nchini China. Alifahamisha:

"Mpaka sasa ni karibu miaka minane tokea ugonjwa wa ukimwi nchini China uingie katika kipindi cha kuenea kwa kasi, na kasi yake bado ni kubwa sana. Takwimu nyingi zinazotokana na uchunguzi na utafiti zinaonesha kuwa hivi sasa kuna watu laki 8.4 ambao ni wagonjwa wa ukimwi au wameambukizwa virusi vya ukimwi."

Pro. Shao ni mmoja wa wataalamu waliofanya utafiti kuhusu ugonjwa wa ukimwi kwa muda mrefu nchini China. Mwaka 1985, alipokuwa mwanafunzi wa shahada ya pili, alishiriki kumtibu mgonjwa wa kwanza wa ukimwi nchini China, na alipokuwa mwanafunzi wa shahada ya tatu alishiriki katika miradi husika ya mpango wa sita wa taifa wa miaka mitano. Baada ya kupata shahada ya udaktari mwaka 1988, Bw. Shao alianzisha utafiti kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi nchini China, na alitoa pendekezo lililokuwa linaambatana na hali halisi ya wakati ule nchini China kuhusu kueneza dawa ya kutambua mara moja kama mtu ameambukizwa ugonjwa wa ukimwi au la katika hospitali vijijini, na pendekezo hilo limekuwa hatua moja muhimu ya China katika kuhakikisha usalama wa damu. Hivi sasa, Pro. Shao sio tu anaongoza kazi ya utafiti kuhusu ugojwa wa ukimwi katika mradi wa taifa wa "863" na "973", miradi inayoongoza katika miradi mingi ya taifa, bali pia anashiriki katika miradi mingi ya kimataifa. Aidha, Pro. Shao anaongoza kazi ya kutafiti na kutengeneza chanjo ya ugonjwa wa ukimwi nchini China.

Ingwa Pro. Shao amepata mafanikio makubwa katika utafiti, lakini anaona kuwa hivi sasa ugonjwa wa ukimwi kimsingi hauwezi kutibiwa, na bado uungaji mkono wa sera husika ya serikali unahitajika, matangazo na mafunzo kuhusu ujuzi wa ugonjwa huo na hatua zinazolenga watu wenye hatari kubwa zinapaswa kuimarishwa. Alisema:

"Katika miaka ya karibuni, serikali ya China imeimarisha zaidi kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi, na kutoa sera na kuchukua hatua nyingi za kuwasimamia watu walioambukizwa virusi vya ukimwi ili wapate matibabu, wakati virusi vinapoongezeka. Aidha, serikali ya China inafanya juhudi kuwaelimisha watu jinsi ugonjwa huo ulivyo, na kuchukua hatua kwa watu wenye hatari kubwa, hivyo, hivi sasa kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo imepungua."

Katika mkutano wa tatu wa baraza la kumi la mashauriano ya kisiasa la China unaofanyika hivi sasa, mjumbe Shao ametoa mapendekezo mawili kuhusu ugonjwa wa ukimwi: ya kwanza ni kuwa kamati kuu ya chama cha vijana na wizara ya afya iunde kikundi cha afya ambacho wajumbe wake ni vijana wanaojitolea, na kukifanya kikundi hicho kiwe sehemu muhimu ya shughuli za afya ya umma.

Kuhusu pendekezo hilo, mjumbe Shao alifahamisha kuwa mlipuko wa ugonjwa wa SARS ulikuwa onyo kwa wananchi, na kuwaonesha kuwa wanapaswa kuzingatia zaidi shughuli za afya. Hivi sasa jumuiya kadhaa za kiraia zimefanya kazi muhimu, lakini kutokana na uwezo wao mdogo, ni vigumu kwao kushiriki katika kazi kubwa ya kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi ya taifa. Kama kikundi cha vijana wanaojitolea kitaundwa, tutaweza kuzishirikisha jumuiya hizo ndogondogo na kushiriki kwa pamoja katika juhudi za kupambana na ugonjwa wa ukimwi za taifa. Alisema:

"Mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi yanahitaji muda mrefu, na mfumo wa kudumu, tunapaswa kuchukua hatua zenye ufanisi kwa muda mrefu. Katika vita hivyo dhidi ya ugonjwa wa ukimwi, tunapaswa kushirikisha idara mbalimbali za afya, na kutumia raslimali zote za matibabu, aidha, ni muhimu kuwahamasisha watu wote washiriki katika vita hivyo, huu ni uzoefu tulioupata kutokana na mafanikio ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi duniani."

Ushauri wake mwingine unahusu kuitaka serikali ilinde haki na maslahi halali ya wagonjwa wa ukumwi na watu walioambukizwa virusi vya ukimwi. Mswada huo unaofuatilia hali ya wagonjwa wa ukimwi na watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi unaonesha kuwa, sharti la kwanza la kudhibiti vizuri ugonjwa huo ni kudhibiti chanzo chake, yaani wagonjwa wa ukimwi na watu wanaoambukizwa virusi vya ukimwi, lakini watu hao walikuwa wanaogopa kukiri kuwa na virusi kutokana na unyenyepaa. Kutokana na uzoefu wa mafanikio katika kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi duniani, kulinda haki na maslahi halali ya watu hao na kuondoa unyenyepa ili wachukue hatua za kinga na tiba, kutainua ufanisi wa kazi yetu. Mjumbe Shao alisema:

"Naona kuwa kuwafuatilia wagonjwa wa ukimwi na watu walioambukizwa virusi vya ukimwi ni sehemu muhimu ya kazi ya chama cha kikomunisiti cha China na serikali ya China katika kujenga jamii yenye masikilizano. Hivyo natumai kuwa serikali itazingatia haki na maslahi halali ya wagonjwa wa ukimwi wakati itakapotunga kanuni mpya za kinga na tiba ya ugonjwa wa ukimwi."

Idhaa ya kiswahili 2005-03-16