|
Mkutano wa Umoja wa Ulaya uliofanyika mwezi Desemba mwaka jana uliamua kuanzisha mazungumzo na Croatia tarehe 17 mwezi huu kuhusu nchi hiyo kujiunga na Umoja huo. Lakini siku moja kabla ya siku hiyo, mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya umeamua kuahirisha mazungumzo hayo, hivyo mchakato wa Croatia kujiunga na Umoja wa Ulaya umekwama
Kisa chenyewe ni kuwa Umoja wa Ulaya ulikuwa na shari kwa kuanza mazungumzo na Croatia kuhusu nchi hiyo kujiunga na Umoja huo. Sharti hilo ni kuwa Croatia lazima ishirikiane kikamilifu na mahakama ya kimataifa ya mjini The Hague nchini Uholanzi. Lakini kwenye mkutano wa tarehe 16 nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Ulaya ziliona kuwa Croatia haikushirikiana vizuri na mahakama hiyo, kwa hiyo mkutano umeamua kuahirisha mazungumzo hayo. Suala kubwa katika ushirikiano kati ya mahakama ya kimataifa na Croatia ni kumkamata jemedari wa zamani wa Croatia Bw. Ante Gotovina na kumpeleka kwenye mahakama ya kimataifa.
Jemedari wa zamani wa Croatia Bw. Gotovina ana umri wa miaka 49, ni mmoja wa washitakiwa wanaotafutwa na mahakama ya kimataifa. Mahakama ya kimataifa inamhitaji kutokana na kuwa katika kipindi cha mwaka 1991 hadi 1995 cha vita vya Croatia aliwaua Waserbia 150. Mahakama ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kwa mara nyingi zilishinikiza Croatia imkamate Bw. Gotovina na kumkabidhi kwenye mahakama ya kimataifa mjini The Hague, lakini mpaka sasa Gotovina bado hajapatikana.
Kutokana na maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mahakama ya kimataifa ndani ya Croatia iliyoundwa mwaka 1993 inashughulikia tu kesi ya wahalifu wa vita wa miaka ya 90 katika Yugoslavia wenye hatia ya kuwaua watu na uhalifu dhidi ya ubinadamu. Mahakama hiyo ina haki ya kuwakamata watuhumiwa hao lakini haina askari polisi, kazi ya kuwakamata inategemea askari wa usalama wa kimataifa kwenye nchi na sehemu watuhumiwa walipo. Tokea mahakama hiyo kuundwa imewashitaki watuhumiwa 150, lakini mpaka sasa bado 17 hawajapatikana wakiwemo rais wa zamani wa Jamhuri ya Serbia Radovan Karadzic na jemedari mkuu Ratko Mladic, mbali na Gotovina.
Sababu ya Umoja wa Mataifa kusisitiza Croatia ishirikiane na mahakama ya kimataifa ni kuwa nchi zote za peninsula ya Balkan zinataka kujiunga na Umoja wa Mataifa, kwa kutumia suala la Croatia unataka kutoa ishara kuwa nchi yoyote ikitaka kujiunga na Umoja huo, lazima iridhie matakwa ya Umoja huo, pili ni kuhimiza kwa nchi zinazotaka kuukaribia Umoja huo kuwakamata watuhumiwa wa vita wanaotafutwa, hasa Gotovina. Lakini Croatia inayotaka kujiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 2007 imefanya juhudi kwa muda mrefu, kuhusu ushirikiano na mahakama ya kimataifa, serikali ya Croatia imesema itajitahidi kushirikiana na mahakama ya kimataifa ikiwa ni pamoja na hatua ya kuzuia mali za Gotovina, hata hivyo haijafanikiwa katika juhudi za kumsaka Gotovina.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Ulaya vinasema kuwa sio uadilifu kwa Umoja wa Ulaya kuilaani serikali ya Croatia kutoshirikiana kikamilifu na mahakama ya kimataifa, bali Umoja huo unapaswa ufikirie hali ilivyo ya Croatia. Hata ndani ya Umoja huo baadhi ya nchi wanachama wanaona kuwa sio hoja kuahirisha mazungumzo kwa sababu ya kutoweza kumkamata Gotovina. Waziri wa mambo ya nje wa Austria Bi. Ursula Plassnik tarehe 16 huko Brussels alisema, Umoja wa Ulaya unafaa kuona kuwa serikali ya Croatia imefanya mageuzi mengi na imepiga hatua katika ushirikiano na mahakama ya kimataifa, maoni kama hayo pia yanaonekana katika nchi nyingine wanachama kama Hungary, Slovenia, Slovakia.
Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya ulisema kuwa mlango wa Umoja wa Ulaya ni wazi kwa Croatia, mradi tu hali inapoiva, mazungumzo yataanza, lakini haukutaja mazungumzo hayo yatafanyika lini hasa.
Idhaa ya kiswahili 2005-03-17
|