Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-28 16:29:52    
Kwenda Xiamen kuonja chai ya Wulong

cri

Xiamen ni mji wa pwani ulioko kusini mashariki mwa China, mazingira yake murua kwa maisha, yana vivutio vingi ambavyo vinawavutia sana watalii. Ukinywa chai katika mikahawa ya chai ya huko, utahisi utamaduni wa chai unaohusiana na mtindo wa mji huo.

Kunywa chai ni desturi ya maisha kwa wakazi wa Xiamen. Kila siku baada ya kuamka, shughuli ya kwanza kwa wakazi wa huko ni kuchemsha maji ya chai. Kwa kilugha cha Minnan cha Xiamen, maana ya Chai ni "Mchele wa chai", wanaona chai ni muhimu kama ulivyo mchele. Wakazi wa Xiamen huwakirimu wageni kwa chai. Nyumbani kwenye kila familia ya huko, chai nzuri na vyombo vya chai vya aina mbalimbali huwa havikosekani, hata makampuni mengi na ofisi za serikali huwakaribisha wageni kwa chai.

Wakazi wa Xiamen wanapenda zaidi kunywa chai ya Wulong. Chai ya Wulong ina ladha nzito kuliko ile ya chai nyekundu, pia ina harufu nzuri ya chai ya kijani. Nchini Japan chai ya Wulong inasifiwa kuwa ni chai ya kurembusha uso na kusaidia afya.

Inasemekana kuwa katika enzi ya Qin ya karne ya 17 wakati wa zama za mfalme Yongzheng, katika wilaya ya Anxi mkoani Fujian, alikuwepo mkulima mmoja aliyeitwa Su Long. Kwa kuwa uso wa mkulima huyo mwenye afya nzuri ulikuwa mweusi, wanakijiji wenzake walimwita Wulong, neno Wu kwa kichina maana yake ni nyeusi, kutokana na uso wake mweusi, wenzake walimwita Wu Long badala ya Su Long. Siku moja ya majira ya mchipuko ya mwaka mmoja, Bwana Wu Long alikwenda mlimani kuchuma majani ya chai, adhuhuri alipotaka kurudi nyumbani alikutana na mnyama, akampiga risasi na kumbeba kurudi naye nyumbani. Usiku huo Bwana Wu Long na jamaa zake walipika chakula cha mnyama, walisahau kutengeneza majani ya chai aliyochuma. Asubuhi ya siku ya pili, walipotengeneza majani ya chai, waliona kuwa majani ya chai yaliyowekwa kwa usiku mmoja yalikuwa na radha nzuri bila uchungu na harufu nzuri zaidi. Baada ya hapo, Bwana Wu Long na familia yake walifanya majaribio mara kwa mara, na wakafanikiwa kutengeneza chai ya Wulong yenye sifa nzuri zaidi. Tangu hapo wilaya ya Anxi, maskani ya Bwana Wu Long ikajulikana kuwa maskani ya chai ya Wulong.

Mjini Xiamen, mikahawa ya chai ipo kila mahali. Mikahawa ya chai imejengwa kwa mitindo ya aina mbalimbali inayopendeza na ina mazingira yenye hali ya utamaduni wa chai, ambayo huwavutia sana watu, ambapo wanajisikia kuwa wanakunywa chai kwenye mikahawa kama wako nyumbani. Mmiliki wa mkahawa mdogo Bwana Wu Xiangdong alisema:

Mikahawa yetu ina chai za aina mbalimbali maarufu kutoka sehemu mbalimbali nchini China, inaweza kuwapatia raha sana watu wanaokuja kunywa chai.

Wakazi wanaokunywa chai katika mikahawa huweza kusikiliza riwaya, kupiga soga, ama kufanya mazungumzo ya biashara.

Mikahawa ya chai ya Xiamen huwapokea wageni kutoka Marekani, Uingereza, Japan, Korea ya kusini na hata nchi kadhaa za Afrika. Mtalii kutoka Uswisi Bibi Clandia Perle alisema, ukinywa chai katika mikahawa ya chai, ndipo unaweza kuona furaha ya kunywa chai.

Wakazi wa Xiamen wanajisikia raha na musterehe wakati wanapokunywa chai katika mikahawa ya chai.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-28