Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-30 14:21:45    
Ariel Sharon aondoa vikwazo kwa ajili ya kutekeleza mpango wa upande mmoja

cri

Tarehe 29 bunge la Israel lilipitisha bajeti ya mwaka 2005 iliyowasilishwa na serikali ya Israel, hivyo baraza la serikali lilisalimika bila kuvunjwa, na vikwazo vya kutekeleza mpango wa upande mmoja wa Sharon vimeondolewa.

Jioni katika siku hiyo bunge la Israel lilipigia kura bajeti ya mwaka 2005, na kupitisha kwa kura za ndio 58, kura za hapana 36 na kura moja iliyoharibika. Kutokana na katiba ya Israel, kama bajeti hiyo isingepitishwa kabla ya tarehe 31, Sharon angelazimika kuondoka madarakani na kufanya uchaguzi mkuu kabla ya wakati, na mpango wa upande mmoja uliotolewa na Sharon ungefutwa. Vyombo vya habari vya Israel vinaona kuwa kupitishwa kwa bajeti hiyo kuna maana ya kuwa wapinzani wa mpango wa upande mmoja wameshindwa kabisa na hawataweza "kuinuka" tena katika siasa na sheria.

Tokea mwaka jana, wapinzani wa mpango wa upande mmoja walikuwa wakijitahidi kila wawezavyo ili kuua mpango huo "kabla ya kuzaliwa". Kwa ujumla walitumia mbinu mbili, moja ni kutaka mpango huo upigiwe kura na wananchi wote ili waahishirishe utekelezaji kwa kutumia taratibu zilizotatanisha za sheria ili kujipatia muda "kuuzika" mpango huo. Lakini tarehe 28 pendekezo la kupigiwa kura lilifutwa kwa kura nyingi katika bunge. Pamoja na pendekezo la kupigiwa kura na wananchi, wapinzani wa mpango huo na hasa "kikundi cha waasi" ndani ya kundi la wapinzani kilijitahidi kuzuia bajeti ambayo kwa kweli haina uhusiano mkubwa na mpango wa upande mmoja isipitishwe ili kuilazimisha serikali ya Sharon kubomoka pamoja na mpango huo wa upande mmoja.

Ili bajeti iweze kupitishwa, Sharon alikuwa mkarimu wa "kutanda barabara kwa fedha". Aliahidi kusaidia chama kidogo cha upinzani kwa dola za Marekani milioni 640 kwa ajili ya shughuli za shule iliyo chini ya chama hicho. Tarehe 26 Sharon aliahidi kukitengea dola za Marekani milioni 160 chama kikubwa cha upinzani kutoka bajeti. Kadhalika, aliahidi kuongeza fedha kwa jaili ya wanafunzi wa vyuo vikuu, askari wa jeshi la ulinzi na wasanii. Isitoshe, aliahidi pia kwa Chama cha Waarabu kwa dola za Marekani milioni 160 ili kuhakikisha chama hicho hakitapigia bajeti kura ya hapana. Baada ya shughuli zote za ukarimu huo, mwishowe bajeti yake iliungwa mkono na watu wengi, na imepitishwa katika bunge.

Hivi sasa, ingawa wapinzani wa mpango wa upande mmoja wameshindwa kabisa lakini wanaendelea na "ukaidi" wao. Walisema, baadaye watahamisha mapambano dhidi ya Sharon kutoka bunge hadi "barabarani", watazuia utekelezaji wa mpango huo kwa kufanya maandamano makubwa na hata kutumia nguvu. Hivi sasa serikali ya Israel tayari imetoa taarifa kwa wakazi 8500 wa sehemu ya Gaza ikiwataka waondoke kutoka kwenye makazi yao kabla ya mwisho wa mwezi Julai, na kuwaahidi kuwa serikali itawapa fidia. Imefahamika kuwa hadi sasa familia 66 za wakazi wa huko wamekubali kuondoka kwa hiyari baada ya kukubali fidia ya serikali. Kutokana na siku ya mwisho kukaribia, wapinzani hakika watazidi watafanya vitendo vyao vya upinzani. Imefahamika kuwa katika wiki kadhaa zilizopita Wayahudi mia kadhaa ambao wamehamia huko Gaza wakiwatia moyo watu wanaokataa kuondoka kutoka sehemu ya Gaza.

Kwa hiyo, ingawa bunge la Israel limefuta pendekezo la mpango wa upande mmoja kupigiwa kura na wananchi na limepitisha bajeti ya mwaka 2005, lakini utekekezaji wa mpango huo hautakuwa shwari.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-30