|
Ni hali ya kawaida kwa Ulaya kushangazwa na uteuzi huo, kwani Bw. Paul Wolfowitz ni ofisa mashuhuri mwenye msimamo wa siasa kali na anachukuliwa kuwa ni mmoja wa wawakilishi wa watu wa wahafidhina wapya nchini Marekani, ambaye alichangia kuanzishwa kwa vita nchini Iraq na ni mmoja wa "wasanifu" wa vita vya Iraq na kuchukiwa na watu wa baadhi ya nchi za Ulaya. Si hayo tu, baada ya shughuli muhimu za kijeshi za vita vya Iraq kuisha, Wolfowitz alisaini amri ya kubagua kampuni za nchi zilizopinga vita vya Iraq katika ujenzi mpya wa Iraq. Kitendo chake hicho kilikosolewa vikali na nchi za Ulaya zilizopiga vita vya Iraq.
Hadi hivi sasa kwa jumla Umoja wa Ulaya na nchi za Ulaya zilikuwa na uangalifu mkubwa juu ya hatua hiyo, isipokuwa Uingereza na baadhi ya nchi chache nyingine ambazo zilieleza kufurahia uteuzi huo. Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bw. Jose Manuel Barroso tarehe 21 kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema kuwa haifai kuwa na kinyongo na Wolfowitz, bali tungesikiliza kwanza mipango na malengo yake, halafu tupime uwezo wake wa kutekeleza malengo hayo. Baada ya rais Bush kutangaza uteuzi huo, mjumbe wa kamati ya Umoja wa Ulaya anayeshughulikia utoaji msaada wa kibinadamu Bw. Louis Michel tarehe 18 alitangaza kuwa amemwalika Bw Wolfwitz kuwa na mazungumzo naye huko Brussels ili kusikiliza maoni yake kuhusu changamoto inayokabili Benki ya Dunia na Benki ya Dunia ya kufanya kazi muhimu. Hatua hiyo ya Ulaya kabisa ni kutaka kumpima uwezo wa Wolfowitz uso kwa uso. Habari zinasema kuwa Bw. Wolfowitz amekubali mwaliko wa Umoja wa Ulaya isipokuwa tarehe kamili ya ziara yake katika Umoja wa Ulaya bado haijathibitishwa.
Aidha, baadhi ya wabunge la bunge la Ulaya wameanzisha kampeni ya kumpinga Bw. Wolfowitz kushika wadhifa wa mkurugenzi mkuu wa Benki ya Dunia, wabunge waliotoka vyama mbalimbali wamesaini barua moja inayotoa wito wa kuwaka nchi wanachama zisiunge mkono pendekezo la kumteua Wolfowitz, wakimtaja kuwa ni "kaimu wa chansela wa Marekani", na kusema yeye siyo mtu anayefaa kuchukua nafasi ya mkurugenzi mkuu wa Benki ya Dunia. Zaidi ya hayo, wanaona kuwa Umoja wa Ulaya una haki nyingi kuhusu uteuzi katika Benki ya Dunia kuliko Marekani, hivyo Umoja wa Ulaya ungetumia ipasavyo haki zake.
Kwa jumla, ingawa Ulaya ina maoni tofauti kuhusu pendekezo la kumteua Wolfowitz, lakini hakuna uwezekano mkubwa kwa Umoja wa Ulaya kumkataa waziwazi. Kwani kwa kufuata desturi, Marekani inawajibika kumteua Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Dunia, ambapo Umoja wa Ulaya unawajibika kumteua mkurugenzi mkuu wa Shirika la Fedha Duniani. Kwa jumla pande hizo mbili hazijafikia hatua ya kubomoleana msingi wa pande mwingine. Hata hivyo, kuna wakati wa kutokea mambo yasiyotarajiwa, mwaka 2000 Umoja wa Ulaya ulipotoa pendekezo la kumteua naibu waziri wa fedha wa Ujerumani Caio Koch-Weser kushika wadhifa wa mkurugenzi mkuu wa Shirika la Fedha Duniani, ulikataliwa na Marekani. Mbali na hayo, hivi sasa pande mbili za Marekani na Ulaya zinajitahidi kuimarisha uhusiano wao, Umoja wa Ulaya pengine hautaki kuleta mgogoro mpya katika uteuzi wa mkurugenzi mkuu wa Benki ya Dunia.
Mwenyekiti wa hivi sasa wa Umoja wa Ulaya ambaye ni ofisa wa Luxemburg hivi karibuni alidokeza kuwa, mawaziri wa fedha wa nchi za Umoja wa Ulaya watajadili suala la uteuzi wa mkurugenzi mkuu wa Benki ya Dunia kwenye mkutano wa viongozi wa umoja huo utakaofanyika tarehe 22 na 23 ili kusuluhisha misimamo yao kuhusu suala hilo.
Idhaa ya kiswahili 2005-03-22
|