Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International Sunday    Apr 6th   2025   
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-23 15:41:57    
Meli ya " PHOENIX" ya China yafika Mombasa, Kenya

cri

Ili kumkumbuka Zheng He, msafiri mkuu wa baharini wa China katika Enzi ya Ming aliyesafiri mbali baharini miaka 600 iliyopita, meli ya "PHOENIX" ilianza safari katika tarehe 8 mwezi Agosti mwaka 2004 kutoka Taicang, mkoani Jiangsu, Kusini mwa China. Katika safari yake, meli hiyo ilipitia Brunei, Malaysia, Indonesia, Singapore, Thailand, Cambodia, Sri Lanka, Maldives, Pakistan, Iraq, Saudi Arabia na Oman, mwishoni imewasili Mombasa, Mashariki mwa Kenya.

Nohodha wa " Phoenix" ambaye pia ni baharia wa China Bw. Weng Yixuan alisema kuwa, katika safari hiyo, walikumbwa na matatizo mbalimbali. Kwa mfano tarehe 26 mwezi Desemba mwaka 2004, tetemeko la ardhi lilipotokea katika bahari ya Hindi, walikuwa wanapumzika kwenye bandari ya Blair, kwenye visiwa vya Andaman vya India. Kutokana na jitihada kubwa za mabaharia walifaulu kulinda usalama wa meli, mbali na hayo, walichangia vifaa vya masomo kwa shule ya sehemu hiyo.

Kwenye safari hii isiyo ya kawaida, walikumbwa na matatizo mengine, kwa mfano meli ilikumbwa na matatizo ya mashine. Lakini matatizo yote yaliondolewa na wakakamilisha safari nzima.

Alipomzungumzia msafiri mkuu wa baharini Zheng He, Bw. Weng Yixuan alisema kuwa, akiwa baharia, anamheshimu sana, na anajivunia sana kwa kitendo chake cha kusafiri mbali baharini mara saba. Alipozungumzia jambo hilo aliwaambia watu wa nchi za nje kuhusu utamaduni na historia ndefu ya safari ya bahari ya China. Wakati huo, msafari wa melikabu wa Zheng He ulikuwa na mamia ya melikabu na watu zaidi ya elfu 20. Baada ya miaka mingi kupita Bw. Columbus na Bw. Da Gamma walikamilisha safari zao kwa nyakati mbalimbali.

Mwezi Julai mwaka 1405, kutokana na amri ya Mfalme wa Enzi ya Ming Zhu Li, Zheng He aliongoza msafari wake wenye melikabu 208 na watu 27,800 kusafiri mbali baharini kutoka China, na baada ya miaka 28, alivuka Bahari ya Hindi kutoka ukingo wa Magharibi wa Bahari ya Pacifiki, na kufika Asia ya Magharibi na Afrika ya Mashariki. Walitembelea sehemu na nchi zaidi ya 30, mafanikio makubwa yalipatikana katika historia ya safari ya bahari duniani. Mbali na hayo alitoa mchango mkubwa katika mambo ya kidiplomasia, uchumi, utamaduni na mambo ya bahari.

mabaharia wanne wa China wafika Mombssa

mabaharia wanne na maofisa wapiga picha pamoja

Nahodha wa meli ya Phoenix aonesha bendera ya China

Balozi wa China nchini Kenya na mawaziri watatu wa Kenya wakaribisha meli ya Phoenix

Idhaa ya kiswahili 2005-03-23

© China Radio International.CRI. All Rights Reserved.
16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040