|
Mkutano wa 17 wa wakuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu (AL) ulifunguliwa tarehe 22 huko Algiers, mji mkuu wa Algeria na utafanyika kwa siku mbili. Viongozi wa nchi mbalimbali watafanya majadiliano kuhusu mageuzi ya AL, mambo ya kisasa ya dunia ya kiarabu na mchakato wa maendeleo, mchakato wa amani ya Mashariki ya Kati na hali ya Iraq, ili kulinda umoja wa dunia ya kiarabu na kuimarisha utaratibu wa shughuli za pamoja wa nchi za kiarabu.
Mwenyeji wa mkutano wa awamu iliyopita rais Ben Ali wa Tunisia kwanza alitoa hotuba, akisema kuwa sasa AL inakabiliwa na changamoto mpya, nchi za kiarabu zinapaswa kuchukua hatua za pamoja na kuhimiza maendeleo ya juhudi za waarabu kwa njia ya mageuzi.
Katibu mkuu wa AL Bw. Amr Moussa alisema kuwa kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine kwa nguvu za kisilaha kumeleta athari kwa utulivu wa sehemu ya Mashariki ya Kati, ni kutokana na juhudi za pamoja tu, ndipo nchi za kiarabu zitakapoweza kupambana na mchakato kwa hivi sasa. Alipozungumzia suala la Palestina, alisema kuwa kutimiza amani kati ya Palestina na Israel kunahitaji kutekeleza ahadi zao na kuzindua upya mchakato wa amani haraka iwezekanavyo. Bw. Amr Moussa alisisitiza kuwa katika hali ambayo Israel bado inatekeleza sera ya kuishambulia Palestina, matakwa ya amani hayatatimizwa, na amani ya Mashariki ya kati ni amani ya usawa kwa pande mbili za Israel na nchi za kiarabu.
Mwenyeji wa mkutano huo rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria alitoa hotuba akisisitiza kuwa nchi za kiarabu zinapaswa kufanya mageuzi kamili, lakini mageuzi hayo hayawezi kufanywa katika shinikizo la nchi za kigeni. Nchi za kigeni kamwe haziwezi kulazimisha pendekezo la mageuzi ya demokrasia kwa nchi za kiarabu. Aliainisha kuwa mageuzi yanaambatana na maslahi ya nchi za kiarabu ambazo zilizindua mchakato wa mageuzi mapema ya miaka kadhaa iliyopita.
Waziri wa mambo ya nje wa serikali ya muda ya Iraq Bw. Hoshyar Zebari aliyehudhuria mkutano huo alizitaka nchi za kiarabu zitoe misaada halisi kwa ukarabati wa kisiasa wa Iraq na kubadilisha msimamo wa kusubiri na kutazama nchi nyingine.
Katika mkutano huo, viongozi wa nchi mbalimbali watajadili pendekezo lililotolewa na Jordan kuhusu kuzindua upya pendekezo la amani ya waarabu. Habari zinasema kuwa nchi za kiarabu zinasisitiza katika pendekezo la amani la Jordan lililorekebishwa kuwa dunia ya kiarabu inapenda kutimiza amani na Israel, lakini sharti lake ni kuwa jeshi la Israel lazima lirejee kwenye mpaka wa kabla ya mwaka 1967, kutatua suala la wakimbizi wa Palestina kwa mujibu wa azimio nambari 194 la Baraza la Usalama na kuanzisha taifa huru la Palestina ambalo mji mkuu wake ni Jerusalem ya Mashariki.
Viongozi wa nchi 13 za kiarabu wakiwemo rais Muammar Al-Qadhafi wa Libya, Bashar Al-Assad wa Syria, mwenyekiti wa mamlaka ya utawala wa Palestina Mahmoud Abbas na rais Ghazi Al-Yawar wa serikali ya muda ya Iraq wamehudhuria mkutano huo. Wakuu wa nchi tisa nyingine muhimu zikiwemo Saudi Arabia na Lebanon hawakuhudhuria mkutano huo kutokana na sababu zao za kisiasa. Vyombo vya habari vinaona kuwa uwakilishi na heshima ya maamuzi ya mkutano huo kuhusu mambo ya kikanda itapungua sana kutokana na kukosa viongozi hao.
Idhaa ya kiswahili 2005-03-23
|