Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-16 16:23:55    
Tiba ya ugonjwa wa ustaarabu wa kisasa

cri

Mtindo usiofaa wa maisha umesababisha watu wengi wa siku hizi kuugua ugonjwa wa ustaarabu wa kisasa, taarifa moja iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani mwaka 1997 ilisema, "utamaduni wa makochi na chips unahatarisha afya za watu". Mtaalamu wa elimu ya afya Dr. Zhao Lin alisema kuwa njia ya kimsingi kabisa ya kutibu ugonjwa wa ustaarabu wa kisasa ni kuachana na mtindo usiofaa wa maisha, kuwa na mpango mzuri wa chakula na kufanya mazoezi ya mwili.

Kutofanya mazoezi ya mwili kwa muda mrefu, si kama tu kutasababisha viungo vya mwilini kudhoofika vibaya na kusababisha ugonjwa, bali pia kunasababisha shinikizo zinazokabili binadamu katika jamii ya kisasa kutoweza kupungua, hatimaye kutasababisha matatizo ya mshipa wa neva hata ugonjwa wa akili. Wakati tunapofanya mazoezi ya mwili, sehemu fulani ya ujoto mwilini kutokana na chakula tulichokula utapotea; ujoto mwingi uliotokea mwilini kutokana na kufanya mazoezi, unapoondoka utatumia ujoto mwingine wa mwilini. Licha ya hayo, baada ya kufanya mazoezi, mwili wa binadamu utadumisha kwa muda kiwango cha juu ya matumizi ya ujoto, hivyo utatumia joto jingi mwilini. Tukiangalia kutoka upande huo peke yake, tutaona kuwa mazoezi ya mwili ni muhimu sana kwa kuhifadhi afya za binadamu. Tunapofuata mpango wa kufanya mazoezi ya mwili, tunatakiwa pia kupanga vizuri ratiba ya maisha na kazi zetu, kuongeza muda wa kupumzika na kulala usingizi.

Kutokea kwa baadhi ya ugonjwa wa ustaarabu ukiwa ni pamoja na kuwa na mafuta mengi ndani ya damu, mshipa wa damu wa ndani ya ubongo kubadilika kuwa mgumu, msukumo mkubwa wa damu katika mshipa, ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa utumbo wa chakula na hali ya kunenepa kupita kiasi, kuna uhusiano mkubwa na desturi mbaya ya chakula, hivyo kuwa na mpango mzuri wa chakula ni muhimu sana kwa afya za binadamu.

Kwa watu wanaofanya kazi za ofisini ni rahisi sana kupungukiwa na vitamin, watu hao wanakaa kwenye viti kwa saa nyingi ndani ya nyumba, na kutopatwa na mwangaza wa jua, hivyo ni rahisi kwao kupungukiwa vitamin D, kupendelea chakula cha aina fulani pia kunasabisha kupungukiwa na vitamin A, B1, B2 na C, ambazo zinaathiri kupata na kutumika kwa calcium, na kusababisha kuharibika kwa afya. Wataalamu wametoa mapendekezo kwa watu wanaofanya kazi maofisini. Usihangaike hata kama umekabiliwa na kazi nyingi; Uwe na mpango mzuri wa chakula kila siku, ule mboga na matunda kila mara, na usile nyama nyingi; Usivute sigara na usinywe pombe nyingi; jaribu kufanya mazoezi ya kukimbia na kupigwa mwangaza wa jua.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-16