Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-17 18:26:39    
Mwelekeo wa kuondoa jeshi nchini Iraq hauzuiliki

cri

Wakati inapotimia miaka miwili tangu kuanza kwa vita vya Iraq, nchi za Italia, Bulgaria, Ukraine na Ureno zilizoiunga mkono Marekani kuanzisha vita hivyo na kupeleka jeshi nchini humo, hivi sasa zote zilitoa ombi la kuondoa majeshi yao nchini Iraq. Kuhusu hali hiyo, Rais Bush wa Marekani jana alisema kuwa, anaelewa nia ya nchi hizo, lakini nchi hizo haziwezi kuondoa majeshi yao nchini humo mpaka polisi na kikosi cha kulinda usalama cha Iraq zitakapoweza kumudu kazi ya hivi sasa ya jeshi la muunganao tu,. Wachambuzi wanaona kuwa, ni vigumu kwa Marekani kuzishawishi nchi hizo kuendelea kubakiza majeshi yao nchini humo.

Kwanza, itachukua muda mrefu kutimiza amani nchini Iraq. Mchakato wa kisiasa wa Iraq uliobuniwa na Marekani unaendelea taratibu. Nchi washirika wa Marekani zinatambua siku hadi siku kuwa, baada ya vita, Iraq haikuingia kwenye "enzi mpya yenye demokraisia, uhuru na utajiri". Hali ya nchini Iraq na maisha ya wa-Iraq hayajaboreka; jeshi la muungano na viongozi wa mamlaka ya nchi hiyo wanashambuliwa mara kwa mara; na migogoro ya kijamii, kikabila na kidini inazidi kuwa mikubwa.

Pili, hali ya usalama ya Iraq inayovurugika siku hadi siku inatoa shinikizo kubwa la kisiasa kwa serikali ya nchi zilizopeleka jeshi nchini humo. Kwa mfano, hivi karibuni, jasusi mmoja aliuawa na jeshi la Marekani nchini humo alipokuwa akimpeleka uwanja wa ndege mwaandishi wa habari wa Italia aliyeokolewa. Tukio hilo limeathiri sana uhusiano kati ya Italia na Marekani, na karibu asilimia 70 ya wananchi wa Italia walipinga zaidi serikali yao kuiunga mkono Marekani kuanzisha vita vya Iraq. Serikali za nchi nyingine zilizopeleka jeshi nchini Iraq pia zinakabiliana na shinikizo kubwa kutoka nchini.

Tatu, suala la kuondoa jeshi nchini Iraq linahusiana na masuala mengi mengine. Mwelekeo wa hivi sasa wa kuondoa jeshi nchini humo si kama tu unaathiri mpango wa jeshi la Marekani, Uingereza na Australia nchini humo, bali pia unatoa shinikizo kubwa kwa nchi kama Poland. Baada ya baadhi ya nchi kuondoa majeshi yao, jeshi linalobaki litakabidhiwa majukumu ya ulinzi ya majeshi hayo. Kwa mfano, askari 300 wa Hungary wanaoshughulikia uchukuzi na mawasiliano na ugavi wa vitu wa jeshi la muungano kwenye sehemu ya kati na kusini ya nchi hiyo watarudishwa nyumbani mwezi huu, hali hiyo itasababisha moja kwa moja jeshi la Poland kwenye sehemu hiyo kupangwa upya. Lakini serikali ya Poland imetangaza kuwa kutokana na kuwa haiwezi kutekeleza majukumu ya ulinzi peke yake, jeshi la Poland pia litaondoka Iraq. Waziri wa ulinzi wa Poland Bw. Jerzy Szmajdzinski alisema kuwa, jeshi la Poland litaongeza nguvu katika kutoa mafunzo kwa jeshi la Iraq ili kuliwezesha limudu kazi ya kulinda usalama.

Wachambuzi wanaona kuwa, nchi washirika wa Marekani na Uingerza kuondoa majeshi yao kutoka nchini Iraq kuna umuhimu mkubwa zadi wa kisiasa kuliko wa kijeshi. Katika siku za baadaye, Jeshi la muungano litategemea kwa kiasi kikubwa jeshi la ulinzi la Iraq kutekeleza majukumu ya kulinda usalama wa nchi hiyo. Lakini pia wanaona kuwa, bado ni mapema kwa jeshi la lraq kutekeleza jukumu la ulinzi, hivyo Marekani na Uingereza lazima ziongeze majeshi yao nchini humo. Hali hiyo si kama tu itaziletea lawama zaidi serikali ya Bush na serikali ya Blair kuhusu suala la Iraq, bali pia itayafanya majeshi ya nchi hizo mbili yatengwe zaidi.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-17