Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-28 16:38:36    
Hali ya Misri imekuwa ya wasiwasi

cri

Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu wa Misri. Tokea mwanzoni mwa mwaka huu, malumbano kuhusu kumchagua rais mpya kati ya watu wa sekta mbalimbali nchini Misri yamekuwa yakiendelea mpaka sasa, ambapo vyama vya upinzani vimefanya maandamano mara kwa mara kupinga Rais Hosni Mubarak asiendelee kugombea wadhifa wa urais, pia kupinga mtoto wa Rais Mubarak, Bw Jamal Mubarak asirithi kiti cha baba yake, na kuutaka utawala wa hivi sasa uongeze kasi ya mageuzi ya kisiasa.

Shirikisho la ndugu waislamu la Misri ambalo ni Jumuiya kubwa ya dini ya kiislamu tarehe 27 lilijiunga na shughuli za vyama vya upinzani, hivyo hali ya Misri ikaongezwa wasiwasi. Shirikisho hilo lilipanga kufanya maandamano makubwa tarehe 27 kuutaka utawala wa sasa uharakishe hatua za mageuzi ya kisiasa, kufuta sheria ya hali hatari inayotekelezwa tokea mwaka 1981 na kuilaani Marekani kuingilia kati mambo ya ndani ya Misri. Kutokana na athari kubwa ya shirikisho hilo, serikali ya Misri iliyapinga maandamano hayo. Aidha, ili kuzuia hali ya mambo isizidi kuwa mbaya, kikosi cha usalama cha Misri siku hiyo kiliwakamata wajumbe kumi kadhaa wa shirikisho hilo, na kufunga njia muhimu katikati ya mji zinazoelekea kwenye ofisi za Bunge la umma la Misri, ubalozi wa Marekani na Uingereza nchini humo. Lakini shirikisho hilo lilifanya maandamano kwenye uwanja uliopo katikati ya Cairo na mitaa mingine mjini humo bila kujali vikwazo vya serikali.

Shirikisho la ndugu waislamu la Misri lilianzishwa mwezi Machi mwaka 1928, nia yake ni kujenga nchi moja yenye madaraka ya Allah ikielekezwa na kanuni za msahafu wa kurani. Mwezi Julai mwaka 1952, shirikisho hilo lilipigwa marufuku kutokana na kuhusishwa na tukio la kumwua rais wa zamani Abdel Nasser, baada ya hapo lilifanya shughuli zake kisirisiri. Mwaka 1954 shirikisho hilo lilitangazwa kuwa chama cha haramu. Tarehe 6 Oktoba mwaka 1981, watu wenye siasa kali wa shirikisho hilo walihusika na tukio la kumwua rais wa zamani wa Misri Sadat aliyefanya usuluhishi na Israel. Baada ya Mubarak kushika madaraka, alichukua mbinu za kulikandamiza huku kulainisha shinikizo. Hivi sasa shirikisho hilo lina wanachama milioni moja ambao wanadhibiti jumuiya kadha wa kadha za sekta mbalimbali.

Kabla ya shirikisho hilo kuandaa maandamano, chama cha kikomunisti cha Misri, chama cha harakani za mageuzi ya Misri na chama cha siku ya kesho cha Misri vimeshaandaa maandamano mara nyingi kumtaka Mubarak aliyeshika madaraka tokea mwezi Oktoba mwaka 1981 asigombee tena wa wadhifa wa urais. Kutokana na kukabiliwa na shinikizo kutoka pande mbalimbali, Rais Mubarak anashikilia juhudi zake za kugombea tena wadhifa wa urais, huku akiahidi kujitahidi kusukuma mbele mageuzi ya kidemokrasia na kufanya juhudi za kuboresha maisha ya wananchi, tena ameagiza kurekebisha katiba ya sasa ya Misri na kuwaruhusu wagombea kadha wa kadha washiriki kwenye uchaguzi wa moja kwa moja wa urais utakaofanyika mwaka huu. Lakini wapinzani wanaona kuwa mchakato wa mageuzi ya kisiasa ya Misri unaendelea pole pole sana, hivyo shughuli za mashitaka za aina mbalimbali zinafanyika mara kwa mara.

Wachunguzi wanaona kuwa hali isiyo ya utulivu ya Misiri kwa hivi sasa inatokana na mazingira ya sehemu ya mashariki ya kati pia inatokana na malalamiko ya raia wa Misri kwa hali ilivyo ya sasa, ambao wanatarajia mageuzi yafanyike nchini humo.

Lakini wachambuzi wanadhihirisha kuwa, hivi sasa nguvu za wapinzani wa Misri bado ni dhaifu ambayo haitaweza kuwa tishio halisi dhidi ya utawala wa sasa, kama utaratibu wa uchaguzi utafanyiwa mageuzi, Mubarak bado hana taabu kuendelea kushika hatamu za serikali, aidha utawala wa sasa ukishughulikia vizuri uhusiano na shirikisho la ndugu waislamu, na kulidhibiti ipasavyo, hali ya Misri inaweza kudhibitiwa.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-28