Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-24 16:22:37    
Wanamji wa Dalian wajifunza sayansi

cri

Kwenda katika Jumba la Maonesho ya Sayansi ya Uhai kufahamu siri ya uhai, kutengeneza vipuzi (toy) wanavyopenda kwenye karakana ndogo ya seremana, kushiriki mashindano ya maroboti au kusikiliza mihadhara iliyotolewa na wataalamu kuhusu maendeleo ya mwafaka kati ya nishati, uchumi na mazingira ni shughuli wanazopenda wanamji wa Dalian kuhusu sayansi.

Mwandishi wetu wa habari alifahamishwa katika Jumuia ya Sayansi ya Mji wa Dalian kuwa ili kuhimiza maendeleo ya sayansi na kuongeza ufahamu wa wanamji kuhusu sayansi, mji wa Dalian mwaka huu umeanzisha harakati ya umma inayojulikana kwa "wanamji milioni moja wajiendeleze kwa elimu ya sayansi", ambayo ni pamoja na kuchapisha vijitabu vya uenezi wa elimu ya sayansi kwa umma, ambavyo vitasambazwa katika sehemu ya mji, viwanda, kampuni na sehemu ya vijiji; kuwashirikisha wanamji katika shughuli mbalimbali za uenezi wa elimu ya sayansi; kuandaa maonesho na mihadhara ya uenezi wa elimu ya sayansi kwa wafanyakazi wa viwanda; kuwaalika wataalamu na wasomi mashuhuri wa nchini na nchi za nje kutoa mihadhara kuhusu maendeleo mwafaka kati ya nishati, uchumi na mazingira; kutoa mafunzo kuhusu elimu maalumu ya kilimo na kazi kwa wakulima, kushirikisha wakulima laki 4 kujifunza miradi ya kilimo ya teknolojia ya kimaendeleo; kuweka sehemu maalumu kwenye magazeti au kuanzisha kipindi maalumu katika radio na televisheni kuhusu uenezi wa elimu ya sayansi, kutangaza habari kuhusu sayansi na teknolojia pamoja na maendeleo yake kwa wanamji, na kuweka siku maalumu ya harakati ya uenezi wa elimu ya sayansi nchini.

Uenezi wa elimu ya sayansi kwa vijana ni moja ya shughuli muhimu katika harakati hiyo ya umma. Habari zinasema kuwa mwaka huu mji wa Dalian utafungua majumba na vituo vya uenezi wa elimu ya sayansi, maabara muhimu, sehemu za kufanyia shughuli za uenezi wa elimu ya sayansi kwenye makazi ya wanamji bila kutoza malipo kwa vijana na watoto; kushirikisha wanafunzi wa shule za sekondari na msingi katika mashindano ya teknolojia ya kisayansi na uvumbuzi. Mbali na hayo, kituo kipya cha sayansi na teknolojia cha watoto cha mji wa Dalian kitazinduliwamwezi May kwa watoto, wakati jumuia ya sayansi ya mji wa Dalian itaanzisha mashindano ya maroboti yaliyotengenezwa na vijana katika mwezi Septemba mkwaka huu.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-24