Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-16 15:32:00    
Wanafunzi wanawake wa shule waliofanya kazi ya uyaya wapata mshahara mzuri nchini China

cri

Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na jinsi uchumi uchumi unavyoendelea haraka nchini China, mapato ya wachina yanaongezeka siku hadi siku. Ingawa maisha ya wachina yanaboreshwa sana, lakini watu wengi siku zote wanafanya kazi kwa bdii, hawana wakati wa kutosha kufanya kazi za nyumbani na kuwatunza watoto. Hivyo mayaya wenye elimu ya juu wanakaribishwa sana katika miji mikubwa nchini China.

Kampuni moja ya huduma ya za nyumbani mjini Guangzhou hivi karibuni iliwaandaa wanafunzi wanawake 12 waliohitimu kutoka shule ya matibabu ya kichina, na baada ya masomo ya siku 13 walianza kufanya kazi katika familia mbalimbali.

Meneja wa kampuni hiyo alijulisha kuwa, wanafunzi wengi waliosomea matibabu ya kichina si kama tu wanaweza kutoa huduma nyumbani, bali pia wanaweza kutibu magonjwa ya kawaida na kufanya usingaji. Kazi za mayaya hao ni kuwatunza wazee na watoto. Kikundi hiki cha mayaya wanafunzi 12 ni kama cha majaribio, lakini kutokana na matokeo ya kazi ya mwanzoni, mayaya hao walifanya vizuri sana, hivyo katika siku za baadaye, kampuni hiyo itaendelea kufanya ushirikiano na shule ya matibabu ya kichina ya Guangxi.

Baada ya sikukuu ya spring ya mwaka huu, mayaya wanahitajika sana mjini Guangzhou, kusini mwa China. Hivi sasa mshahara wa mayaya wa kawaida umeongeza kuliko mwaka jana, mwaka huu mshahara wa yaya mmoja unafikia Yuan 500 yuan kwa mwezi. Meneja wa kampuni ya huduma za nyumbani alidokeza kuwa, kutokana na hali ya soko, mshahara wa kikundi hiki cha mayaya wanafunzi umepangwa kuwa Yuan 900 kwa mwezi. Na wakifanya vizuri, mshahara utaongezwa zaidi baada ya muda wa mwezi mmoja..

Habari zinasema kuwa, kwa kulinganishwa na mayaya wa kawaida, ubora na uwezo wa mayaya wanafunzi ni mzuri zaidi. Mbali na kutibu magonjwa ya kawaida au kufanya usingaji, mayaya wanafunzi pia wanaweza kuwasaidia watoto kusoma.

Naibu mkuu wa shule ya matibabu ya kichina ya Guangxi Bw. Wu Bin alisema kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, ni vigumu kupata ajira kwa wanafunzi waliohitimu kutoka shule za mafunzo maalumu au vyuo vikuu, mwishoni mwa mwaka jana, chini ya msaada wa Kamati ya huduma za familia ya China, shule hiyo ilianza kufanya ushirikiano na kampuni ya huduma za familia. Bw. Wu Bin alisema, kwa kuwa, hivi sasa familia nyingi za China zinahitaji hudumu nzuri za familia, ambazo sio tu huduma kama za zamani zikiwemo kupika chakula, na kuwatunza watoto, bali watu wengi zaidi wanahitaji huduma za matibabu, afya na elimu.

Waandishi wa habari wametambua kuwa, kikundi hiki cha mayaya wanafunzi 12 wanaonekana, wanatofautiana na mayaya wa kawaida. Mwanafunzi mmoja alisema, hivi sasa kazi ya huduma za familia inahitaji watu wenye ujuzi, anajiamini atafanya vizuri kazi yake.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-16