Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-21 17:00:18    
Je, nchi za kiarabu zitachukua hatua kwa pamoja?

cri
    Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu, ambao ulifanyika kwa siku mbili, umefungwa jana huko Algiers, Algeria. Pande mbalimbali zilizoshiriki kwenye mkutano zilikuwa na majadiliano kuhusu ratiba ya mkutano wa wakuu wa nchi za kiarabu utakaofanyika tarehe 22 mjini Algiers na kuafikiana kwenye mpango kuhusu suala la uhusiano wa nchi za kiarabu. Wachambuzi wanaona kuwa bado kuna tofauti kubwa katika misimamo ya nchi za kiarabu kuhusu baadhi ya masuala nyeti.

    Kabla ya kufanyika kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu, Jordan iliwasilisha mswada wa azimio kwenye mkutano huo, ukisisitiza kuwa nchi za kiarabu zinachagua kutimiza amani, usalama na utulivu kuwa ni lengo lao kubwa na kutangaza kuwa nchi za kiarabu zinakubali kumaliza mapambano kati yake na Israeli, kuanzisha uhusiano mwafaka kati ya pande hizo mbili, lakini masharti yake ni kanuni za kubadilisha ardhi kwa amani na utimizaji wa amani ya haki na kudumu chini ya mpango uliothibitishwa kwenye mazungumzo ya amani ya Madrid. Ikilinganishwa na pendekezo la amani la nchi za kiarabu lililopitishwa kwenye mkutano wa wakuu wa nchi mwaka 2002 huko Beirut, mswada huo wa azimio umeweka mbele sana nia ya nchi za kiarabu ya kuanzisha uhusiano mwafaka na Israel.

    Ingawa Jordan imesisitiza mara nyingi kuwa lengo la kutoa mswada huo wa azimio ni kuhimiza utekelezaji wa pendekezo la amani la nchi za kiarabu lililokwama kwa zaidi ya miaka mitatu, ambao haukufanya marekebisho halisi juu ya pendekezo hilo, lakini mswada huo bado unapingwa na watu wenye msimamo wa siasa kali ikiwemo Palestina, na kulaumiwa kuwa ni kufanya "usuluhishi kwa bei rahisi na Israeli".

    Ili kutuliza mgogoro huo, pande mbalimbali zilizoshiriki kwenye mkutano ziliafikiana kwenye mpango, ambao unakubali kufanya marekebisho juu ya pendekezo la amani la nchi za kiarabu na kulipitisha kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za kiarabu. Habari zinasema kuwa katika mpango huo nchi za kiarabu zinasisitiza kuwa nchi za kiarabu zinakubali kuleta amani kati yao na Israeli, lakini masharti ni kuwa jeshi la Israel lazima lirudi nyuma hadi kwenye mpaka wa mwaka 1967kabla ya vita vya tatu vya mashariki ya kati, na kutatua suala la wakimbizi wa palestina kwa kufuata maazimio husika ya baraza la usalama na kuanzisha nchi ya Palestina, ambayo mji mkuu wake utakuwa Jerusalem. Kutokana na malalamiko ya Jordan juu ya matokeo hayo, mwakilishi wa Jordan kwenye mkutano huo ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Hani al-Mulki tarehe 20 alisema kuwa mfalme wa Jordan hatashiriki kwenye mkutano wa wakuu wa nchi utakaofanyika tarehe 22.

    Habari nyingine zinasema kuwa kutokana na malalamiko ya Syria na Lebanon juu ya msimamo wa nchi za kiarabu katika suala la mgogoro wa Lebanon, nchi hizo mbili zinashikilia kuwa mgogoro wa Lebanon ni "suala la pande mbili", zinakataa kuwasilisha mswada wa azimio husika kwenye mkutano wa wakuu wa nchi, hivyo mkutano huo wa wakuu wa nchi hautaweka suala la mgogoro wa Lebanon katika ratiba rasmi ya mkutano, rais Lahud wa Lebanon ametangaza kuwa hatashiriki kwenye mkutano wa wakuu wa nchi kutokana na kuwa na shughuli nyingi kuhusu mgogoro wa nchini, ambapo kushiriki kwenye mkutano kwa rais Bashar Al Assad wa Syria bado hakufahamiki kwa hivi sasa.

    Wachambuzi wanasema kuwa ili kukabiliana na hali ya kimataifa yenye mabadiliko mengi, kuchukua hatua za pamoja kumekuwa mkondo kwenye mikutano ya nchi za kiarabu, lakini katika mikutano ya nchi za kiarabu iliyofanyika katika miaka ya karibuni, nchi zenye msimamo wa upole zimekuwa na sauti kubwa, hivyo na namna ya mkutano huo wa wakuu wa nchi kusawazisha misimamo tofauti na kuchukua hatua halisi za pamoja, limekuwa jambo linalohusiana na umuhimu na maendeleo ya umoja wa nchi za kiarabu.

Idhaa ya Kiswahili