Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-29 15:06:04    
Mwanasayansi wa kilimo wa China Bw. Jia Jizeng

cri

Bw. Jia Jizeng ni mwanasayansi anayedhamiria kubadilisha hali ya kilimo iliyo nyuma ya China. Alizaliwa mwezi Agosti mwaka 1945 katika ukoo wa wakulima mkoani Henan. Alipokuwa mtoto alipata kula magome, majani ya miti katika kipoindi ambapo China ilipokumbwa na maafa ya kimaumbile kwa miaka mitatu mfululizo tokea mwaka 1959. Alikulia vijijini na kufanya kazi za kilimo kabla ya kujiunga na chuo kikuu, alielewa vizuri nini maana ya mavuno mazuri na mabaya.

Katika miaka yake ya sekondari aliamua kujifunza sayansi ya kilimo ili kugeuza hali ya kilimo iliyo nyuma ya China. Mwaka 1965 aliposhiriki kwenye mtihani wa kujiunga na chuo kikuu, vyuo vitatu alivyoruhusiwa kuvichagua vyote ni vya ni vya kilimo, mwishowe alikuwa mwanafunzi wa idara ya kilimo katika Chuo Kikuu cha Beijing. Mwaka 1970 alipohitimu alipewa kazi ya ualimu vijijini katika mkoa wa Shanxi. Kutokana na hamu yake na sayansi ya kilimo alianza kufanya majaribio ya kuotesha mbegu za aina mpya ya ngano.

Mwaka 1979 alifanikiwa mtihani wa kujiunga na kozi ya uzamili katika taasisi ya taifa ya kilimo akisomea shahada ya pili katika utafiti wa ngano.

Katika muda wa miaka 30 alipokuwa akifanya utafiti wa kilimo siku zote akitafuta jini (gene) ya ngano inayoweza kupata ngano bora, yenye mavuno makubwa, uwezo wa kuvumilia ukame na kujikinga na ugonjwa, na mafanikio ya utafiti wake uliongoza duniani. Mbegu aliyopata imeongeza mavuno kwa asilimia 5 hadi 30. Kwa msisimko alisema kuwa majukumu ya wanasayansi ya kilimo ni kuwapatia wakulima mbegu zenye jeni bora ili wakulima wapate mavuno makubwa kwa gharama ndogo.

Kutokana na ufanisi wake wa utafiti wa sayansi aliwahi kupewa tuzo za aina mbalimbali za serikali na kupata sifa ya mwanasayansi bora wa China.

Bw. Jia Jizeng siku zote alikuwa akifanya utafiti wa jeni bora kutoka kwenye mbegu za aina mbalimbali. Katika utafiti huo ameelewa kuwa China ni nchi yenye utajiri mkubwa wa aina nyingi za jeni, na pia anaelewa kuwa hivi sasa duniani kuna mashindano makali ya jeni bora za mbegu. Nchi zilizoendelea na makampuni makubwa ya kimataifa yamekuwa yakijitahidi kupata jeni bora na kuzifanya "clone", ili kumiliki kwa hakimiliki na kuziuzia hakimiliki nchi zinazoendelea kwa bei kubwa. Shirika moja la Marekani limeanza kuomba hakimiliki ya jeni bora iliyopatikana kutoka kunde soya za China, kama hakimiliki ikiidhinishwa, wakulima wa mazao ya kunde soya pengine watashitakiwa kukiuka hakimiliki na kunde hizo za China hazitaweza kuuzwa katika nchi za nje. Hali kama hiyo pia imetokea katika ngano, mahindi na mpunga.

Mwaka 1990 alienda Uingereza kusoma zaidi katika maabara ya Chuo Kikuu cha Cambridge. Kutokana na juhudi zake ilikuwa ni kawaida kwake kufanya majaribio mpaka siku ya pili alfajiri.

Mwaka 1992 kipindi chake katika chuo hicho cha Uingereza kilimalizika, wakati huo alikuwa na machaguo matatu, yaani kurudi nyumbani China, kuendelea na masomo ya kupata shahada ya daktari na kubaki nchini Uingereza kufanya kazi. Ingawa kwa Bw. Jia Jizeng mwenye shahada ya pili na miaka yake ya kufanya kazi katika maabara ya chuo maarufu cha Uingereza hakuwa na shida yoyote kupata kazi nchini humo, lakini aliamua kurudi nyumbani.

Bw. Jia Jizeng alisema, "Nikiwa mwanasayansi wa kilimo jukumu langu ni kuipatia China nafasi ya mbele duniani katika nyanja ya utafiti wa kilimo. Lengo letu ni kuifanya China iwe "benki ya jeni" inayowatajirisha wakulima wa China.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-29