Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-25 19:46:40    
Mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika kupata maendeleo mazuri

cri
    Ushirikiano katika kilimo kati ya China na Afrika unachukua nafasi muhimu katika mkakati wa kuhimiza kampuni za China kuanzisha shughuli katika nchi za nje. Tangu yaanzishwe mageuzi na ufunguaji mlango, China imekuwa ikifanya mawasiliano na ushirikiano na nchi za Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, maofisa wa ngazi ya juu wa Wizara ya kilimo ya China na idara za kilimo za Afrika wanawasiliana zaidi. Mpaka sasa, China imepokea ujumbe wa ngazi ya juu zaidi ya 20 kutoka nchi za Afrika. manaibu mawaziri wa kilimo wa China kwa nyakati tofauti walizitembelea Misiri, Afrika ya Kusini, Kenya na Ethiopia. Pande hizo zilibadilishana uzoefu kuhusu maendeleo ya kilimo na kujadili nyanja muhimu za ushirikiano, na kuweka msingi mzuri wa ushirikiano katika sekta ya kilimo. Mpaka sasa, China imesaini mikataba kumi ya ushirikiano na Misiri, Ethiopia, Afrika ya Kusini na Msumbiji katika sekta za kilimo na uvuvi.

    Katika miaka ya hivi karibuni, Wizara ya Kilimo ya China ilifanya semina saba kuhusu utaalamu wa kilimo, na kutoa mafunzo mbalimbali ya kilimo kwa maofisa na wataalamu kutoka nchi zaidi ya 40 za Afrika.

    Tangu Semina ya mafunzo ya utaalamu wa kilimo iliyoendeshwa kwa pamoja na wizara za kilimo za China na Ethiopia kuanzishwa mwaka 2001, China imepeleka wataalam 190 nchini Ethiopia, na kuisaidia kuanzisha utaratibu wa mafunzo ya elimu. Hivi sasa semina hiyo ya nne inafanyika, na wakulima 40 wa China wanafanya kazi nchini Ethiopia. Mradi huo imesifiwa sana na serikali ya nchi hiyo.

    Aidha, China inajitahidi kuhimiza ushirikiano katika sekta ya Sierra Leone, na ilipeleka kikundi cha wataalamu wa kilimo mwezi Septemba mwaka 2002 kufanya ukaguzi kuhusu hali ya kilimo nchini humo, na kutoa mapendekezo halisi kuhusu kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kilimo kati ya nchi hizo mbili. Wakati huo huo, wizara ya kilimo ya China pia inazingatia mawasiliano ya utaalamu wa kilimo na Msumbiji. Mwezi Julai, mwaka 2004 China ilipeleka wataalamu wa korosho na kinga ya wadudu kufanya ukaguzi nchini Msumbiji na kujadili shughuli za kuanzisha ushirikiano kati ya China na Afrika, na kutoa mapendekezo ya kufanya ushirikiano kuhusu uzalishaji wa korosho na kinga ya wadudu.

    Mbali na hayo, wizara ya kilimo ya China na idara zinazohusika zilianzisha kongamano kuhusu ushirikiano na uwekezaji katika sekta ya kilimo kati ya China na Afrika mwezi Septemba, mwaka 2002, ili kufahamu hali ya Afrika, na kujadili njia mpya za kupanua eneo la ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta ya kilimo. Mwaka 2003, wakati wa Mkutano wa pili wa mawaziri wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika lilipofanyika, kampuni nyingi za kilimo za China zilishiriki kwenye Mkutano wa wafanyabiashara wa China na Afrika, na kupata fursa ya kufahamu hali ya kilimo ilivyo barani Afrika. Aidha, semina za wataalam wa kilimo zilipofanyika nchini Ethiopia na Mali, wafanyabiashara wa kilimo wa China walialikwa kushiriki kwenye kikundi cha wataalamu wa China. Licha ya kutoa mafunzo, kampuni za kilimo za China zilikubaliana na nchi za Afrika kuhusu kufanya ushirikiano katika kilimo. Mwezi Novemba, mwaka 2004, waziri mkuu wa Ethiopia alipotembelea China, alikutana na wafanyabiashara wa kilimo wa China, na kutoa fursa ya kushirikiana kuanzisha shughuli nchini Ethiopia.

    Licha ya hayo, tangu mwaka 1994, China inajitahidi kushiriki kwenye mpango maalum wa utekelezaji wa usalama wa chakula unaoanzishwa na Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, na imetia saini mkataba wa ushirikiano wa Kusini na Kusini na nchi za Afrika zikiwemo Mauritania, Ghana, Ethiopia, Mali na Nigeria, na kupeleka wataalamu wengi barani Afrika, kuzisaidia katika kuzalishaji mazao ya kilimo, na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kilimo. Kutokana na takwimu zisizokamilika, China imepeleka wataalamu wa kilimo zaidi ya 500. Katika mradi unaotekelezwa hivi karibuni nchini Nigeria, China imepeleka wataalamu 392. Aidha, China inajiandaa kuwekeana saini nchi nyingi za Afrika zikiwemo Guinea, Sierra Lenon na Gabon mkataba wa ushirikiano wa Kusini na Kusini.

    Ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta ya kilimo una historia ndefu. Kwenye mkutano wa kwanza na wa pili wa mkutano wa mawaziri wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2000 na mwaka 2003, ushirikiano wa kilimo unachukuliwa kama ni kazi muhimu katika ushirikiano kati ya China na Afrika. Ili kutekeleza mipango iliyowekwa kwenye mikutano hiyo, na kusukuma mbele ushirikiano wa kilimo kati ya China na Afrika, Wizara ya Kilimo ya China itaendelea kutafuta njia mpya za ushirikiano katika kilimo kati ya pande hizo mbili, ili kutoa mchango mpya kwa kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika nyanja zote za kilimo.

Idhaa ya Kiswahili 2005-03-25