Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-17 16:51:26    
Sera ya kujiendesha kwa maeneo ya makabila madogo yamehimiza maendeleo ya uchumi na jamii katika maeneo hayo nchini China

cri

Ofisi ya habari ya baraza la serikali hivi karibuni ilitoa waraka wa serikali kuhusu "Kujiendesha kwa maeneo ya makabila madogo nchini China". Waraka huo umetathmini na kueleza uzoefu na mafanikio yaliyopatikana katika muda wa zaidi ya miaka 50 tangu itekelezwe sera ya kujiendesha kwa maeneo ya makabila madogo. Watu wa makabila madogo madogo walisema kuwa, sera ya kujiendesha kwa maeneo ya makabila madogo nchini China imehimiza sana ujenzi wa uchumi na maendeleo ya elimu, utamaduni na sekta nyingine katika maeneo hayo.

China ni nchi yenye makabila mengi. Katika idadi ya watu bilioni 1.3, watu wa kabila la wahan wanachukua asilimia 91, na makabila mengine 55 yanachukua asilimia 9 tu ya idadi yote ya watu wa China. Hivyo makabila hayo 55 yanaitwa makabila madogo. Kuanzia miaka ya 50 ya karne iliyopita, China ilianza kushughulikia mambo ya makabila madogo kwa njia ya kujiendesha kwa maeneo ya makabila madogo.

Kati ya mikoa 34 nchini China, mikoa 5 ni mikoa inayojiendesha ya makabila madogo. Licha ya mikoa hiyo mitano, katika mikoa mingine yenye makabila madogo, pia zimewekwa wilaya zinazojiendesha za makabila madogo. Wakazi wa makabila madogo wana haki ya kushughulikia mambo yao. Hivi sasa, maeneo ya kujiendesha ya makabila madogo yanachukua zaidi ya nusu ya maeneo yote ya China.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi, sheria ya kujiendesha kwa maeneo ya makabila madogo na sheria nyingine, nyadhifa za ngazi ya juu kabisa katika sehemu zinazojiendesha lazima zinachukuliwa na watu wa makabila madogo. Na watu wa makabila madogo pia watachukua asilimia kubwa ya maofisa katika idara za serikali za ngazi tofauti.

Bwana Bai Zhao ni mjumbe wa bunge la mkoa unaojiendesha wa kabila la watibet. Alisema kuwa, serikali za maeneo ya kujiendesha kwa makabila madogo licha ya kushughulikia mambo ya makabila yao na ujenzi wa uchumi wao, pia zinaweza kutunga sheria na taratibu zinazoambatana na hali halisi ya makabila yao. Alisema:

"Bunge la umma la mkoa unaojiendesha wa kabila la watibet kwa nyakati tofauti lilikuwa limetunga na kuidhinisha sheria, taratibu na maazimio 237 ya kisehemu, ambazo zimetoa uhakikisho wa kisheria katika kusukuma mbele maendeleo ya uchumi, siasa, jamii na utamaduni wa mkoa huo."

Kwa mfano, vifungu vya marekebisho vya "sheria ya ndoa" vilivyotungwa na bunge la umma la Tibet si kama tu vimepunguza umri wa miaka ya kuoa na kuolewa, bali pia vimeruhusu kuendelea kuwepo kwa desturi ya zamani ya ndoa ya "mke mmoja na waume wengi", au "mume mmoja na wake wengi". Zaidi ya hayo, mkoa unaojiendesha wa kabila la watibet pia umetunga vifungu vya sheria vya kujifunza na kutumia lugha mitala ya kitibet, hifadhi ya mazingira, hifadhi ya vitu vya kale na kadhalika ili kuhakikisha mkoa huo uendeleze uchumi, jamii na mazingira kwa pamoja.

Watu wa makabila mengi madogo ya China wanaishi katika sehemu za mpakani, hivyo uchumi wao uko nyuma kidogo. Katika miaka mingi iliyopita, serikali kuu ya China imechukua hatua za kuunga mkono sehemu za makabila madogo katika mambo ya fedha, ushuru na hifadhi ya ardhi. Hivi sasa fedha zilizotengwa na serikali kuu kwa ajili ya kuhimiza maendeleo ya makabila madogo zimezidi yuan trilioni moja.

Bw. Long Yuanwei wa kabila la wazhuang ni msomi wa Taasisi ya Sayansi ya Jamii ya China, aliwahi kutembelea sehemu nyingi za makabila madogo. Muda si mrefu uliopita alirudi maskani yake, sehemu ya Baise ya mkoa unaojiendesha wa Guangxi, ambayo wakazi wengi ni wa kabila la wazhuang. Alisema

"Mabadiliko ya sehemu ya Baise yananishangaza sana. Zamani hapa ilikuwa maskini sana, lakini sasa sehemu hiyo inatumia uzalishaji wa njia ya kisasa ya kilimo. Mashamba makubwa ya mboga, matunda na miwani yanaleta mapato makubwa kwa wakulima wa huko."

Bwana Long alisema kuwa, kutokana na sababu ya kihistoria na kijiografia, maeneo ya makabila madogo huwa yalikuwa maeneo yenye matatizo ya kiuchumi, lakini sasa barabara zimefika kila kijiji, wakazi wa vijiji vyote wanaweza kutumia simu, kusikiliza radio na kutazama televisheni, maisha ya wakazi wa maeneo hayo yamepata maendeleo makubwa kwa kweli.

Wakati wa kuinua kiwango cha maisha cha wakazi wa makabila madogo, serikali kuu pia imeimarisha kazi ya elimu katika maeneo hayo. Kama vile kueneza elimu ya lazima ya miaka tisa na kuwapa kipaumbele wanafunzi wa makabila madogo kuingia katika vyuo vikuu. Zaidi ya hayo, China pia imeanzisha vyuo vikuu 13 vya makabila madogo ili kuwaandaa makada wa makabila madogo.

Bw. Yang Jiangling aliyehitimu kutoka chuo kikuu kimoja cha makabila cha Beijing ni wa kabila la wadulong lililoko mkoani Yunnan, kusini magharibi mwa China. Kabila hilo lina idadi ya watu wasiozidi 6000, lakini limepata maendeleo makubwa katika sekta ya elimu katika miaka ya hivi karibuni. Bw. Yang alisema:

"Hivi sasa wakazi wengi wa kabila la wadulong wamepata elimu ya lazima ya miaka tisa. Kabila hilo limekuwa na watu zaidi ya mia moja waliohitimu masomo ya chuo kikuu. Katika hospitali, idara ya ujenzi na sekta nyingine za mji wa Kunming na miji mingine ya mkoa wa Yunnan, unaweza kuwakuta wasomi wa kabila la wadulong kwa urahisi."

Idhaa ya kiswahili 2005-03-17