Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-18 18:12:08    
Kampuni ya COSCO yaanzisha daraja salama wa mawasiliano baharini Kati ya China na Afrika

cri

Karibuni katika kipindi cha Daraja la Urafiki kati ya China na Afrika. Wapendwa wasikilizaji, katikati ya mwezi uliopita, meli ya mizigo ya Ruaha inayomilikiwa na Kampuni ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ya Uchukuzi wa Baharini ilifika kwenye bandari ya Dar es Salaam, mji mkuu wa Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka huu. Ili kusherehekea meli hiyo kuwasili salama nchini Tanzania kwa usalama baada ya kukumbwa na dhoruba kubwa, kampuni hiyo iliwaalika watu wa fani mbalimbali wa Tanzania kuitembelea meli hiyo kubwa kwa mara ya kwanza. Katika kipindi hiki cha leo, tunawaletea maelezo kuhusu Kampuni ya COSCO kuanzisha daraja salama la mawasiliano ya baharini lati ya China na Afrika.

Meli ya mizigo ya Ruaha ilipewa jina lake kutokana na mto maarufu nchini Tanzania Mto Ruaha. Meli hiyo iliondoka kutoka Shanghai, mji maarufu wa mashariki wa China, na ilipita kwa usalama dhoruba kubwa lililosababishwa na tetemeko la ardhi la Indonesia. Hii ni safari ndefu ya 120 kwa meli hiyo tangu ilipoanza kufanya kazi mwaka 1980. Wageni walioalikwa walitembelea sehemu mbalimbali za meli hiyo, na kuisifu sana.

Kampuni ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ya Uchukuzi wa Baharini ilianzishwa tarehe 22 mwezi Mei, mwaka 1967 huko Dar es Salaam, mji mkuu wa Tanzania, kutokana na mapendekezo ya pamoja ya hayati mwalimu Julius Nyerere aliyekuwa rais wa Tanzania na hayati Zhou Enlai aliyekuwa waziri mkuu wa China. Ukiwa ni ushirikiano kati ya serikali ya nchi hizo mbili, meli tatu kubwa za kampuni hiyo zimetoa mchango mkubwa kwa kazi ya uchukuzi wa safari ndefu baharini. Meli hizo za Kampuni ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ya uchukuzi Baharini zimehakikisha usalama wa uchukuzi wa mizigo kati ya mabara ya Asia na Afrika kwa kupita sehemu ya Mashariki ya Kati.

Likiwa shirika kuu la Kampuni ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ya uchukuzi Baharini, Shirika la uchukuzi Baharini wa Safari Ndefu la China COSCO lilianzishwa tarehe 16 mwezi Februari mwaka 1993, zamani lilikuwa Kampuni ya Uchukuzi Baharini wa Safari Ndefu ya China ambayo ilianzishwa mwaka 1961. Wakati huo, kampuni hiyo ilikuwa na meli nne tu, lakini baada ya juhudi za miaka 40, sasa shirika hilo limepata maendeleo makubwa, na limekuwa shirika la kimataifa lenye meli zaidi ya 600 za kisasa, ambapo linasafirisha mizigo yenye uzito wa tani milioni 260 kila mwaka. Likiwa ni shirika la kimataifa, sasa COSCO ina matawi karibu elfu moja, na wafanyakazi zaidi ya elfu 80. Nchini China, matawi ya shirika hilo yameenea katika sehemu mbalimbali zikiwemo Guangzhou, Shanghai, Tianjin, Qingdao, Dalian na Hongkong, na yanajishughulisha na kazi za uchukuzi wa bidhaa mbalimbali; wakati huo huo, mtandao wa kimataifa wa shughuli za shirika hilo umeanzishwa katika nchi mbalimbali zikiwemo Japan, Korea ya Kusini, Singapore, Amerika ya Kaskazini, Ulaya, Australia, Afrika Kusini na Asia ya Magharibi, ambapo meli zenye nembo ya COSCO zinafika kwenye bandari zaidi ya 1300 katika nchi zaidi ya 160 duniani.

Kampuni ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ya Uchukuzi Baharini ni kampuni pekee yenye meli zinazoweza kusafirisha migizo kwa safari ndefu katika sehemu ya Afrika Mashariki. Kampuni hiyo imegharimiwa fedha takriban pound za Kiingereza milioni 5, na sasa ina meli 3 za ngazi ya tani elfu 15, na imeanzisha ofisi yake hapa Beijing, mji mkuu wa China, na ina tawi huko Mombasa, Kenya. Kampuni ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ya Uchukuzi Baharini inashughulikia uchukuzi wa mizigo na kazi nyingine. Njia ya meli zake inaanzia kutoka China, kupita nchi za Asia ya Kusini Mashariki, India na kufika katika Afrika Mashariki, nchi za Bahari ya Mediteranan na Ghuba ya Uajemi, na kusafirisha bidhaa na mizigo kati ya sehemu hizo.

Meneja wa upande wa China wa Kampuni hiyo Bw. Li Keliang alieleza kuwa, urafiki kati ya China na Tanzania ulianzishwa katika miaka mingi iliyopita, na pande hizo mbili zitaendelea kushikilia kanuni ya ushirikiano wa kirafiki na kunufaisha pande zote, na kuzidi kuimarisha usimamizi na kupanua eneo la shughuli zake, ili kuifanya iwe kama daraja la uchumi na biashara kati ya Asia na Afrika ya Mashariki.

Mwenyekiti wa Kampuni ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ya uchukuzi Baharini, ambaye pia ni katibu wa kudumu wa Wizara ya mawasiliano na uchukuzi ya Tanzania Bw. Musoma alisema kuwa, meli ya Ruaha iliandikishwa kwenye bandari ya Dar es Salaam, hivyo kila mara meli hiyo inaporudi, Watanzania wanaona fahari kubwa, kwa sababu hii ni meli kubwa pekee yenye bendera ya taifa ya Tanzani. Bw. Musoma alieleza kuwa, Kampuni ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ya uchukuzi Baharini imeonesha urafiki mkubwa kati ya watu wa Tanzania na China.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-18