Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-21 16:21:38    
Waimbaji mahiri wachangia kampeni ya kulinda hakimiliki

cri

Katika miaka ya 80 ya karne iliyopita, China ilifanya maonesho kama hayo mara mbili. Katika karne hii serikali ya China ilifanya kampeni ya kupinga wizi wa hakimiliki kwa miaka miwili mfululizo. Ili kuonesha nia thabiti ya serikali na kuhamasisha umma uamke na kushiriki kwenye mapambano ya kulinda hakimili idara husika za serikali ziliandaa maonesho hayo kwa mara nyingine tena. Naibu mkuu wa Idara ya Hifadhi ya Hakimiliki Bw. Yan Xiaohong alieleza, "Lengo la maonesho hayo sio ya kuonesha michezo tu lakini maana yake kubwa zaidi ni kuchangia kampeni ya kulinda hakimiliki kwa kuwashirikisha waimbaji wengi mahiri ili kuhamasisha watu wengi zaidi katika jamii."

Imefahamika kuwa vituo 25 vya redio na televisheni nchini China vilitangaza maonesho hayo kwa wakati mmoja, na kutazamwa na kusikilizwa na watu milioni 500.

Pamoja na maonesho hayo Idara ya Hifadhi ya Hakimiliki ilifanya shughuli nyingine ya kuharibu diski na vitabu elfu kumi kadhaa hadharani vilivyochapishwa kinyume cha sheria, baadhi ya wasanii walishindilia mashapisho ndani ya mashine ya kuharibu vitu hivyo. Mkuu wa Idara ya Hifadhi ya Hakimiliki Bi. Sun Xiangdong kwenye shughuli hiyo alisema, "Katika miaka ya karibuni, shughuli ya kuharibu diski na vitabu vinavyokiuka hakimiliki imekukwa ikifanyika kila mwaka, lakini hii ni mara ya kwanza shughuli hiyo kufanywa na wasanii wenyewe."

Pamoja na maonesho hayo, katika siku hiyo pia kulikuwa na mkutano mjini Beijing ulioandaliwa na Shirikisho la Mashirika ya Gramafoni la China kuhusu hifadhi ya hakimiliki. Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe kutoka Shirikisho la Audio na Video, Shirikisho la Wachapishaji, Shirikisho la Hakimiliki na Shirikisho la Mashirika ya Gramafoni, na kwenye mkutano walitoa "Taarifa ya Beijing ya Kupinga Ukiukaji wa Hakimiliki". Msemaji wa harakati za kupinga ukiukaji wa hakimiliki Bw. Feng Xiaogang ambaye ni mwongozaji mashuhuri wa filamu, kwenye mkutanno alisema, "Katika miaka mingi iliyopita filamu nyingi nilizotengeneza zilirudufiwa, kwa hiyo mimi ni mmoja wa walionyimwa hakimiliki na kudhurika, natumai kuwa watu wote wataitikia wito wetu na watajitokeza kushiriki kwenye kampeni yetu."

Kwenye mkutano huo Feng Xiaogang alisoma "Taarifa" hiyo.

Tokea China ianze kutekeleza sheria ya hakimiliki mwaka 1991, China kwa mara nyingi ilihimiza utekelezaji wa sheria hiyo, na kueneza elimu kuhusu sheria hiyo ili kuinua mwamko wa umma wa kulinda hakimiliki. Mada ya maonesho hayo ni "Tulinde Hakimiliki", na ilisifiwa na kuungwa mkono na watu wengi. Bi. Guo Chunfei kutoka Shirikisho la Mashirika ya Gramafoni alisema, "Serikali yetu imetumia kila njia kueneza mwamko wa kulinda hakimiliki. Maonesho hayo yamewashirikisha wasanii wa sehemu mbalimbali nchini China wakiwemo wasani kutoka Hong Kong na Macau. Hii inadhihirisha kuwa serikali ya China inatilia maanani suala la kulinda hakimiliki."

Mwongozaji mashuhuri wa filamu Bw. Xia Gang alisema, kutatua kabisa tatizo la ukiukaji wa hakimiliki kunahitaji juhudi za pamoja na za muda mrefu, lakini safari bado ni ndefu."

Imefahamika kuwa, mwaka huu Idara ya Hifadhi ya Hakimiliki itafanya harakati za kulinda hakimiliki miongoni mwa wanafunzi wa sekondari milioni 300 nchini China, ili kuleta mazingira mazuri ya hakimiliki.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-21