Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili ya CRI
China Radio International
China
Dunia
(GMT+08:00) 2005-03-31 20:10:23    
Mabadiliko mapya yatokea nchini Kyrgyzstan

cri

Mabadiliko mapya yametokea hivi karibuni nchini Kyrgyzstan. Rais Askar Akayev wa nchi hiyo aliyekwenda nchini Russia amebadilisha msimamo wa kushikilia kutojiuzulu wadhifa wa urais na kueleza kujiuzulu kwa masharti. Wakati huo huo, spika wa bunge jipya Bw. Omurbek Tekebayev ambaye pia ni kiongozi wa makundi ya upinzani alieleza kupenda kuzungumza na Bw. Akayev.

Askar Akayev tarehe 29 alieleza kupitia kituo cha televisheni cha Russia kuwa kama atapewa dhamana ya usalama kwa kuambatana na utaratibu wa kisheria, anaweza kujiuzulu urais kabla ya wakati uliopangwa. Pia alieleza matumaini yake kuwa anapenda kuzungumza na makundi ya upinzani, lakini sasa anaweza tu kuzungumza na spika wa bunge jipya Omurbek Tekebayev ambaye pia ni kiongozi halali pekee nchini Kyrgyzstan.

Tarehe 30, Tekebayev aliitikia msimamo wa Akayev, akisema kuwa Akayev kujiuzulu kwa hiari wadhifa wa urais ni hatua nzuri kabisa ya kuepusha na mgogoro wa hivi sasa. Pia alieleza kuwa bunge lake litaunda kamati moja kushughulikia kuzungumza na Akayev.

Mabadiliko makubwa mfululizo yaliyotokea katika utawala wa Kyrgyzstan yalisababishwa na kutoridhika na matokeo ya uchaguzi wa bunge kwa makundi ya upinzani. Mwanzoni, Akayev na viongozi wa makundi hayo hawakuzungumza, lakini hali ya hivi sasa inaonesha kuwa uhusiano wa kukabiliana kati ya pande hizo mbili umetulia, jambo hilo hakika litafanya juhudi  kutuliza hali ya nchi hiyo.

Baada ya kuzushwa kwa "mapinduzi ya rangi" nchini Kyrgyzstan, mabadiliko makubwa yalitokea nchini humo. kutokana na Akayev kwenda nchini Russia, makundi ya upinzani pia yana wasiwasi kuwa mgogoro wa nchi hiyo utaendelea na kusababisha kutodhibiti hali ya nchi hiyo, hivyo yanataka kutafuta msingi halali kwa vitendo vyao. Katika hali hiyo, bunge jipya kuapishwa kushika madaraka kumekuwa chaguo zuri wa kuonesha uhalali wa utawala mpya.

Sasa viongozi wa makundi ya upinzani wanaosimamia mamlaka ya taifa hawakiri kuwa walipanga "mapinduzi" ya kuipindua serikali ya Akayev. Kaimu rais Kurmanbek Bakiyev tarehe 30 alitoa hotuba kupitia kituo cha televisheni cha nchi hiyo akieleza kuwa kuna watu nchini humo ambao walikusudia kuzusha

Mgogoro. Wakati huo, vyombo vya habari vinaona kuwa maoni tofauti kati ya kaimu rais Bakiyev na makamu wa rais Feliks Kulov yamesababisha mafarakano katika makundi ya upinzani.

Wachambuzi wanaona kuwa mgogoro huo wa kisiasa nchini humo umesababishwa na sababu mbalimbali. Kati yao, kuna athari za nguvu za kigeni, ambapo pia ni matokeo ya lazima kuhusu kutotatuliwa kwa muda mrefu kwa matatizo ya kisiasa na kiuchumi nchini humo. Kutokana na hali hiyo yenye mazonge, maendeleo ya hali ya Kyrgyzstan hayatabiriki. Watu wanatumai kuwa nguvu za kigeni hazitaingilia kati mambo ya ndani ya nchi hiyo na makundi mbalimbali ya nchi hiyo pia yapaswa kuzingatia mustakbali wa nchi hiyo, kufanya mazungumzo na kutafuta maafikiano ya taifa.

Idhaa ya kiswahili 2005-03-31