Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-18 21:14:49    
Mazungumzo kati ya makundi mbalimbali ya Palestina yapata maendeleo mazuri

cri

Mazungumzo mapya kati ya makundi mbalimbali ya Palestina yalimalizika tarehe 17 huko Cairo. Mkutano huo ulitoa taarifa ukiahidi kuhakikisha hali ya utulivu kati ya Palestina na Israel tangu mwezi Februari mwaka huu. Wachambuzi wanaona kuwa, ahadi hiyo imeonasha kuwa Palestina imetangaza kusimamisha mapambano dhidi ya Israel kwa sharti la Israel kutobadilisha hali ya kusimamisha mapambano. Aidha, mkutano huo pia ulipata maoni ya pamoja kuhusu masuala kadhaa muhimu ya upangaji wa mambo ya kisiasa ya Palestina. Hivyo maendeleo yaliyopatikana katika mazungumzo hayo ni ya maana sana.

Wakuu na wawakilishi wa makundi 13 ya Palestina waliohudhuria mkutano huo waliahidi kwenye taarifa kuwa, katika hali ya Israel kusimamisha shughuli zote dhidi ya Wapalestina na kuwaachia huru Wapalestina waliofungwa, makundi mbalimbali ya Palestina yanakubali kuhakikisha hali ya utulivu kati ya Palestina na Israel na kutoweka muda wa mwisho wa hali hiyo. Taarifa ilisisitiza kuwa, Watu wa Palestina wana haki ya kupambana ili kumaliza ukaliaji wa Israel.

Lakini baada ya mkutano huo, mwakilishi wa kundi la Hamas Bw. Mohammed Nazal alisema kuwa, pande mbalimbali zilizohudhuria mkutano huo zilikubali kuhakikisha muda usiozidi mwaka mmoja wa hali ya utulivu, muda huo utakapoisha, kama Israel haitachukua hatua katika kusimamisha shughuli uadui, kuwaachia huru Wapalestina waliofungwa na kuondoa jeshi lake, kundi la Hamas halitatekeleza ahadi ya kuhakikisha hali ya utulivu. Katibu mkuu wa kundi la Jihad alisema kuwa, Palestina na Israel kuweza au kutoweza kuhakikisha hali ya utulivu kunaamuliwa na Israel. Na mwakilishi wa kundi la Popular Front for the Liberation of Palestine alisema kuwa, kwa sababu katibu mkuu wa kundi hilo Bw. Ahmed Saadat aliyeshitakiwa kupanga kumwua waziri wa zamani wa utalii wa Israel Bw. Rehavam Zeevi bado amefungwa huko Jericho, hivyo kundi hilo linabaki na maoni yake huhusu ahadi hiyo.

Katika suala la upangaji wa kisiasa wa mambo ya ndani ya Palestina, kwa mujibu wa taarifa ya mwisho, wawakilishi wa makundi mbalimbali wamekubali kuboresha mageuzi ya ndani na kuunga mkono mchakato wa kidemokrasia.

Uchaguzi wa kamati ya utungaji wa sheria ya Palestina na suala linalofuatiliwa na makundi mbalimbali. Kundi la Fatah limekubali kufanya marekebisho makubwa kuhusu mfumo wa sasa wa uchaguzi ili kuhakikisha makundi mbalimbali yapate fursa ya kushiriki kwenye kamati mpya ya utungaji wa sheria. Baada ya majadiliano, makundi hayo yalikubali kufanya uchaguzi kwa wakati mwezi Julai mwaka huu, na kutunga mpango wa marekebisho ya sheria husika ya uchaguzi wa kamati hiyo.

Katika suala la kupanga tena chama cha ukombozi wa Palestina, pande mbalimbali zilizohudhuria mkutano huo zinaona kuwa, hivi sasa chama hicho kinachukuliwa kama ni mwakilishi halali wa Wapalestina duniani, lazima makundi yote yakiwemo kundi la Hamas na kundi la Jihadi yaruhusiwe kushiriki kwenye chama hicho. Mkutano huo umeamua kuanzisha tume maalum inatakayoundwa na wakuu wa makundi mbalimbali, mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji wa chama cha ukombozi wa Palestina na watu huru kujadili suala la kupanua chama hicho ili kuimarisha umoja wa makundi mbalimbali ya Palestina.

Kuhusu makundi mbalimbali ya Palestina kupata maoni ya pamoja, waziri mkuu wa Israel Bw. Ariel Sharon alipompigia simu Rais Hosni Mubarak alisema kuwa, hii ni hatua ya kwanza ya Palestina inayosaidia. Lakini alisistiza kuwa, mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel ukitaka kupata maendeleo makubwa, Palestina lazima ivunje "makundi ya kigaidi" yakiwemo kundi la Hamas na kundi la Jihad na kuyanyang'anya silaha.

Wachambuzi wanaona kuwa, maendeleo yaliyopatikana katika mazungumzo hayo ni mafanikio ya kisiasa yenye athari kubwa kwa mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina ambaye ameshika cheo hicho kwa miezi miwili tu. Na maendeleo hayo yatasaidia kuimarisha umoja wa makundi mbalimbali ya Palestina, kupata uungaji mkono mkubwa zaidi wa jumuiya ya kimataifa na kurejesha mchakato wa amani kati ya Palestina na Israel.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-18