Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-18 16:13:42    
Picha za kuchora za Li Qi

cri

Li Qi ni profesa wa Chuo Kikuu cha Uchoraji , aidha ni mchoraji maarufu wa sura za watu. Picha nyingi zaidi alizochora zinahusu watu mashuhuri wa zama zetu na vilevile nyingine zinahusu wafanyakazi, wakulima, askari na wasomi. Yeye anachora sura hizo za watu juu ya karatasi za Xuan (aina ya karatasi bora zilizotengenezwa Xuancheng jimboni Anhui) kwa kutumia nguvu ya brashi na kuonyesha tena mioyo ya binadamu, ili kuchechemua akili na tabia za watazamaji. Mwaka nwa 1960 Li Qi alichora picha ya "Mwenyekiti Mao Akitembelea Kila Sehemu ya China". Katika picha hiyo ya kuchora Mwenyekiti Mao anaonekana akiwa amevaa mavazi ya kawaida, kofia ya ukoka mkononi na akikagua ardhi ya China kwa uchangamfu. Ingawa mchoraji hakuchora mandhari yoyote nyuma ya Mwenyekiti Mao, lakini watazamaji wanaweza kupata picha ya mara moja ya Mwenyekiti Mao akiwa amekwishafika miongoni mwa umma. Picha hiyo ya kuchora inapendwa na umma na hutundikwa ndani ya kumbi.

Li Qi ni hodari wa kuchora picha za kuwaburudisha watazamaji kwa kutumia njia rahisi za kisanaa. Kifaa anachotumia wakati wa kuchora ni brashi na nyenzo ni rangi na karatasi za Xuan. Kila anapopitisha brashi yake mara moja huwa habahatishi. Sanaa yake yenye mtindo wa kipekee na wa ajabu husifiwa na watazamaji na wachoraji wa China na wa ng'ambo.

Licha ya hayo Li Qi ana uwezo mmoja wa kuchora sura za binadamu kutokana na kumbukumbu. Pengine baadhi ya marafiki zake hupewa picha za sura zao bila ya kutarajia ambazo zinafanana na sura zao halisi, lakini wao wenyewe hawakujua lini na wapi waliangaliwa na mchoraji huyo.

Mwaka wa 1937 Li Qi alipokuwa na umri wa miaka tisa, alifika kwenye kituo cha kimapinduzi cha Yanan kutoka mahali alipozaliwa, Wilaya ya Pingyao jimboni Shanxi akiongozana na wazazi wake. Huko Yanan alipata mafunzo ya kumapinduzi na hatua kwa hatua akawa na wazo la kupigania juhudi ya maendeleo ya binadamu. Katika maisha yake marefu ya kisanaa siku zote huwa na upeo mpana kwamba sanaa itumikie wananchi. Hivi leo amekuwa na umri wa zaidi ya miaka 80, lakini angali bado anachora na kufanya jitihada katika kazi bila ya kusimama.

      


1  2