Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-23 15:05:22    
Umoja wa Ulaya wapitisha mswada wa marekebisho ya "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko"

cri
    Mkutano wa viongozi wa nchi unaofanyika huko Brussels, tarehe 22 ulipitisha mswada wa marekebisho ya "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko", hatua ambayo inaonesha kuwa mabishano ndani ya Umoja wa Ulaya kuhusu suala la marekebisho ya "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko" yamekwisha.

    Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya ambaye ni waziri mkuu wa Luxemburg Bw. Jean-Claude Juncker kwenye mkutano na waandishi wa habari mara tu baada ya kumalizika kwa mkutano wa viongozi, alisema kuwa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya walipitisha mswada huo baada ya majadiliano ya muda mfupi. Mwenyekiti wa kamati ya Ulaya Bw. Manuel Barroso kwenye mkutano huo na waandishi wa habari alisema kuwa kuafikiana kwenye suala hilo nyeti kuhusu "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko" kwa viongozi wa Umoja wa Ulaya ni mafanikio ya Ulaya, ambayo yataimarisha imani ya Ulaya.

    Ili kuhakikisha utulivu wa Euro, Umoja wa Ulaya ulitunga "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko" mwaka 1997, ambao unataka nchi zinazotumia Euro zisiwe na bajeti yenye nakisi ya zaidi ya asilimia 3 kwa mwaka ya jumla ya thamani ya uzalishaji mali wa nchi zao kwa miaka mitatu mfululizo, na madeni yao yasizidi asilimia 60 ya jumla ya thamani ya uzalishaji mali wa nchi zao, la sivyo zitapigwa faini. Kutokana na nguvu dhaifu za uhuishaji wa uchumi wa Ulaya, ilipofika mwaka    2004, nakisi ya bajeti za Ujerumani na Ufaransa zilikuwa zimezidi 3% kwa miaka mitatu mfululizo. Hivyo yalitokea mabishano miongoni mwa nchi wanachama kuhusu namna ya kutekeleza "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko". Nchi za Ufaransa, Ujerumani na Italia zinataka kutekeleza mkataba huo kwa unyumbufu, na kufikiria zaidi "hali maalumu" wakati wa kufanya uamuzi kuziadhibu nchi zilizokuwa na nakisi katika bajeti. Lakini baadhi ya nchi ndogo ikiwemo Austria, zinadai kutekeleza kwa makini "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko" bila kujali ni nchi kubwa au ndogo.

    Mawaziri wa fedha wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya walijadili mara nyingi kwenye mikutano kuhusu suala la kurekebisha "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko" na hawakufikia mwafaka kutokana na misimamo yao tofauti. Tarehe 20 mwezi huu, kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa nchi, mawaziri wa fedha wa nchi zinazotumia Euro walikubaliana kwenye mkutano kuhusu marekebisho ya "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko", ambayo yatajadiliwa kwenye mkutano wa viongozi wa nchi.

    Marekebisho ya "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko" ni matokeo ya usuluhisho wao, ambayo yanazingatia maslahi ya pande mbalimbali, hivyo yamekubaliwa na chi wanachama wa Umoja wa Ulaya. "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko" baada ya kurekebishwa utasisitiza utekelezaji wa kinyumbufu, ambao umezifurahisha baadhi ya nchi zilizozidi kiwango zikiwemo Ufaransa na Ujerumani. Rais Jacques Chirac wa Ufaransa alisema kuwa marekebisho ya mkataba yanatoa kipaumbele katika suala la maendeleo, na ni mkataba wenye hekima, unaopendeza na kuheshimiwa. Waziri wa fedha wa Ujerumani Bw. Hans Eichel amesema "Mkataba wa Utulivu na Ongezeko" uliorekebishwa unanufaisha uchumi wa Ulaya kupata maendeleo katika hali isiyoathiri utulivu, wakati kiwango kilichowekwa kuhusu 3% na 60% kwenye mkataba kimeridhisha baadhi ya nchi ndogo za Umoja wa Ulaya zinazodai kutekeleza kwa makini mkataba huo. Aidha, uwezo wa usimamizi wa kamati ya Umoja wa Ulaya kuhusu utekelezaji wa mkataba huo pia unaheshimiwa.

Idhaa ya Kiswahili