Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-22 14:17:45    
Wasiwasi wazuka tena kati ya Jordan na Iraq

cri

Msemaji wa serikali ya Jordan Bi. Asma Khodr tarehe 21 huko Amman, mji mkuu wa Jordan, alisema kuwa serikali ya Jordan imerudisha balozi wake mdogo kutoka Iraq. Hata hivyo, Bi. Khodr alisema Jordan inatumai kutuliza wasiwasi huo mapema iwezekanavyo. Alisisitiza, serikali ya Jordan inaona kuwa kuendelea na kuimarisha uhusiano mzuri kati ya nchi mbili ni muhimu sana na Jordan haitaki kuona wasiwasi huo unazidi kuwa mbaya.

Wasiwasi huo kati ya nchi mbili ulisababishwa na mlipuko uliotokea tarehe 28 Februari kusini ya Baghdad kwa maili 60. Mlipuko huo ulisababisha vifo vya watu 125. Hili ni tukio la kuua watu wengi kabisa tokea vita vya Iraq vianze katika mlipuko mmoja, na waliouawa karibu wote ni askari wa polisi wa Iraq na vijana waliokuwa wanajiandikisha na jeshi karibuni kutoka waumini wa madhehebu ya Shia.

Baada ya mlipuko huo kutokea, vyombo vya habari vya Jordan vilisema kuwa raia mmoja wa Jordan alipanga mlipuko huo. Habari hiyo iliwakasirisha sana waislamu wa madhehebu ya Shia, Chama cha Umoja wa Iraq kilichoshinda katika uchaguzi uliofanyika Januari mwaka jana kilishutumu kwamba Jordan iliruhusu magaidi waingie nchini Iraq. Serikali ya Iraq pia ilionesha ililaani. Katika wiki iliyopita waislamu wa madhehebu ya Shia kwa mara nyingi walifanya maandamano na kuishambulia ofisi ya ubalozi ya Jordan nchini Iraq. Waandamanaji walichoma moto bendera ya taifa ya Jordan na hata walipandisha bendera ya taifa ya Iraq ubalozini.

Lakini Jordan ilikana kabisa shutuma za Iraq. Waziri wa mambo ya nje wa Jordan aliyekuwa Algiers kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za Umoja wa Kiarabu Hani al-Mulki tarehe 20 alisema kuwa kutokana na wasiwasi uliotokea sasa, Jordan imeamua kumwondoa mwanadiplomasia wake mwandamizi nchini Iraq. Baada ya Jordan kutangaza habari hiyo, Iraq mara ikajibu, kwamba waziri wa mambo ya nje wa serikali ya muda ya Iraq Hoshyar Zebari alisema, anasikitishwa na wasiwasi uliotokea kati ya Iraq na Jordan, serikali ya Iraq imeamua kuondoa balozi wake mjini Amman ili kujadili hali ya wasiwasi huo.

Wasiwasi uliotokea sasa sio mara ya kwanza. Baada ya vita dhidi ya Iraq kutokea, uhusiano kati ya nchi mbili umewahi kuwa na wasiwasi mara kadhaa. Jordan ni moja ya nchi rafiki za Marekani kati ya nchi za Kiarabu, ingawa Jordan haikubali Marekani kuanzisha vita dhidi ya Iraq lakini inaruhusu askari 6000 wa Marekani kukaa nchini, jambo hilo liliwachukiza watu wa Iraq wanaounga mkono Saddam Hussein. Baada ya mamlaka ya Saddam Hussein kupinduliwa, Jordan aliwapokea mabinti wawili wa Saddam, jambo hilo lilihamakisha waislamu wa madhehebu ya Shia waliokandamizwa kwa muda mrefu wa Saddam. Mwezi Agosti mwaka 2003 ofisi ya ubalozi ya Jordan iliyoko nje kidogo ya Baghdad ilishambuliwa kwa bomu lililotegwa ndani ya gari na kusababisha vifo vya watu 18 na 40 kujeruhiwa. Baada ya mlipuko, watu wa Iraq waliokasirika walikimbilia ndani ya ubalozi wakateremsha bendera ya Jordan na kufanya fujo mpaka askari wa Marekani kufika huko.

Uhusiano wa kiuchumi na kisiasa kati ya nchi mbili ni mkubwa, serikali za nchi mbili hazitaki kuona mlipuko huo unaathiri maslahai ya nchi mbili. Kwa upande wa Iraq, kutokana na kuwa serikali mpya haijaanzishwa, hali ya nchini bado ni vurugu, serikali ya Iraq inataka mazingira ya utulivu ili kujijenga upya katika siasa na uchumi. Kwa upande wa Jordan pia haitaki kuona hali ya wasiwasi inatokea. Msemaji wa serikali ya Jordan Bi. Khord alisisitiza kuwa kumwondoa balozi wake mdogo kunamaanisha uhusiano wa kisiasa kati ya nchini mbili umekatika, serikali ya Jordan inatumai kuwa uhusiano huo utarejea mapema iwezekanavyo. Watu wamegundua kuwamba pande mbili zilipotangaza kurudisha mabalozi, zote zilitumia neno "ili kujadili" hali ilivyo ya sasa. Hii inamaanisha kuwa pande hizo zimejiwekea nafasi ya kuweza kutuliza wasiwasi huo, hazitaki kuona unazidi kuwa mbaya.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-22