Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-21 20:01:18    
Nchi zinazoendelea zatoa maoni kuhusu haki na za binadamu na mkutano wa haki za binadamu

cri

Wiki moja imepita tangu mkutano wa 61 wa Kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ufunguliwe, wajumbe wa nchi zinazoendelea wametoa maoni kuhusu haki za binadamu na hali yake ilivyo ya sasa, na baadhi yao wametoa mapendekezo kuhusu mageuzi ya kamati ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Kuhusu haki za binadamu, ofisa mwandamizi mpya wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya haki za binadamu Bwana Louise Arbour alidhihirisha kwenye ufunguzi wa mkutano kuwa, haki ya maendeleo, haki za uchumi, jamii na utamaduni pamoja na haki ya raia na haki ya siasa, zote hizo haziwezi kutenganishwa, binadamu akiwa na heshima ya kimsingi ndipo atakapoweza kuzungumzia utimizaji wa haki mbalimbali za binadamu. Waziri wa mambo ya nje wa Indonesia Bw Asan Wirayuda ameeleza kuwa, kuhusu haki mbalimbali za binadamu, haipaswi kusisitiza zaidi haki fulani na kupuuza haki nyingine, ambapo haki za uchumi, jamii na utamaduni zinapaswa kuheshimiwa vilevile kama ilivyo haki ya raia ya siasa. Waziri wa sheria wa Kenya Kiraitu Murungi alisisitiza kuwa, haki za binadamu hazitaonekana muhimu kama hazitajadiliwa pamoja na masuala kuhusu hali isiyo na usalama, ukosefu wa ajira, njaa, umaskini na maradhi.

"Kundi lenye maoni yanayofanana" linaloundwa na nchi 20 zinazoendelea ni jumuiya muhimu inayojishirikisha katika shughuli za sekta ya haki za binadamu duniani katika miaka ya hivi karibuni. Mwaka huu China imechaguliwa tena kuwa mratibu wa jumuiya hiyo. Mwakilishi wa kudumu wa China katika mashirika ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Bwana Sha Zukang kwa niaba ya jumuiya hiyo alidhihirisha kwenye mkutano huo kuwa, wakati wa kutimiza haki za uchumi, jamii na utamaduni na haki ya maendeleo, hukukuwa na pengo kubwa kati ya hali halisi na matumaini. Haki hizo bado hazijatambuliwa kuwa haki za kimsingi za binadamu kote duniani. Nchi nyingi, hasa nchi zinazoendelea zinapotimiza haki hizo hukutana na vikwazo na taabu nyingi.

Waziri wa mambo ya nje wa Malaysia Bw Jaafar Albar alisisitiza kuwa, hali ya kuwa nyuma kiuchumi na kuwekwa ukingoni husababisha moja kwa moja kukiukwa kwa haki za kimsingi za binadamu na heshima za watu; ofisa mwandamizi wa Mauritania Bwana Hamadi Ould Meimou aliainisha kuwa, kujenga hali inayosaidia maendeleo ya uchumi na jamii kunasaidia kuondoa sababu mbalimbali zinazotishia amani, kutokomeza umaskini na kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja wa Mataifa ni silaha zenye ufanisi mkubwa kabisa za kulinda utulivu na kupambana na ugaidi; waziri wa mambo ya nje wa Nigeria Alhaji Abubakar Tanko alisema kuwa, kwa nchi nyingi zinazoendelea, kazi ya dharura ni kupata njia halisi za kutatua masuala yaliyokuwepo kwa muda mrefu kuhusu umaskini, madeni makubwa, pengo kubwa kati ya maskini na matajiri na hali isiyo ya utulivu.

Kuhusu mkutano wa haki za binadamu wa hivi sasa, nchi nyingi zinazoendelea zinaona kuwa, mkutano huo umekuwa chombo cha kufanya mapigano ya kisiasa siku hadi siku katika miaka ya hivi karibuni. Nchi kadhaa za magharibi zinapuuza masuala ya haki za binadamu ya nchi zao, zikitumia ovyo maazimio ya mkutano huo, kuzikosoa nchi nyingi zinazoendelea na kuharibu vibaya heshima ya mkutano wa haki za binadamu. Hivi sasa mwelekeo wa kisiasa unaonekana dhahiri kwenye mkutano wa haki za binadamu, na mapambano kwenye mkutano huo yamezidi kuwa makali, hayo yamekiuka nia na malengo ya mkutano huo. Wajumbe wa nchi zinazoendelea wanazitaka nchi wanachama wa mkutano huo zifanye ushirikiano na mazungumzo zaidi badala ya malalamiko na mapambano, na kufanya juhudi za pamoja ili kufufua umuhimu na heshima ya mkutano wa haki za binadamu.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-21