Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-30 18:26:20    
Kuchemsha vipande vya nyama ya nguruwe

cri

Mahitaji

Nyama ya nguruwe gramu 300, yai, chumvi, M.S.G, vipande vya tangawizi, vitunguu maji na vitunguu saumu, wanga, sosi ya pilipili, pilipili manga, siki, mvinyo wa kupikia, mboga, na mafuta ya kupikia.

Njia

1. kata nyama ya nguruwe iwe vipande, vipakue ndani ya bakuli moja, tia chumvi, wanga, na yai lililokorogwa, koroga, na chemsha mboga na ipakue weka ndani ya bakuli kubwa.

2.tia mafuta kwenye sufuria, pasha moto hadi yawe na joto la nyuzi 60, tia vipande vya tangawizi, vitunguu maji na vitunguu saumu, na sosi ya pilipili, korogakoroga, mimina maji ya wanga, siki, mvinyo wa kupikia, M.S.G, koroga, halafu mimina maji, chemsha kwa dakika 5, tia vipande vya nyama ya nguruwe, chemsha tena, vipakue ndani ya bakuli kubwa lenye mboga, tia pilipili manga, halafu pasha moto tena, chemsha mafuta kidogo kisha yamimine kwenye vipande vya nyama ya nguruwe. Mpaka hapo kitoweo hiki kitakuwa tayari kuliwa.